Na Tumaini Makene
CHAMA Cha Wananchi (CUF) kimepata pigo baada ya kada wake maarufu Profesa Abdallah Safari, kutangaza rasmi kujiondoa katika chama hicho huku
akitaja sababu kuu kuwa ni chama hicho kukosa mwelekeo na kupoteza mvuto kwa watanzania.
Akitangaza uamuzi wake Dar es Slaam jana, Prof. Safari alisema CUF imepoteza mwelekeo wa kuwa chama cha kitaifa hali iliyoifanya ipoteze mvuto hivyo haoni sababu ya kuendelea kuwa mwanchama bila matarajoo ya kufikia lengo la kuwakomboa watanzania.
Alitaja moja ya mambo yaliyomhuzunisha ndani ya CUF kuwa ni kitendo cha kuzomewa na kubezwa wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho mwaka 2009 licha ya yeye mwenyewe kufukuzwa serikalini kwa ajili ya chama hicho.
Alisema licha ya hali hiyo lakini yeye kama msomi aliamua kuvumilia kwa miaka miwili kabla ya kufikia uamuzi huo wa kujitoa ili kutathmini kama kutakuwa na mabadiliko au la.
Alisema ukosefu wa demokrasia ndani ya CUF ni mkubwa na kwamba zipo nafasi za uongozi zinazoonekana kuwa za kisultani au kifalme na kwamba mtu mwingine akigombea anaonekana wa ajabu hivyo kusakamwa.
"Nimewaita kutangaza rasmi kuwa mimi si mwanachama wa CUF tena, nahisi CUF kimekosa mwelekeo wa chama cha kitaifa. Wakati ule vuguvugu la vyama vingi likianza nchini nilikuwa Uingereza, nilivyorudi mwaka 1995 mimi na mke wangu tulijiunga na CUF bila kusita kwa sababu mbili.
"Kwanza jina la chama Cha Wananchi, yaani chama cha watu wenyewe, pia kauli mbiu yake ya haki sawa kwa wote...safi sana maana hata kila dini duniani inalilia haki kwa watu wote...nilitarajia kuona haki sawa kwa wote kweli, ili tuisimamie kwa nguvu," alisema Prof. Safari.
Alisema wakati huo CUF ilikuwa na nguvu ikiwemo safu yake ya uongozi waandamizi kutisha na kuvutia huku akiwataja baadhi ya viongozi wa wakati huo kuwa ni Bw. James Mapalala, Bw. Msobi Mageni, Bw. Wilfred Lwakatare.
Aliwataja wengine kuwa ni Bw. Akwilombe Shaibu, Bw. mwarobaini ule, Bw. kijana Namata, Bw. Kassanga Tumbo, Bw. Ramadhan Mzee, Bw. Kamara Kusupa pamoja na Bi. Jidawi, Maghimbi ambao wote wamejiondoa katika chama hicho.
Alisema tangu chama hicho kiondokewe na watu madhubuti kama hao hakuna jitihada zilizofanyika kupata watu wengine na kwamba chama cha siasa ni sawa na timu ya mpira inayotakiwa kuweka imara safu yake kuanzia ulinzi, kiungo na ushambuliaji ili ipate ushindi katika mechi.
Licha ya chama hicho kupotea uelekeo Prof. Safari alitaja sababu ya pili ya kujiondoa CUF kuwa ni kutokuwepo kwa demokrasia ndani ya chama hicho na kusisitiza kuwa yeye si mtu wa kwanza kulalamikia hali hiyo.
"Nilipogombea nafasi ya mwenyekiti katika uchaguzi mkuu uliopita nilioneshwa uhasama kama kwamba sitakiwi, nikaulizwa maswali ya kipuuzi kabisa," alidai Prof. Safari. Bado hata Hamad (Rashid Mohamed) aliniuliza swali la kipuuzi kabisa eti nini mchango wangu kwa chama...mimi nimefukuzwa kazi yangu ya maana serikalini kwa sababu ya kumbeba Lipumba ndani ya gari yangu."
