Na Tumaini Makene
SAKATA la Kampuni 'tata' ya Dowans inayotakiwa kulipwa mabilioni ya fedha na serikali baada ya kushinda katika Mahakama ya usuluhishi wa Biashara (ICC) na vurugu za kisiasa za Arusha, ni mambo yanayotarajiwa
kutinga katika kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC) inayotarajiwa kuketi leo.
Wachambuzi wa masuala ya siasa nchini waliozungumza na Majira jana juu ya kikao hicho ambacho ni moja ya vikao nyeti na vya ngazi ya juu katika uendeshaji na ufikiaji wa maamuzi ya chama hicho, wamesema kuwa ni vigumu kwa CC kutozungumzia sakata la Dowans ambalo kwa sasa ni moja ya mijadala iliyochukua nafasi kubwa katika duru za siasa nchini.
Ugumu huo, kwa mujibu wa wachambuzi hao, unatokana na ukweli kuwa sakata hilo mbali ya kuwa limevuta hisia za watu mbalimbali na kuibua mijadala mikali nchini, kila wananchi wa kada mbalimbali wakitoa maoni yao tofauti tofauti, limewagawanya baadhi ya viongozi waandamizi serikalini na ndani ya CCM yenyewe.
Pia mkutano huo umeitishwa muda mfupi tu baada ya kuibuka mgogoro wa umeya Arusha, ambapo CHADEMA walipinga uchaguzi ulioipa ushindi CCM, na kuamua kufanya maandamano ya amani yaliyozimwa kwa risasi na polisi hadi watu watatu wakauawa na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM, CC itakutana leo Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete katika kikao chake cha tatu tangu kufanyika uchaguzi mkuu mwaka jana, ambapo kinatarajiwa kuwa na ajenda tatu.
"Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, itakutana tarehe 20 Januari, 2011 mjini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete. Katika kikao hicho, Kamati Kuu pamoja na mambo mengine, itapokea na kujadili mambo yafuatayo;
"Hali ya kisiasa nchini, maandalizi ya sherehe za maadhimisho ya CCM kutimiza miaka 34 na matembezi ya mshikamano na kupokea taarifa ya mkutano wa makatibu wakuu wa vyama vya ukombozi kusini mwa Afrika uliofanyika mjini Luanda, nchini Angola kuanzia tarehe 7-10 Desemba, 2010, ambao Chama Cha Mapinduzi kiliwakilishwa," ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya CCM.
Kikao hicho kinafanyika siku chache baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri kilichokutana chini ya mwenyekiti wake, Rais Kikwete, ambacho taarifa zinasema suala la Dowans kulipwa mabilioni ya fedha, ni moja ya hoja zilizopata nafasi kubwa kujadiliwa barazani, ambapo kumekuwepo na mgawanyiko wa wazi na wa chini chini, kundi moja likipinga, lingine likiunga mkono serikali kutekeleza uamuzi wa ICC.
Suala jingine kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya siasa waliozungumza na Majira ni juu ya mjadala mwingine mkali wa katiba mpya, ambapo imeanza kudaiwa kuwa CCM kinaonekana kukosa mtu wa kuzungumzia mchango wa chama hicho, hata baada ya Rais Kikwete kuweka bayana kuwa haliepukiki.
Nadhani magazeti ndiyo yanayofanya kikao hiki cha wahuni kionekane ni kikao muhimu. AMA kwa hakika vikao vya CCM vimepoteza hadhi na hatuhitaji kujua kama vinafanyika. Tuvipuuze kwa kuwa ndio chimbuko la madudu yote hapa nchini, Kama unabisha sikia utabiri huu: wataamua kuhalalisha mauaji ya Arusha, hawazungumzia mauaji ya Mbarali kwa kuwa hakuna wa kumsingizia, watahalalisha malipo ya dowans, na watataka CCM isimamie mjadala wa Katiba badala ya wananchi, na suala la mgao wa Umeme, kupanda kwa bei ya gesi au nauli hawatahoji.
