25 January 2011

Carrol kukaa nje kwa wiki mbili

LONDON, Uingereza

MSHAMBULIAJI Andy Carroll, atakuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili baada ya kuumia paja.Kutokana na kuwa nje katika kipindi hicho, mchezaji huyo atakosa
mechi saba za Ligi Kuu England, ambazo timu yake ya Newcastle itacheza na pia kukosa mechi tatu za England.

Habari hizo zimethibitishwa na timu ya madaktari ambao wameeleza kuwa amechanika nyama za kwenye paja, ambapo awali aliumia na kukosa mechi kwa wiki mbili.

Carroll, ambaye ameshafunga magoli 11 katika Ligi Kuu ya England msimu huu, sasa haionekani kama anaweza kurejea kucheza hadi Machi.

Baada ya kucheza ugenini dhidi ya Stoke Machi 19, Carrol anaweza asicheze tena hadi mechi ya nyumbani, dhidi ya Wolves Aprili 2 mwaka huu.

England ina mechi tatu kwa wakati huo ya kuwania kufuzu Euro 2012 dhidi ya Wales na za kirafiki dhidi ya Denmark na Ghana.

No comments:

Post a Comment