13 December 2010

Zitto, Shibuda waundiwa kamati

Na Mwandishi Wetu

WAKATI Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikitarajiwa kutoa msimamo wa chama hicho juu ya masuala mbalimbali ikiwemo hali ya kisiasa nchini na ndani ya chama hicho, imeelezwa kuwa Mbunge wa
Kigoma Kaskazini Bw. Zitto Kabwe ametakiwa kujipima mwenyewe kisha ajiuzulu, baada ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani na wabunge wa chama hicho.

Imeelezwa kuwa kura za kutokuwa na imani naye, zilizopigwa wiki iliyopita na wabunge wa CHADEMA katika kikao cha kamati yao, kilichofanyika Mjini Bagamoyo, hakizumwondoa moja kwa moja katika cheo chake cha naibu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, bali ilikuwa ni ishara ya kuwa watu anaowaongoza bungeni hawana imani naye tena hivyo kumtaka afikirie mwenyewe kisha achukue uamuzi wa kujiuzulu kabla wabunge hao hawajachukua hatua za kinidhamu juu yake.

Habari kutoka ndani ya chama hicho zimebainisha pia kuwa Kamati Kuu iliyoketi mwisho wa juma katika kikao maalumu, imeunda kamati kwa ajili ya kumshauri Bw. Zitto, baada ya wajumbe kuona kuwa kuna umuhimu wa kumsaidia ushauri nasaha kutokana na mwenendo wake ndani ya chama hicho.Vyanzo mbalimbali vimesema kamati hiyo inajumuisha Profesa Mwesiga Baregu, Dkt. Mkumbo Kitila, Shida Salum na mwanachama mwingine wa chama hicho.

Mbali ya kubainika kwa suala hilo, pia habari kutoka vyanzo mbalimbali vya kuaminika zimeeleza kuwa Kamati Kuu ya CHADEMA, imeunda kamati nyingine kumchunguza Mbunge wa Maswa Magharibi, Bw. John Shibuda, kutokana na tuhuma zilizowasilishwa na kamati ya wabunge, iliyokutana wiki
iliyopita Mjini Bagamoyo.

"Nafikiri hilo la Zitto waandishi wamwelipotosha kwa kiasi kikubwa, mimi ninavyojua walichofanya wabunge wale ni kupiga kura ya kutokuwa na imani naye (Zitto), kisha mwenyewe apime uzito wa uamuzi huo kuwa watu anaowaongoza hawana imani naye, kisha mwenyewe ajiuzulu, kabla wabunge wenyewe hawajachukua hatua za kinidhamu juu yake.

"Hata hivyo uamuzi huo wa kuchukua hatua za kinidhamu ikiwemo hata kumwondoa katika cheo hicho, imo katika mamlaka ya Kamati ya Wabunge wa CHADEMA, yaani Party Caucus, wanayo mamlaka hayo kabisa wakiona kuna haja ya kufanya hivyo, baada ya yeye kushindwa kuchukua hatua yoyote hasa kujiuzulu maana ni kiongozi wao wenyewe, hivyo haihusiani na chombo kingine ndani ya chama."Kumbuka pia kuwa naye ataitwa kama alivyoitwa wengine kuhojiwa juu ya kutotekeleza maamuzi halali ya kikao ya kuingia ukumbini siku ya ufunguzi wa bunge kama
ilivyokuwa imeamuriwa...lakini cheo hajavuliwa, mwenyewe apime kisha ajiuzulu," kilisema moja ya chanzo chetu cha habari.

Chanzo chetu kikiwa na tahadhari ya kutotaka kufafanua masuala mengi, pia kilisema kuwa Kamati Kuu ya CHADEMA imeona kuna umuhimu kukaa na Bw. Zitto kisha apatiwe ushauri juu ya mwenendo wake wa kisiasa akiwa kama mmoja wa viongozi waandamizi wa chama hicho, ambapo mbali ya kuwa ni naibu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni pia ni naibu katibu mkuu wa chama hicho kwa upande wa Tanzania Bara.

