Na Joseph Mwambije,Songea
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)kimefanya maandamano ya amani kushinikiza Mkuu wa Wilaya ya Songea, Bw. Thomas Sabaya ajiuzulu
kutokana na utaratibu mbaya wa ugawaji wa mbolea ya ruzuku na kusabababisha wananchi wa kata saba za wilaya hiyo kuikosa.
Maandamano hayo yalianza kwenye ofisi ya Chama hicho Wilaya ya Songea katika Kata ya Mfaranyaki na kuzunguka maeneo ya Mjini na kuishia kwenye uwanja wa Malori katika kata ya Majengo.
Katika maandamano hayo ambayo yalipambwa na polisi wengi vijana ambao walikuwa wakikimbia kimbia kuhakikisha hakuna vurugu, waandamanaji walitanguliwa na gari ambalo lilifungwa vipaza sauti vikitangaza kuwa Mkuu wa Wilaya anatakiwa ajiuzulu kwa ugawaji mbovu mbolea.
Matangazo hayo, yalisema vigogo waliokamatwa na vocha za mbolea za ruzuku wameonewa na kwamba mwenye makosa ni Bw. Sabaya.
Katika Uwanja wa Malori viongozi wa chama hicho walihutubia mkutano wa hadhara ambao ulihudhuliwa na umati mkubwa wa watu kutoka maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Songea.
Akihutubia kwenye mkutano huo Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mjini, Bw. Joseph Fuime alisema Mkuu huyo wa wilaya amefanya hujuma na kuzinyima mbolea kata saba, tano kati ya hizo zikiwa zinaongozwa na madiwani wa CHADEMA.
Bw. Fuime alisema hali inaonyesha kuwa Mkuu wa Wilaya ameshindwa kazi kwa kushindwa kusimamia mbolea ya ruzuku na anapaswa kujiuzulu.
Kwa upande wake mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA, Wakili Edson Mbogoro akizungumzia sakata la Dowans alisema Serikali inafanya mchezo na maisha ya Watanzania kwa kuwabebesha mizigo isiyo wahusu kwa kupandisha gharama za umeme kufidia ulipaji wa Dowans.
Alisema kuwa hali inaonesha kuwa CCM inafikia ukiongoni baada ya kutofautiana na vijana wao kuhusu kuilipa kampuni hiyo hewa ambayo ilirithi mkataba wa Richmond, na kwamba ndani ya Chama hicho kuna watu wenye uchungu kwa kuona Samuel Sita na Dkt. Harrison Mwakyembe wanaangamizwa.
Wakati huo huo, mwandishi Wetu Cresensia Kapinga, Songea anaripoti kuwa watu wanne wametiwa mbaroni na polosi mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa vocha 459 za ruzuku za pembejeo za kilimo zenye thamani ya sh. 21,114,000.
Waliokamatwa ni maofisa wawili waandamizi wa Idara ya Kilimo katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, mhasibu msaidizi pamoja na wakala mmoja wa pembejeo za kilimo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Bw. Michael Kamuhanda alisema kuwa watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi, wanadaiwa kuwa walishirikiana na mawakala hao kuiba vocha hizo.
Alieleza kuwa vocha zilizoibwa ni za mbolea ya kukuzia mahindi ambazo zilipaswa kusambazwa kwenye kata za halmashauri ya manispaa ya Songea lakini wakazi wengi wamezikosa, jambo ambalo lilisababisha kero kubwa kwa mkuu wa wilaya ya Songea, Bw. Thomas Ole Sabaya.
Alifafanua zaidi kuwa vocha hizo hapo awali ilidaiwa kuwa zimepelekwa vijijini ambako wakazi wa Manispaa ya Songea wanakolima, lakini baada ya kufuatilia kwa makini imebainika kuwa hazikuwafikia wakulima hao.
Bw. Kamuhanda alisema polisi inaendelea na uchunguzi wa kina katika maeneo mengine ya vijiji ambayo yanadaiwa kukumbwa na wizi huo.