ReplyDeleteMtoa maoni hapo juu ,ingawa una uhuru wa kutoa maoni utakavyo lakini lazima uwe na adabu huwezi kuwaita viongozi wa nchi wahuni hiyo ni ishara ya kuwa wewe ndio muhuni, maana una fikra chofu na chafu,maana kioo cha mtu ni mtu tabia zako unaona kila mtu ni kama wewe acha hizo,uwe na adabu sio wewe unakaa kupanga fujo kila kukicha,na kupinga kila kitu akilini mwako kisa eti mpinzani!!Hawa ni viongozi wetu inabidi tuwape heshima yao,nina wasiwasi na malezi na uzawa wako
ReplyDeleteHivi wewe unayesma kikao cha halmashauri kuu ya ccm hakina umuhimu wa watu kupewa taarifa kweli una akili nzuri.umelazimishwa na nani usome? mimi nikiona habari za Mbowe,Slaa na Ndesamburo kwenye gazeti hata kama nilikuwa nataka kununua sinunui tena maana naona kama nimeshika mavi,lakini simzuii wala kumshawishi mtu mwingine asinunue. na suala la upandaji wa maisha haukwepeki kama mtakimbia mashamba kuja mjini kuuza shanga mkiwaacha mama zenu na dada zenu kuwa mapunda wa kuwalimia na baba zenu kuamkia kwenye vilabu vya pombe
ReplyDeletemtoaa maoniwa kwanza unatakiwa kutumia lugha ya uungwana kwani nia wengi wanaosoma maoni hayo viongozi wa kitaifa wamechaguliwa na wananchi unatakiwa kuwaheshimu unachotakiwa ni kukosoa kwa hoja huo ndio uungwana kwani ni viongozi wako tu hata kama wewe hutaki.
ReplyDeleteToeni maoni kulingana na habari inayozungumwa. Vinginevyo mnaonekana ni wehu kuzungumzia maoni ya mwenzio na hasa kwa kutumia lugha ndivyo sivyo.
ReplyDeleteMtoa maoni wa kwanza hakukosea..Ukweli ni kwamba viongozi wetu (hasa wa CCM) ni wahuni. Mhuni hamsikilizi mtu mwingine yeyote bali muhuni mwenzie, hata kama analoambiwa/analofanya ni kinyume na ubinadamu/sheria..
ReplyDeleteHivi unafikiri kama hiyo DOWANS ingekuwa ya Mbowe/Dr.Slaa/Lipumba/Mtikila si wangeshawekwa jela???
Kama kuna mtu anayeamini kwamba Mr.Prez/Waziri Mkuu/Makamba hawawajui DOWANS ni ya nani aseme..
Na kama wanajua na hawatuambii Watanzania tuliowachagua watufanyie kazi maana yake ni nini kama sio UHUNI???
Dowans wameishatajwa wenye kumiliki kilichobaki ni majungu ya ujinga,hoja yetu sisi kama kuna watanzania wenye hoja za msingi za kisheria za kulipa malipo hayo waende mahakamani kuzuia and nothing more,kwani leo tukisema Mbowe kamilikishwa jumba lile la NHC kinyemela utaamini? si mpaka ushahidi? pingeni hizo habari za wamiliki kwenye vyombo vya sheria sio majungu
ReplyDeleteSiku hizi kila kitu tu ni siasa! Tena siasa za chuki ya wazi wazi. Kwa mtindo huu tutafika kweli?!
ReplyDeleteHebu tubadilike Watanzania, tuanze kujenga hoja kisayansi, si tu kumchukia mtu! Mkumbuke watanzania wote ni sawa, tutafute hawa wanaotugawa kwa msingi ya mali, udini na ukabila tuwajuwe na tutafute njia za kuwakabili na kuwaadabisha kwa kutumia sheria zetu!
Carwin! (Liberal Democratic Person)
Wachangiaji namba mbili na tatu nahisi wamechangia wakiwa na ghadhabu, kila mwananchi ana uhuru wa kutoa maoni yake, sijaona kosa alilofanya mchangiaji wa kwanza katika kutumia neno "uhuni" - hebu tungejiuliza kwanza maana yake kabla hatujaamua kujikita kwenye kutumia maneno machafu kama yaliyotumiwa na mchangiaji namba mbili. Sisi sote ni watanzania na sote tunapaswa kuendelea upendo na mshikamno bila kujali jinsia, dini, itikadi wala makabila yetu. Uchaguzi wa maneno katika kutoa hoja uzingatiwe tafadhali...