Alisema katika mkutano huo mkuu taratibu za demokrasia kwa ajili ya uchaguzi huru na wa haki zilifinyangwa kiasi cha wajumbe kupiga kura huku wakipiga soga na kujadiliana mgombea yupi apigiwe kura.
"Nikaitwa pandikizi la CCM, ulikuwa upuuzi...sasa huwezi kudai demokrasia katika ngazi ya juu wakati ndani ya chama mmeshindwa kuitimiza."alisema Prof. Safari
Aliweka wazi machungu yake kwa CUF kushindwa kutambua mchango wake katika kesi kadhaa bila malipo pamoja na baba yake kufariki dunia kwa mshituko baada ya yeye kufukuzwa kazi kufuatia uamuzi wake wa kujiunga na chama hicho.
Hata hivyo msomi huyo aliweka wazi kuwa uamuzi huo si mwisho wake katika siasa na kuongeza kuwa ataendelea kuchangia kupitia njia nyingine katika mijadala ya kitaifa.
Alitaja sababu ya tatu ya kujiondoa katika chama hicho kuwa ni tofauti ya kimtazamo ya kushiriki chaguzi bila kuwa na tume huru ya uchaguzi.
"Wenzangu wamekuwa na msimamo kuwa si lazima kuwa na tume huru ya uchaguzi, wamekuwa na msemo mmoja kuwa usiposhiriki uchaguzi ni sawa na kumwachia nguruwe shamba la mihogo ale peke yake.
"Mbona nguruwe ameshakula mpaka hata mti, mbegu yenyewe ya mhogo, nimekuwa nikisema kushiriki uchaguzi bila tume huru ya uchaguzi ni kuwapeleka wananchi machinjioni,"alisema.
Prof. Safari ambaye kitaaluma ni mwanasheria aliyebobea katika masuala ya ushahidi alisema kutokana na mchango wake mkubwa katika CUF hakutarajia kama wanachama wenzake wangembeza na kumdharau baada ya kuamua kugombea uongozi wa juu.
ulichokifanya ni sawa kwani kila mtu nanauhuru wake, endelea kutoa mchango wako wa upeo wako wa elimu katika mihadhara. hata mimi naunga mkono uamuzi wako.
ReplyDeletemimi sikutegemea kama CUF wangekua mgando wa mawazo kuwa anayepingana na Lipumba au Maalim Seifu basi ni msaliti profesa Safari hongera kwa uamuzi huo acha CUF iwafie wenyewe
ReplyDeletekaribu chadema prof
ReplyDeleteProf. Safari pole kwa yaliyokukuta lakini utambuwe kwamba washindanao wawili mmoja hushindwa, wala usisubiri mpaka unaposhindwa ndio ukaanza kutoa aibu ya mwenzako kila mtu atasema ni machungu tu kwa sababu umeshindwa. Tumia elimu yako kuendelea na ujenzi wa Taifa tafuta chama unachokipenda ugombee nafasi yoyote au subiri tupate Katiba mpya ugombee kama mgombea binafsi.
ReplyDeleteCUF wamekosa utu na utshi wakisiasa,mtu aliyejitoa kwaajili yao leo kaonekana kama msaliti ndani ya chama,nakuunga mkono Prof.Safari..pole sana kwa kumpoteza baba yako pamoja na kazi yako,naamini mwenyezi MUNGU ambaye ni mwingi wa rehema atakusaidia katika maisha yako..kiukweli inauma sana,ila CUF ya lo sio ile ya 1995 wala 2000 wameishiwa mbinu na hawajui wafanye nini!wakati CCm ikijiingiza kwenye mwafaka nilijua wameshajipima wakajiona hakuna mtu wakusimama Zanzibar,wakawadanganya CUF ili watakapochakachua matokeo washindwe kulalamika..iweje Maalim Seif apate 49% alafu Lipumba apate karibu 60% na CUF wamekaa kimya wameshindwa kutetea udhalimi juu ya wazanzibar na tanzania kwa ujumla..