Nafasi hiyo ya naibu katibu mkuu bara, inamfanya kuwa mmoja wa watu wawili wanaomsaidia Katibu Mkuu Dkt. Willibrod Slaa, mwingine akiwa ni Hamad Mussa Yusuf, kwa Zanzibar, lakini nafasi ya naibu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, inamfanya kuwa msaidizi wa Mkuu wa Kambi, Bw. Freeman Mbowe.

Kwa upande wa suala la Bw. Shibuda, vyanzo vyetu vilieleza kuwa mbunge huyo ambaye alihamia CHADEMA kutoka Chama Cha Mapinduzi, siku chache kabla ya kampeni za uchaguzi kuanza, baada ya kubwagwa katika kura za maoni, atachunguzwa kwa tuhuma kadhaa, ikiwa ni pamoja na kutotii maagizo na maamuzi kikao halali cha chama, kulaumu na kulalamikia nje ya chama maagizo na maamuzi hayo, kujaribu au kutaka kuleta mgawanyiko ndani ya chama.

"Bw. Shibuda alisema hana kosa wala hana haja ya kuomba msamaha, chanzo hicho kilisema wabunge walikuwa wazi kabisa kwake, wakimwambia asifikiri wanamwogopa, asifikiri kuwa wao hawakushinda uchaguzi...maana amekuwa akijigamba kuwa yeye ametumwa na watu wa Maswa.Juhudi za gazeti hili kuwapata viongozi wa chama hicho kuzungumzia taarifa hizo hazikuzaa matunda jana.

37 comments:

  1. KAMA CCM HAWANA JIPYA HAO

    ReplyDelete
  2. BRAVO CHADEMA! MTU AKIKOSEA AADABISHWE KULINGANA NA TARATIBU ZA CHAMA!MSIANGALIA NJE AU KWENYE VYOMBO VYA HABARI! MNAJENGA TAASISI YA KUELEWEKA SI YA UBABAISHAJI!

    ReplyDelete
  3. Hao ndio mamluki wa CCM, wachunguzwe kwa karibu sana

    ReplyDelete
  4. MFUKUZENI ZITTO HAMNA HAJA YA KUCHUNGUZA AU KUNDA KAMATI MAAN MAKOSA YAKE YKO WAZI WAZI

    ReplyDelete
  5. Nice,Tabora
    Zitto kuwa mkweli ,hapo ulipofika ni chademe wamekufukisha hapo,weka maslahi ya chama mbeli kwanza ,umaarufu sio hoja,hoja ni maslahi ya Taifa.
    Bw.Shibuda,wewe ni mamluki na kibaraka wa CCM,fikria ulikotoka,kama sio chadema kukushika mkono leo ungekuwa wapi?hebu jali maslahi ya chama kwanza.

    ReplyDelete
  6. Zitto hata sisi vijana wenzako tuliofikiri labda ulikuwa na nia ya kweli ya kuleta mabadiliko,lakini kumbe ni mtu wa kutapatapa kwani tangu uwepo kwenye kamati ya madini ndiyo ulipojimaliza mwenyewe.
    Kwa taarifa ndugu yangu zitto nafikiri kama unadhani bado unaungwa mkono na kundi kubwa jaribu kuhama chama ndiyo utagundua kama utaona mtu anakufata.
    labda niwakumbushe kidogo huyu jamaa(zitto) wakati fulani pale udsm aliwahi kuandika barua za vitisho kwa uongozi chuo sasa naanza kupata picha ya kuwa jeuri alikuwa anaipata kwa mgongo wa ridhiuan wakati wote.pia tunakuhifadhi lakini faili lako lipo...
    Labda niwakumbushe

    ReplyDelete
  7. kwa mtindo huu, ccm itatawala miaka yote kama mtu hana nidhamu kwa maana ya kutoheshimu maamuzi ya chama apewe adhabu sio kila siku kujadili mambo ya mtu mmoja kwenye vyombo vya habari, watanzania tuna mambo mengi sana ya kujadili kuhusu kujikwamua na umasikini, mimi nilifikiri huu ndio wakati wa vyombo vya habari pamoja na wananchi na vyama vya siasa kujadili vipaumbele alivotoa Mh. Raisi wakati akifungua bunge, badala yake tunatumia muda mwingi kumjadili mtu mmoja ambae hawezi kusaidia lolote katika swala zima la kujikomoa kiuchumu, kila siku zito, zito, zito, ni mambo mangapi yanayotokea ambayo watanzania tungepaswa kuyajua
    Jamani watanzania ifike mahali tujadili mambo ya msingi sio kujadili mtu ambae hawezi kuleta mabadiliko yeyote ya kiuchumi.
    Sasa ivi kuna tatizo kubwa la mgao wa umeme, pengine tungetumia fursa hizi kujadili athari za kutokuwepo umeme katika uchumi wa mtu wa kawaida, sio habari za mtu mmoja kila siku.
    Watanzia tuamkeni jamani

