Na Mwandishi wa Polisi Zanzibar
JESHI la Polisi Zanzibar linawashikilia watu watatu wakiwemo wakazi wawili wa Dar es Salaam kwa tuhuma za kupatikana na dola bandia za Marekani 359,000 sawa na sh milioni 59.5 za Tanzania.Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, ACP Aziz Juma Mohammed, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Hassan Mpanda(40) na Elia Justin Silwimba (32) wote, wakazi wa Zakhem Mbagala, Dar es Salaam na Saidi Mpanda(28), mkazi wa Mwembenjugu mjini Unguja.
Alisema watuhumiwa hao wametiwa mbaroni kwenye eneo la Mwembenjugu na Makachero wa polisi wanaofuatilia nyendo za mtandao wa matapeli wanaoingiza fedha bandia visiwani humo kwa lengo la kuwatapeli wananchi wakiwemo
wafanyabiashara wakubwa.
Kamanda Aziz amesema kuwa kwa muda mrefu Makachero wa Polisi hapa nchini wamekuwa wakifuatilia kwa siri mtandao unaosambaza fedha bandia kwa baadhi ya wafanyabiasha na kwamba kukamatwa kwa watuhumiwa hao ni mwanzo mzuri wa kulibaini kundi hilo na kulisambaratisha.
Good work! Lakini mbona wameshindwa kuwatia mbaroni mafisadi waibao mabilioni ya fedha katika mabenki na mashirika ya umma?
ReplyDelete