ReplyDeleteHongera sana Prof.Safari, CUF ni kama imefika mwisho wake, kitendo cha kukubali kufunga ndoa na CCM kilikuwa ni kupoteza dira, hakuna upinzani wowote from CUF! laiti wangekumbuka jinsi walivyotuhumiwa mwaka 2005 karibia na uchaguzi kuwa limekamatwa kontena lililobeba visu na kontena lilikuwa mali ya CUF! wangeiogopa CCM kama ukoma! lakini kwakuwa viongozi wake ni short sighted hawajaweza kuona hatima ya chama chao in nearest future... CUF will undergo natural death.. Prof.Safari karibu sana CHADEMA chama chenya dira ya kweli na uongozi thabiti, karibu ulete challenge zenye manufaa kwa Tanzania na chama kwa ujumla, ushauri na mawazo yote yenye kuleta Tanzania mpya, tunakuahidi ushiruikiano wa kweli usio na unafiki.Pamoja tutajenga Tanzania mpya!
ReplyDeleteMBINU YA KUJENGA CHAMA INATEGEMEANA NA WAKATI HUSIKA,MATUKIO NA MTAZAMO WA ULIMWENGU KWA WAKATI HUSIKA. CUF kama chama chochote hakina budi kingefanyaje kama si kuingia seriklini kwani bado lipi ambalo ccm hawajalifanya hawajaua hawa? kama ni kususa CUF hawajasusa? nini ilikuwa faida.Mmesahau unafiki wa vyama vyengine wakati cuf inataka tume huru na katiba mpya yale maandamano kila siku jee? kuna chama chochote kilichoweka weka historia kama CUF ktk kudai haki za wananchi?
ReplyDeletemimi naamini kuna mgongano wa mawazo tu na hili si ndani ya CUF pekee cha msingi watu watambue wajibu wao na kwamba suala la mabadiliko si mchezo.
Wasia kwa Prof Safari ikiwa lengo ni kuwatumikia wa tz nafasi zipo au ikiwa issue ni CUF tu basi hata aje kiongozi gani kwa mazingira ya siasa za hapa bila mabadiliko ya katiba hakuna kitu hii yote ni athari ya mgando kuanzia ccm hadi tlp hujawasikia chadema wakilalamikiwa kwa umajimbo,udini nk? mawazo ya mtu yasipwane lengo kuu la chama nionavyo CUF hawajakosea ni suala la wakati tu
Nafikiri CUF ipo juu, ktk vyama vya upinzani Tanzania, Prof. Safari ana uchu wa Madaraka, muache aende huko anakofikiria atapata uongozi wa juu. Unda chama chako basi.
ReplyDeleteProf. Safari nakuamini kuwa wewe ni mtu Makini sana, Ila inaonyesha imekuuma sana kushindwa katika uchaguzi mwaka 2009. Bw. Wilfred LwakatareAlihama CUF baada ya kuondolewa kwenye uongozi, Fatuma Maghibi baada ya kukosa kuchaguliwa kuwa Mbunge kwenye Kura za Maoni. Ipo haja ya kutambua kuwa Chama kinakuwa kizuri ukipata kile unachokihitaji, ukikosa kinakuwa kibaya. Kulikuwa hakuna haja ya kuita waandishi kueleza yooote yaliyokupa. Mbona ulipokuwa mwanachama hukuweza kuwaita waandishi na kuelezea mikasa iliyokupata. Siasa ni uvumilivu.Ungeweza tu kwenda pale Buguruni kweneye Makao makuu ya Chama ukarudisha kadi ingetosha. Hivi unatarajia Watanzania wataelewana kuwa hukutendewa haki au ulikosa uongozi ndio maana unalalamika. inawezekama kweli hukuwa na mchango ndio maana hata katibu mkuu alikuuliza unamchango gani? ingawa mwenyewe unasema swali la kijinga. ungetafakari nini umewafanyia wanachama wenzio hadi wakakuzomea. Tusipende kung'ang'ania madaraka. Taaruma yako ni nzuri inaweza kutoka mchango mkubwa kwa jamii ambayo inahitaji msaada wa kisheria. fungua Taasisi ka vile TAMWA ukatoka ajira kwa vijana. Pole sana Prof
ReplyDeleteMimi ni yule yule Hafidh mpenda mageuzi kutoka Zanzibar.Napenda kuchangia katika Hoja hii ya Prof Safari kuachia uanachama kutoka CUF.Inaonyesha hoja za Prof hazina mantiki wala haitaji Degree kuona hili.