    ReplyDelete
  8. udini tu unawasumbua, ww zito kwa vile muislamu hapo hutokaa kila siku watakuzulia tu kila aina ya balaa, tafuta chama mapema ujiunge...

    ReplyDelete
  9. Kwa kweli Chama cha CHADEMA ninawapongeza mkiendelea hivi tutapata faraja na matumaini ya kuwa tunaweza kupata chama chenye upinzani bila kuyumba mara hiki mara kile. Tunawaombea mungu kwa hilo.

    Tunawaomba wanachadema jicho liwe macho saa zote kupambana na ambao hawaitakii mema chama hiki. Viongozi mnajuao mkishaanza kupigana huko juu huku chini hawakawii kukasirika. kwa hiyo mshikamane, mheshimiane kama familia.

    Kuhusu MH ZITTO, mmefanya vizuri kukanusha nakumpa uhuru zaidi wa kujieleza. Itakuwa ni uwanja mzuri wa kutoa hilo dukuduku lake rohoni ili chama kiendelee kufanya shughuli zake.

    ReplyDelete
  10. wanaoingiza udini kwenye mijadala ni masikini wa fikira. hatudanganyiki

    ReplyDelete
  11. Sidhani kumfukuza Zitto ndio suluhisho la mgogoro wa Chadema. Lakini zaidi wana Chadema wenye ndio wenye kauli ya mwisho na ni wao wenye kujuwa umuhimu wake ndani ya chama. Sisi wengine ni wachupiaji gari tu.

    Kuna mifano mingi ya watu walio hama kutoka CCM nakwenda upizani na wengine kutoka upizani na kurudi CCM tena. Wapo waliobahatika kupata kuungwa mkono kama huyo Shibuda na kuwa Mbunge kupitia Chadema.

    Kwa mtazamo wangu Zitto bado ni kijana, msomi na tayari ameshapata uzoefu wa kisiasa kwenye majukwaa na Bunge. Kama kuna kijana maarufu kwa Tanzania basi Zitto ndio wa mwanzo. Zitto ni mtu mwenye kuona mbali na ni mtu mwenye kupena kujifunza na ni mtu mwene kujiamini kwa maamuzi yake. Kama tungekuwa kule Zanzibar, bas huyu ni kama Ismail Jussa.

    Kama tulivyosoma magazetini kuwa yeye hajaomba hicho kinachopiganiwa kelele cha unaibu uongozi wa Bunge kwa kupia upizani. Na yupo tayari kuachana nacho ikiwa hawamtaki, leo hii ndi tunaona chama cha chadema kinakuja na kauli kama hiyo ya kumtaka ajiuzulu mwenyewe, wakati ni wao walio towa kauli za kusema amepoteza nafasi hiyo. wametanabahi kuwa kumfukuza tu, kumjengea umaarufu zaidi.

    Nakumbuka zitto alitaka kujitowa kwenye uchaguz uliopita kwa kujiendeleza na masomo kwanza, chama cha chadea ndio walio muomba agombaniye.

    Wakati ndio utakao tupa ukweli, hapa ni hamasa tu. Kwenye CUF anatufaa huyu kijana ha ha ha! Na sio CUF tu, leo akiingia NCCR mageuzi, bazi watampokea na ataweza kukipa hadhi chama hicho na chochote kile cha Tanzania

    ReplyDelete
  12. Udini udini na ukatoliki ndio unaouisumbua chadema. Lakini ukweli ni kuwa hawawezi kabisa kumfukuza Zitto,ni kujichimbia kaburi

    Bundi mbaya ananyemelea Chadema. Acheni udini na mtafanikiwa

    ReplyDelete
  13. mgondo wa mawazo, issue sio dini hapa,nyie mnao changia habari za dini mnalitia mchanga jamvi...nina wasiwasi na hoja yenu au mmetumwa na dr.wenu kikwete?au na nyie hamna uelewa wa udini kama kikwete?

