LONDON, Uingereza
MCHEZAJI nyota wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry anaiunga mkono timu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu wa England msimu huu.Mchezaji huyo mwenye historia ya kufunga magoli mengi katika klabu hiyo, amekana kuhusu
uwezekano wa kurejea tena kucheza kwa mkopoa
Emirates na amemtaka nahodha wa sasa wa timu hiyo, Cesc Fabregas kutofikiria kuhusu watu wanaomsema.
Henry alikuwa akizungumza kwenye chakula maalumu cha mchana kilichotayarishwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo, wakati wa kupatiwa tuzo ya mafanikio.
Arsenal kwa mara ya mwisho ilitwaa ubingwa katika msimu wa 2003/04.
"Ninafikiri wanaweza kufanya hivyo kutokana na soka wanayocheza," Henry alisema na kuongeza kuwa itakuwa ni kitu kizuri kwa klabu kutwaa ubingwa, hasa kwa ajili ya mashabiki.
Mchezaji huyo wa Ufaransa kwa sasa amekuwa akifanya mazoezi na Arsenal, lakini amekana taarifa za uwezekano wa kujiunga na timu hiyo kuichezea kwa mkopo akitokea timu yake ya sasa ya New York Red Bulls, inayoshiriki Ligi ya Major League Soccer ya Marekani.
Alisema alipokuwa Arsenal, alifurahia maisha na sasa yuko Marekani ambapo anafurahia.Kuhusu mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Arsenal na Barcelona, alisema itakuwa ngumu kwa kuwa timu zote zinacheza soka nzuri.
Alisema yeye ni shabiki wa Arsenal, lakini pia ana marafiki Barcelona ambayo ni timu aliyoichezea kabla ya kuhamia Marekani.
No comments:
Post a Comment