ReplyDelete1) Anasema CUF kimekosa utaifa ! ni chama kilicho base Zanzibar tu na kinaonekana kama chama cha wapemba !!
Huyu Prof kweli ?! mana anaongea pumba tupu!! ok napangua hoja hizi za kitoto sasa.
Mimi nathubutu kusema CUF ni chama chenye utaifa kwa Tanzania kwa sababu hizi.
a) ni chama pekee cha upinzani chenye wabunge kutoka pande tatu za Jamhuri ya muungano wa Tanzania- Unguja ,Pemba na Tanganyika.
b) M/Kiti ni kutoka Tanganyika ,Katibu mkuu kutoka Pemba na N/K/Mkuu kutoka Unguja ,(Lipumba ,Seif na Duni)
Hakuna chama chochote cha upinzani chenye mfumo kama huu kama kipo mtu aweke mezani hapa!!
Prof amewataja Viongozi wa Cuf waliondoka !! lakini cha kushangaza hakutaja sababu zilizowafanya waondoke !! tunapenda kumwambia Prof kua ukiwa msaliti au una element za usaliti basi utakwenda na maji tuu huwezi kuachwa ukivuruge chama . Hta huyu Seif aliponekana anakua msaliti wanachama walimbadilishia kibao kama una kumbukumbu nzuri maalim Sef ameshaonja joto ya jiwe mara kadhaa ya wannachama ktk viunga vya darajani akaokolewa na walinzi wake sasa na yeye angesema najivua watu wangemuambia nenda baba njia nyeupe lkn alisoma alama za wakati akawa mvumilivu akaendelea na jahazi ndio mana yupo. hii ndio CUF.
wANACHADEMA MSIROPOKWE TUU WEKENI HOJA MEZANI ILI TUJADILI SIO KULETA UBAGUZI NA KUPONDA BILA SABABU ZA MSINGI.
HeHEHe!! Prof tulikujua kuwa wewe ni kinyonga au prof lipumba kakuzidi kete. Prof safali njema uendako
ReplyDeleteHuyo anaejiita Hafidh mpenda mageuzi mbona anatushangaza? Tanzania sasa ina pande tatu? Ama kweli dhambi ya ubaguzi ishaanza kuwatafuna.Namnukuu " Cuf ni chama pekee cha upinzani chenye wabunge kutoka pande tatu za Jamhuri ya muungano wa Tanzania- Unguja ,Pemba na Tanganyika" Hawa jamaa bila muungano watachinjana wapemba na waunguja.
ReplyDeleteDu! kumbe Prof. umekifia sana chama cha wananchi CUF. Pole sana
ReplyDeleteMimi ni yule yule Hafidh mpenda mageuzi kutoka Zanzibar.napenda nimuweke sawa ndugu yangu anaeshangaa kwa kusema Tanzania ina pande tatu.1) Ndugu yangu napenda ukijibu hoja au ukileta hoja ni vyema ukaweka Jina kama ninavyoweka mimi kwa sababu ntapenda nikujibu kwa jina lako ndio ungwana.