    ReplyDelete
  14. Ni bahati mbaya wanasiasa wababaishaji wa CCM wameanzisha matumizi ya silaha ya udini na sasa kila mtu ambaye ni mwisilamu hata akifanya kosa aogopwe kusemwa eti wasije wakasema udini!!! Zitto, tena kama kiongozi, ameamua kutofautiana na viongozi wenzake na hakuficha hisia na msimamo wake - sasa hapo napo katumwa na wakristo au wapagani kuwa mpinzani dhidi ya viongozi wenzake? Na katika chama cho chote cha siasa duniani kote kiongozi akitofautiana na wenzake ama hulazimika kujiuzulu au hutakiwa kujiuzulu. Mimi binafsi ninaheshimu uhuru wake wa kutofautina na wenzake, lakini kama angekuwa ni mkomavu wa kisiasa (inaeleweka bado ni kijana) angefanya hivyo huku akijiandaa kujiuzulu badala ya kutaka umma uone kuwa anaonewa (kwa kutetea CCM na viongozi wake). Hapa hakuna udini wala ni nini, hizo ni propoganda za CCM.
    Ni sawa CHADEMA kucheza na diplomasia (na hapo hawana jinsi) lakini ninataka kuwahakikishia kuwa Zitto ni KIRUSI ambacho hatimaye kitawatokea puani.

    ReplyDelete
  15. Wanaoleta mawazo ya udini ni mfilisi wa fikra ambao siku zote wanapenda kutazama kila jambo kwa fikra za udini. Hawa ndiyo hata likapita gari likamrushia maji, anachoanza kufikiria ni kuwa labda hilo gari anayeendesha ni mkristo na amenirushia maji kwa vile mimi ni muislam. Rubbish ninyi wote wenye fikra za udini!! Watanzania wote wenye akili timamu, wakristo kwa waislam, wahindu kwa wapagani, n.k. n.k. tutaendelea kujadili kwa kuzingatia hoja siyo udini. Na ninyi ambao kila leo mawazo yenu yamekaa kwenye udini, endeleeni hivyo hivyo, wakati wenzenu wanatafuta maendeleo ninyi mnataka hata kivuli cha mkristo kikikupitia mwanze mjadala wa kwa nini kimekupitia, labda kimekwishachukua kitu fulani toka kwangu. Hawa ndiyo wanaofikiria kuwa kwa kila shida wanayopata imesababishwa na mtu anayeishi vizuri. Poleni sana maana umaskini wa mawazo ni laana zaidi ya laana zote.

    ReplyDelete
  16. Ohoo tayari mambo ya udini,hapo hakuna udini ni sauti ya wenye chama itukuzwe,msimuingize JK kwenye mambo yenu,mbona kila chama kina mgogoro wake lakini hawasemi wenye mawazo tofauti wametumwa na Chadema? na wewe Shibuda funga mdomo wako, huko si CCM na usilogwe siku moja ukasema unataka kugombea Urais kwa tiketi ya Chadema watakuu....... hao. Hao ni nyamaume,tunawajua vizuri

    ReplyDelete
  17. Sijui tutiteje sisa za Tanzania, sijui ni "BIASHARA KATIKA SIASA" au " SIASA KATIKA BIASHARA" ole wenu nyie wenye vidomodomo kwenye vyama vya watu,Watanzania tuko katika mfumo hatari sana wa siasa kwa asali tunayopakwa kwenye siasa tunadanganyika na asali feki tunayolmbishwa kwenye siasa na sisi tunailamba. NAWASIHI WATANZANIA WENZANGU TUNAPOCHAGUA CHAMA TUANGALIE MFUMO WA MAISHA WANAYOISHI VIONGOZI WALIOANZISHA HIVYI VYAMA KAMA NI WAFANYABIASHARA HAWATUFAI KATIKA NCHI YETU,TUACHE KUANGALIA UDINI TUMUANGALIE MTU NA VIONGOZI WENZAKE WANAISHI VIPI,TUTAIMALIZA NCHI YETU,YALIBORONGWA NA CCM NI MAKUBWA SANA LAKINI TUSIPOANGALIA YATAFANYWA MAKUBWA ZAIDI YA HAYO NA KWA UKWELI KABISA NAWAAMBIE SI CHADEMA WALA CCM NDIE MKOMBOZI WA WANYONGE KATIKA NCHI YETU,HAWA WAWILI NI NYOKA WA VICHWA VIWILI.