Hongereni CADEMA
ReplyDeleteTutaendelea kupambana ili tupate viongozi ambao
KISIASA, KIUTAWALA, KIFIKRA na KI-UZALENDO ni watu safi kama Dr Wilbroad Slaa.
Tanzania hatutafuti kuongozwa na MALAIKA. Wala hatuangalii mtu ametoka dini ipi. Tunayemtaka ni mwanasiasa ambaye :-
1/ Anayo mapenzi ya kweli na nchi yake.
2/ Anayechukia rushwa, wizi, ufisani, nk.
3/ Na anajua nchi yetu inapaswa kuelekea wapi, kwa njia ipi na kwa manufaa ya Watanzania wote.
Je, huko CCM ni wangapi wenye sifa kama hizi
Watanzania wote wanajua kwamba Dr Slaa anazo sifa zote hizi.
Ninachomwomba Dr Slaa ni hiki: usikatishwe tamaa na watu wenye mawazo finyu na wasioitakia mema Tanzania. Wewe pamoja na chama chako, Tafathali endelezeni mapambano, tupo nyuma yenu kwa hali na mali !!!!
by
Abdalha Ali Juma.
Chadema sasa mmezidi, ni vile hamna kazi ya kufanya, kila kitu maandamano halafu mnasema mnataka kuongoza nhi. Mh yetu macho ila mnakoelekea siyo kuzuri
ReplyDeletesisi wanasongea tumesema maandamano ya Chadema ni kokosa kazi lakini wote tunajua Mbogoro ni kizazi cha uhaini nani asiyejua kaka yake Kapteni Ditrick Mbogoro na wenzake walitaka kumuua baba wataifa akiwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1983 leo Edsoni Mbogolo bila aibu anajifanya anauchungu na watu wa Songea wakati waototo wake wa kuzaa mwenyewe amewatelekeza huyo bwana ni mjinga sana anatamani kuona damu ina mwagika ya wanasongea tumeshituka.
ReplyDeleteChonde chonde Chadema tumieni akili jamani. Maandamano maandamano. Au mna ndoto kuwa yaliyotokea Tunisia yanaweza kutokea Tz? Hizo ni ndoto. Historia ya Tunisia na Tz ni tofauti. Tunisia ni nchi iliyokuwa ikiendeshwa kwa udikteta na wananchi wote walichoka. Sidhani kama viongozi wetu wametufikisha huko. Kumbukeni CCM ina wafuasi wengi ambao nao wakiamua kuingia mitaani sijui kama patakalika. Jamani CCM na Kikwete wanaungwa mkono na watanzania walio wengi. Kampeni zimeisha subirini 2015. Anzeni kazi ya kujenga chama chenu bado kichanga sana. Msiwe na ndoto eti mnaweza kupindua serikali kwa kutumia nguvu ya umma. Sehemu kubwa ya umma wa watanzania bado iko nyuma ya ccm. Mmejitahidi sana kupotosha umma kuhusu serikali, Kikwete sijui kama mnafanikiwa katika hilo. Kule Arusha bado mna kesi ya kujibu. Haiwezekani Slaa kuamuru watu kwenda kuvamia kituo cha polisi halafu aachiwe hivi hivi. Ingekuwa enzi ya Nyerere Slaa angeozea ndani. Bila aibu unamsikia Mbowe eti waliokufa walikuwa wanapigania kukomboa nchi. Maneno haya yanatia kinyaa kabisa. Chadema chagueni strategy nyingine la sivyo mkiendelea hivi hata maendeleo mliyoyapata katika uchaguzi uliopita yatapotea ikifika 2015.
ReplyDeleteNaona kuna vifisadi vimetumwa hapa kupigania yasiyo piganika. Mapambano na maandamano nchi nzima hadi kieleweke kitu. Bora kufa kwa kuipigania nchi yangu kuliko kufa kwa Ukimwi au kwa Ujambazi!
ReplyDeleteMoto uliowashwa na CHADEMA hautazimika kamwe. Viongozi wa vyama vingene someni alama za nyakati. Treni inaondoka hiyooooooooo ole wenu mkianchwa nyuma - utakuwa ndiyo kifo chenu kisiasa
May God Bless Tanzania !!!!
Juma