ReplyDeleteNarejea tena kua maelezo nliotoa sijayakosea hata chembe maana kimuundo Tanzania ni muungano wa nchi mbili Zanzibar na Tanganyika (Hili Halikwepeki) na sio dhambi kusema hivi maana hata tukisherehekea Muungano wetu tunasema kua ni muungano wa Zanzibar na Tanganyika . sasa ikiwa ndugu atakubaliana na mimi kwa hili basi na unaposema Zanzibar maana yake ni visiwa viwili Unguja na Pemba,sasa ndugu yangu unashangaa nini sasa hapo!! na ndio maana wawakilishi wa CUF wanatoka sehemu hizi tatu za jamhuri ya muungano wa Tanzania . ndugu yangu kusema hivi haina maana huu ni ubaguzi !! la hasha sehemu hizi ni zaki Geografia kwa hiyo huwezi kuziunganisha mpaka kiama kitasimama. hata leo hii tutangaze kua tunafuta Zanzibar (kitu amabacho sifikirii kuwepo) basi sehemu hizi zitabakia pale pale kua tatu amabayo ni mapande makubwa ya ardhi.
Ndugu yangu bado hujajibu hoja niliweka mezani bado kilichokuchanganya wewe ni fikra na mawazo mgando.huna upeo wa kuchambua mambo.
NAREJEA TENA KAMA KUNA MTU ANAHOJA ZA MSINGI BASI WEKA MEZANI TUCHANGIE.
Hafidhi mbona unaongea pumba hivyo? Kwa mantiki yako kutakuwa na pande zaidi ya tatu maana kuna visiwa vya ukerewe, mafya, rubondo na kadhalika ! Acheni ubaguzi huko zenji nyie ni nchi mmoja (au mkoa mmoja) japo mwatenganishwa na maji! Kwa mantiki yako Zanzibar Ina unguja, Pemba, tumbatu, changuu n k.? Acha ujinga wa kiunguja!
ReplyDeleteProfesa Safari nakushauri uende Chadema. Hawana wasomi sana hasa katika ngazi mbalimbali za juu, kumbuka mwaka wa 2010 walimsimamisha mtu wa darasa la 7 kuwa mgombea mwenza wa rais! Unahitajika sana chadema, achana na hao CUF waendelee kunywa kahawa na kashata barazani, wewe jiunge na watu makini wenye nia ya kweli ya kuleta mabadiliko kwa wote.
ReplyDeleteMimi ni yule yule Hafidh kutoka Zanzibar.Ni kweli akili ni nywele kila mtu ana zake ! huu msemo wa wazee wetu una maana. Ndugu yangu kaponda hoja yangu lakini cha kushangaza hajatoa hajajenga hoja ya msingi , sababu zake eti Mafya ,tumabatu na Changuu !! hapa ndipo ninapoamini kwamba baadhi ya watanzania hawajui kutafautisha pumba na mchele safi!!au niseme hajaelewa labda ! mimi sikusema Zanzibar ni nchi mbili la hasha! ila nimesema unaposema Zanzibar manayake ni Visiwa viwili vikuu Unguja na Pemba.huu ndio ukweli hata historia yetu inasema hivi ndugu yangu huwezi kuifuta.hakuna asiyejua kama Zanzibar ni nchi moja kwa sababu tangu enzi na enzi hakujawahi kua na muungano wa visiwa hivi - kwa hiyo wakaazi wa Zanzibar nikiwa na maana Unguja na Pemba ni ndugu na huwezi kuwatenganisha naomba uelewe hilo.Historia yetu haijawahi kutaja Zanzibar ni mkusanyiko wa visiwa vingi vidogo vidogo kama vile ulotaja wewe kikiwamo Tumbatu,Changuu,Mnemba,Kojani,Uzi NK.
ReplyDeleteWasi wasi wangu ni kwamba huijui vizuri historia ya Zanzibar ! unakurupuka tuu kutoa maoni sasa ni vyema ukaisoma halafu ndio utoe Comments zako kwa kujenga hoja zenye mantiki.
Karibu tena na weka hoja mezani bado hamjajibu.
Hafidh utapata tabu bure na hao watu,CUF imekosa mwelekeo na mvuto kwa vipi? Cuf ndio chama cha pili katika chaguzi za wenyeviti wa vijiji na safari hii wameongeza wabunge kuliko alipokuwepo Bw Safari,kama umetoka chama ondoka tu huna sababu ya kukiponda.
ReplyDelete