    ReplyDelete
  18. Zitto amekuwa maarufu sababu ya chadema na msimamo wake,lakini kujiamini kuvuka mpaka ni makosa. Ukihama hutakuwa maarufu zaidi utashuka yuko wapi Mrema?

    Shibuda awe muungwana! mwenye akili anajua maana yangu kama Shibuda hataelewa msaidieni. Kuwa muungwana tu inatosha kwa shibuda

    ReplyDelete
  19. kwa nini zitto tu na shibuda kina ndesa vipi?

    ReplyDelete
  20. Shibuda kweli funga domo lako huko maana huko si ccm ulipokuwa unaropoka unavyotaka,unaambiwa uwe mstaarabu kwa maana uwe mtumwa wa fikra za wenye chama,hayo yanayofanyika Chadema ingekuwa CCM ungeona,gazeti la Mawananchi lingelivalia njuga kulaumu viongozi kwa kuwachukulia hatua wenye mawazo tofauti na viongozi,kamwe kwa sasa watu hawafungiki midomo,hivyo vinyangarika vinavyolipa fadhila ya kuteuliwa bado hawana ujasiri lakini itafika wakati nao watakataa

    ReplyDelete
  21. Hakuna ishu yoyote ya udini na kama ni kweli nyie mlioshupalia udini mna uhakika na mnalolisema basi JK asingeshinda uraisi kwakuwa naamini na ndio ukweli kuwa wakristo ni wengi nchi hii kuliko waislamu mpende msipende hivyo kama mmeishiwa sera kaeni kimya na sio kusema mambo ambayo hayako tukileta udini wakristo ndio watatawala nchi hii alieanzisha ishu ya udini na aseme kwa mifano hai na sio kuongea tu pasipo mifano wakati mwenyewe kachaguliwa na hao wakristo na wakatoliki mnaowasema kutwa wako CHADEMA.

    ReplyDelete
  22. Watu wenye fitina na chadema wanataka ife na haitokufa kaeni chini zungumzeni wenyewe kwenye chama kama kuna tofauti mzimalize wenyewe huko kwenye vikao muwaache solemba wote wanaoinenea mabaya CHADEMA na kusema kuwa ni chama cha wachagga kama vile wote waliomo ni wachaga au wafuasi wa dhehebu moja la dini ya kikriso wala wengine waseme maruhani wao ndio wabaguzi na wadini kwakuwa wameinyooshea chadema kidole kimoja vingine vinne vimebaki kwao.

    ReplyDelete
  23. Kwa kweli tumechoka kuwaelimisha hawa ndugu zetu na sijui huko shuleni kulikuwaje kwa sababu hawabadiliki kila saa udini. Huu ugonjwa upo Zanzibar. Leo nimeingia ktk gazeti la mzalendo kwa kweli sikuamini, yaani hawa wajamaa wanaakili za kitoto za hovyo, yaani maoni yaliyopo ni kafiri aondolewe Zanzibar, nani kawauzia ardhi, makafiri wametoka wapi wengi hivi nk. Kisa ni kupatikana kwa ASKOFU wa kanisa huko Zanzibar. Samahanini ndugu watoa maoni kwa huu usumbufu, sikuvumilia.

    ReplyDelete
  24. mnamuonea zito,katika miaka mitano iliyopita Zito na Dkt Slaa walishirikiana na watanzania wakaiamini Chadema hivyo umaarufu wa Chadema ni wa Zito na Slaa ndio maana akina Tundu lisu na wenzake wakachaguliwa na wananchi kwa imani watashirikiana na akina zito na wenzao sasa nyie kuingia mnaingia na migogoro na sasa mnamsingizia Zito jamani kweli mkataa pema pabaya panamuita.

