21 January 2011

Kili Music awards yazinduliwa

Na Elizabeth Mayemba

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro, juzi ilizindua rasmi Tuzo za Muziki za Kilimanjaro 'Kilimanjaro Music Awards' kwa mwaka
huu, ambapo kilele chake kitafanyika Machi 26, mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam juzi wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema kila mwaka wanaboresha tuzo hizo na mwaka huu yatakuwa na ubora zaidi.

"Kwa mwaka huu tumeboresha zaidi tuzo hizi na pia wasanii wa ndani tutawapa kipaumbele zaidi kwa lengo la kukuza vipaji vyao," alisema Kavishe.

Alisema watakuwa wakiboresha zaidi tuzo hizo kila mwaka, lengo ni kujenga vipaji vya wasanii wa hapa nchini na mwaka huu wamejaribu kuboresha maeneo yote muhimu.

Naye Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, George Minja alisema nia ya kamapuni yao ni kutaka kufanya kazi karibu zaidi na wasanii, ikiwa na kukuza vipaji vyao.

"Kampuni yetu ina nia nzuri kwa wasanii na ndiyo maana tumekuwa karibu nao kuhakikish  tunakuza vipaji vyao kupitia tuzo hizi na mwaka huu tumeboresha zaidi," alisema Minja.

Alisema mwaka huu, watakuwa wakifanya matamasha mbalimbali nje ya Dar es Salaam na pia wamewaomba wadau wa muziki watoe ushirikiano mkubwa, ili kufanikisha shughuli hiyo.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Gonje Materego alisema tuzo hizo zitaendelea kutolewa kwa utaratibu mzuri na mwaka huu watafanya mabadiliko makubwa mno.

No comments:

Post a Comment