ReplyDeleteTatizo la vikao vingi ni kwamba yale tunayoelezwa wananchi ni yale waliyopatana tu,yale yaliyoleta ushindani hayasemwi,demokrasia ya wengi wape inatoa nafasi kwa mafisadi wengi kuamua na tukadhani hayo ndiyo maamuzi ya chama.Ikumbukwe vikao vingi hualalisha maovu na kulazimisha wapinzani wa hoja zao kunyamazishwa kimya kwa kisingizio cha maamuzi ya wengi ndio ya kweli..lakini kuna siku tutafika,uongo ni mipango ya muda mfupi,ukweli hudumu milele.
ReplyDeleteAmaa kweli UKWELI UNAUMA hapa mtu anatoa maoni yake tayari watu wanaumia, bila shaka huu ndo ushamba wa wana sisiem. Wamepoteza dira kabisaaa!!!!
ReplyDeleteLaima waitwe wahuni kwani kauli zao matendo yao ni ya kuhuni suala la mtu kutoa maoni yake na wa wengine kupinga linatoka wapi wewe zungumzia mada ya gazetin sio mtoa maon mwenzako hao ni viongoz wa watu wachache sio wa wengi mtu anachaguliwa kwa kula milion tano out of million 19 na bado milion 5 kuna kura kachakachua nadhan CCM inatumia kodi ya wananchi kuwapa watu waende kuwasafisha magazetin baada ya mafisadi kununua baadhi ya magazeti kuwasafisha wameona watanzania wengi hawasomi magazeti yao kwa hiyo wanawatumia watu kuja kujisafisha humu kumbuka wanasoma magazet online na kutoa maon ni wasomi na waelewa wasiowaelewa hawana elimu ya kuja kutoa maoni yao humu ndani
ReplyDeleteMUNGU IBARIKI TANZANIA
elimu busara ustaarabu na hekima siolazima uende shule ni hulka ya mtu jama wabongo tuwe makini na vibaraka wanaotaka kutuharibia nchi yetu kuna mijitu baba msomali mama mtanzania unadhani mtuhuyo kale katabia kausomali kataisha?jihadharini sana na watu hawa la sivyo tutaishia pabaya nchi haitatawalika
ReplyDeleteTunakubaliana kutoa maoni ni Uhuru wa mtu lakini unapodai eti waliopiga kura ni Mill 5 ina maana unawaongoza haohao tu, wewe unaongozwa na nani? kama si fujo na ubishi? Unapodai vyombo vya habari vinanunuliwa kuwasafisha unataka tukubaliane na wewe?na hayo yenu yanayozua uongo kila kukicha ndio uandishi? Ni fujo maan leo Ikulu inaandaa Slaa akamatwe, mara JK awaziba midomo Sitta na Mwakyembe mara hili mara lile ni unafiki na nia ni kuongeza chuki baina ya watu na watu Vyombo vya habari ni silaha kubwa inayoweza kuleta machafuko na ikitumiwa vema ni silaha ya kuleta amani na masikilizano nia yenu nini na hizo chokochoko za uzushi kila kukicha, magazeti kama TZ Daima,Mwananchi,Mawanahalisi nk, uandishi wao ni staili ya kulipuwa hakuna siku wanaandika mema wao ni maovu tu
ReplyDeleteHasira na chuki zako ni za Mkizi ewe mtoa maoni wa kwanza.Hutaki kusikia vikao vya CCM kwa lipi?Kwa uongo na uzushi unaoandikwa na magazeti yenye njaa baada ya kuahidiwa kupatiwa "Sembe"?Ninakuonea huruma sababu huna ukaribu na hao waganga njaa.Masikini unaburuzwa,toa hoja siyo kujazibishwa na wajanja,tena mabepari wa bongo na waliokwisha inadi nchi kwa chama cha mabepari wa "Conservative" cha Uingereza kabla hawajatawala.Tz Daima au Mwanahalisi na hata Mwananchi mnaharibu bongo za watanzania kwa maslahi yenu binafsi?Hivi hili ndilo jukumu tulilolitegemea kwenu la kujenga fikra sahihi za watanzania?Hebu balace story zenu na ziwe za ukweli watanzania wafikiri kiusahihi.Ninyi mmeishachambua utajiri wa viongozi wa chadema kama mnavyowachambua wa CCM.Hivi hamjui kuwa tunafahamu wazalendo wakileta habari za usahihina zenye usawa kisiasa kwa wahariri wanazitupa katika shimo la taka?Lakini mlishasema wajinga ndio waliwao,ila mtalipa tu,haki ya watu haitapotea.Pata fahamu msomaji.
ReplyDelete