    ZITO NASEMA HIVI TULIA WATUMIKIE WANANCHI WAKO WALIOKUPA DHAMANA YA KUWAWAKILISHA BUNGENI VYEO VYAO VYOTE WAVULIE TUNAJUA WANAKUNYANYASA KWA VILE WEWE SIYO MCHAGA NA SIYO MKATOLIKI,WATANZANIA TUPO NYUMA YAKO.ENDEPO WATAKUFUKUZA WEWE WASHAWISHI WENZAKO 16 WANAOKUUNGA MKONO MUONDOKE NAO MKAJIUNGE NA CHAMA CHOCHOTE UKIFANYIKA UCHAGUZI MDOGO MTASHINDA MKIRUDI MTAUNDA KAMBI YENYE NGUVU YA UPINZANI BUNGENI,WEWE NI KAMANDA USIOGOPE KUPIGANA SONGA MBELE

    ReplyDelete
  25. WEWE MBAYU MBAYU UMETOKA WAPI? WEWE NDIO MNAOJIITA WAZANZIBARI AU.

    ReplyDelete
  26. Hata mkibisha ni udini tu ndio unaowasumbua tena udini wenyewe kama ule wa Tea Party ya Sarah Palin Marekani, habari ndio hiyo mkitema mkimeza shauri yenu. Maana kama kukaidi kutoka si Zitto peke yake ni mpaka mtoto wa Ndesamburo pia alikaidi na wengineo hao kina Shibuda, lakini wote hawakumuona wamemuona Zitto tu.

    Ila kikubwa ni kuwa Mbowe ANAMUOGOPA SANA na kumhara Zitto hilo halina ubishi, hata mkipinga hapa nyie vichamcho wake bali haisaidii. Na ushahidi ni pale alipokataa kugombea naye nafasi ya Uenyekiti, kwa hiyo hapo anataka mtu mwingine ambaye anaweza kumburuza kuwa naibu wake, anamjua Zitto ni ngoma nzito hawezi kumburuza.

    Na wewe Zitto unataka uambiwe vipi kuwa Chadema hawakufai, kwani ni kabila hiyo kusema huwezi kubadili, maana ni kabila peke yake ndio haibadiliki hata dini watu hubadili sasa hiyo Chadema ni kabila lako? Lakini ukitaka kuwakomesha hao waonyeshe ubishi wako wa kibangu bangu na kiha, hawajui kuwa sie waha wabishi kishenzi kula nao sahani moja mpaka kieleweke tujue kama hiki ni chama cha watanzania wote au cha kikundi kidogo cha wafanyabiashara kama ilivyoandikwa na gazeti la economist.

    Mwisho nyie mnaobisha kuwa si chama cha Waraka wa Kanisa Katoliki kwanini basi waumini wanafukuzwa huko makanisani kwa kushabikia wabunge wa vyama vyao vya siasa wasio wakatoliki? Kama huyo Mgombea alisema maneno hayo ya kukufuru, je hao wanachama waliyarudia hayo maneno? Au wanakuwa guilty by association? Chadema ni chama cha udini sana maana hata wakati wa uchaguzi kila siku walikuwa wanasema mgombea wao ni chaguo la Mungu! Sasa kama mambo ya Mungu sio ya dini ni nini au mlikuwa mnatania?

    Zitto wewe kaa pembeni halafu Tundu Lissu ndiye achukue nafasi yako nakwambia huyo Mbowe atakiona cha moto maana Tundu naye anajua mwenyewe mambo yake kwanza anavyopenda kuongea na kujiweka kimbelembele sasa hivi atampiku Mwenyekiti naye atamfanyia mizengwe na vibweka kama Zitto maana huwa hataki apitwe na mtu kwenye umaarufu.

    Mwisho mliingiza wenyewe kirusi cha Marando kwenye chama kisha mnalia na CCM? Waulizeni wenzenu kina NCCR na kina Mrema watawaambia, kwanza mbona ni yeye ndiye anayetetea baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi mahakamani!

    Lol! Waache nikanunue kokakola yangu baridi na popcorn nikae niangalie Movie la Chadema linavyoendelea!

    ReplyDelete
  27. Haya mawazo yako haya msumbui mtu kalale.

