Na Mwajuma Juma, Zanzibar
WAZIRI wa Katiba na Sheria Zanzibar, Bw. Abubakar Khamis Bakar amekiri kuwa Katiba ya Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinagongana.Hivyo, alisema
kutokana na hali hiyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano inapaswa kuangaliwa upya kwa lengo la kuondosha utata unaojitokeza hasa kwa kuanisha histoia ya nchi mbili zilizounda Muungano.
Hayo aliyaeleza katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi jana, alipokuwa akijibu suali la mwakilishi wa jimbo la Chaani bw. Issa Jecha Simai, ambaye alitaka kujua wananchi wafuate katiba ipi kati ya mbili hizo kutokana na kuwa zimegongana kiuandishi.
Alisema kuwa ni kweli kifungu namba 2(a) cha katiba ya Zanzibar kinampa uwezo Rais wa Zanzibar kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maneo mengine kwa kufata utaratibu uliowekwa na sheria na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi na pia ibara ya 2(2) ya Katiba ya Jamhuri inampa uwezo Rais wa Muungano kuigawa Jamhuri ya Muungano katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu lakini kwa kwa Zanzibar alilazimika kushauriana na Rais wa Zanzibar.
Ni kweli kuwa katiba hizi mbili zinazogongana kiuandishi na hivyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano inapaswa kuangaliwa upya ili kuondoa utata huo hasa katika kuainsisha historia ya nchi mbili hizi na kuainisha mamlaka na majukumu ya
serikali hizi mbili kulingana na Mambo ya Muungano na yasiyokuwa ya Muungano kwa kila upande, alisema.
Aidha alisema kwamba upande wa Mambo ya Muungano, katiba inayopaswa kufuatwa ni ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Mambo Yasiyohusu Muungano, kwa Zanzibar, katiba inayopaswa kufuatwa ni ile ya Zanzibar ya mwaka 1984 kama ilivyorekebishwa kwa nyakati mbalimbali.
Hata hivyo, alisema kuwa Marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 yamezingatia zaidi maamuzi ya wananchi kuhusu mfumo mpya wa serikali, ambao utendaji wake utafanywa katika utaratibu utakaohakikisha kuendelezwa
kw umoja nchini kwa lengo la kufikia demokrasia.
Wakati umefika kwa Watanzania kujua aina ya muungano tulionao. Muungano wa mwaka 1964 ulikuwa tufauti na tulionao sasa hivi. Hili tatizo la kugongana kwa katiba linapaswa siyo tu kurekebishwa bali na muungano wenyewe. Kwa kipindi hiki sijui mimi niliyeshuhudia muungano tangu mwanzo wake kuna kitu gani kilichobaki ambacho Rais wa Jamhuri anakifanya huko visiwani. Nchi nyingi zikiungana kunakuwepo serikali moja, au serikali moja yenye serikali ndogondogo za majimbo. Nafikuri hata sisi umefika wakati kama huo kama tunataka kuendelea na muungano huu wetu mzuri. Sioni kama huu wa serikali mbili tulionao utatufikisha mbali.
ReplyDeletemuunguano ni kichaka fulani cha ulaji, sioni faida yoyote ya muungano zaidi ya watawala wetu kuwa na vyeo vingi na kurithishana madaraka, kila siku zinavyokwenda ndio upande mmoja wa mungano uanapoainisha tofauiti za kujitenga na kudai mamlaka zaidi, na sifa lukuki za muungano ooh muungano wa kipekee duniani, unaonesha umoja etc, kama ni wa kipekee upekee ni wakufoji, upekee wa kijipendekeza tuu, hakuna upekee wowote. Bora uvunjike tuu kila upande ubaki na ishu zake sio sifa za kijinga.
ReplyDeleteMuungano ulipo haufai na umepitwa na wakati. Mbinu za CCM kufanya Serikali moja ni sawa na kukaribisha umwagaji wa damu.
ReplyDeleteSuluhisho: Vunja Muungano na kila upande umuheshimu jirani yake. Vyenginevyo,uweko Muungano kama wa nchi za Ulaya. Full control kwa kila nchi except few things chini ya Raisi wa Heshima.