    ReplyDelete
  28. Komeni na Zanzibar. Hofu yenu kubwa ipo huko kutokana na waumini wa dini ya Kiislamu kuwa wengi,wala hamna kauli za kafiri kupewa ardhi Zanzibar ila ni USHE... wenu ndio mnapakaza hivyo. TUNAWAAMBIA WAKATI WA KUWAKANDAMIZA WAISLAMU UMEKWISHA MTAZAMENI BABA YENU MMAREKANI NA WENZAKE WANAVYOTAFUTA SULUHU, TUNAWATAKA MSIHARIBU NCHI. BIASHARA YENU YA SIASA MSIIHUSISHE NA UISLAMU,SISI AMRI ZETU HAZIENDANI NA UCHAGUZI WALA MATUKIO.ZIPO NA HAZIBADILIKIBADILKI,SHERIA YA DINI YETU HAINA PAHALA PA KUCHAGUA SLAA WALA KIKWETE. INAWATAKA KUMTII ALLAH (MUNGU)NA KUFUATA AMRI ZAKE AMBAZO HAZIHUSIANI NA SIASA.IKOMENI ZANZIBAR KABISA

    ReplyDelete
  29. Haya maoni kayatoa nani.

    Tangu Askofu Mkuu Toto alipofariki shughuli za kanisa hilo zilikuwa zikiongozwa na Askofu Mkuu mstaafu wa Anglikana Tanzania, Askofu Mtetemela na baada ya kustaafu hivi sasa kanisa hilo linaendesha shughuli za kiroho chini ya usimamizi wa Askofu Mkuu wa Tanzania, Valentine Mokiwa.

    Sambaza chapisho hili!
    Ingizo hili limetumwa na makame silima tarehe 12/12/2010 nyakati za 9:24 mu, na limehifadhiwa katikaHabari. Fuatilia majibu yoyote katika chapisho hili kwa RSS 2.0. Unaweza kuruka hadi mwisho na kutoa majibu.Pingi hairuhusiwi kwa sasa.

    MAONI (27)
    • #1 andikwa na Hassan10
    takriban siku 1 iliopita
    Jee wz’bar mupoooo? huyu Agustino Ramadhani jaji mkuu wa Tanganyika juzi aliulizwa kuhusu katiba ya Zanzibar kuandikwa upya alisema haijuwi maana hajapelekewa akaisoma?. lakini ya Tanzania anaijuwa maana kaisoma? na mimi nilikuwa sijuwi kuwa Popo wa Z’bar kumbe na yeye huchaguliwa Dodoma tena wa mara hii asitoke zanzibar atoke vatican Rome Itali?

    #2 andikwa na sale
    takriban siku 1 iliopita
    Jamani hizi sura za kikafiri zipo Zanzibar ama hii picha imechukuliwa toka Tanganyika? na kama zanzibar basi kumbe kuna makafiri wengi,,,
    Msalieni mtume janiiiiiiiiiiii,,,,,
    Hongera Komando Salmin Amour na Bilali matunda yenu tumeyaona,,,,,,,,,,,,

    #3 andikwa na Mrfroasty (Ufundi)
    takriban siku 1 iliopita
    Hadi viongozi wa dini pia wanachaguliwa Dodoma, nilidhani ni viongozi wa kisiasa pekee!

    #4 andikwa na salix2020
    takriban masaa 23 yaliopita
    ah hawa wengine kujipachika majina ya kiisilamu na wakati ni makafiri sijui wanahisi wanamzuga nani kwa sababu nakumbuka miaka ya iliyopita wakati wa utawala wa mkapa aliwahi kupelekewa barua kutoka jumuia moja ya kiislamu tanzania ya kutaka usawa katika nyanja mbali mbali ndani ya serikali ya tanganyika baina ya waislamu na wengineoe kutokana na kuonekana serikali ya tanganyika kulibeba kanisa na waumini wake na kuwabana waislamu wasipate haki zao inavyostahiki basi miongoni mwa majibu yake alisema hamuoni katika serikali kuna viongozi kibao wana majina ya kiislamu mimi nilidhani atasema huoni kuwa kuna viongozi kibao wakiislamu wamo katika serikali yake lakini akasema viongozi wenye majina ya kiislamu sasa ninachokusudia hapa inaonekana hawa makafiri wa tanganyika kujipachika majina ya kiislamu ndio kujipatia kibali cha kuaminiwa na waislamu ama nini? au wenzangu mna maoni gani?

    #5 andikwa na salix2020
    takriban masaa 22 yaliopita
    na jengine ndugu zangu wazanzibari nawausia jamani hata kama kwetu kuna dhiki vipi basi kama una viwanja basi ni bora kumuuzia ndugu yako yoyote wa kizanzibari na sio kafiri yoyote wakitanganyika hata akikwambia anataka kufanya jambo gani basi ni kheri usiuze kwa sababu miongoni mwa ajenda kuu za ukoloni wa kitanganyika kwa zanzibar ni kuifanya zanzibar kuwa haina tofauti na dar-es-salaam kwa makanisa kwa hiyo jamani mujue ukimuuzia mgeni yoyote kiwanja na ikathibiti kuwa simuislamu hasara yake ni kwa kizazi kijacho kama tuna uchungu na uzalendo na nchi yetu basi suala hili ni la kulizingatia ahsanteni

    #6 andikwa na Manyamba
    takriban masaa 21 yaliopita
    acheni chuki za kidini, nyinyi wenyewe mmejazana ktk nchi za watu huko ulaya mbona hamjafukuzwa? wakristo wana haki km walivyo waislam zanzibar, hata Mtume SAW aliishi na wakristo kwa wema tu ktk kipind chake, hakuwatukana wala kuwanyanyasa, someni dini vizuri msijitie waislam kumbe hamna lolote mnalolijua, kwanza Zanzibar sio nchi ya kiislam bali ni nchi ya waislam, tena nn kupiga kelele zilokuwa hazina maana? hata km ingekuwa ya kiislam basi bado wakristo wana haki ya kuishi zanzibar, hakuna baya lolote kuchagua viongozi wao, na nyinyi chaguen wenu msiwatukane wakristo bureeee…

    ReplyDelete
  30. Wakatoliki mmeyataka,msiwachokoze Waislam,siasa haina dini katika nchi yetu. Wanasiasa wa Kiafrika ni wezi,ugomvi wote huo ni maslahi ya kuuziana tenda za miradi,kumiliki hazina ya nchi na kutanua na familia zao. Cha kwanza Watanzania cha kufanya katika katiba mpya ni kuondoa ruzuku katika vyama,huu ni ufisadi wa hali ya juu,kuondoa marupurupu ya wabunge,mishahara isipindukie kisha mtaona kama hao jamaa wauaji na wahujumu wa nchi yetu kutoka mkoa wa Kili... kama watajikita kwenye siasa kwa nguvu za hali yajuu kama ilivyo sasa,hawa jamaa hata huko makanisani huwa hawakubali jamii nyingine idhibiti madaraka,fanyeni nyie wenye dini hiyo sensa muone,hata ugomvi wa dayosisi ya Pare na Arusha ilikuwa ni hivyo. Sasa Watz wenzangu tupiganie kwenye katiba mpya maslahi ya kupindukia ya vyama na wabunge ziondolewe hamtakaa kuona vurugu hizi. Hapa issue ilikuwa ni zitto na shibuda kusakamwa kupingana na maamuzi ya chama chao, lakini ghafla mamluki wa pande zote mbili za dini zimejipenyeza. Kujua kutumia internet hakuwafanyi kuwa na uwezo wa kujenga hoja na kuandika,kama issue haikuwa ya dini,basi tujadili uhuru wa mawazo ya mtu against fikra za mwenyekiti kuwa ndio mwisho.

    ReplyDelete
  31. Zito umarufu huo ni wakwako na kuwadhihirishia hilo waachie chama chao hao wachagga nawewe hamia chama chochote cha watanzania uone kama watashinda kwenye jimbo lako

    Hamiss Songea

    ReplyDelete
  32. Zitto wewe ni kamanda unatisha Mbowe na wenzake wanakuhara,akina tundu lisu ni wapambe tu wanazani watakuweza watanzania wapo nawewe pambana kamanda.

    Pitter Challe Njombe

    ReplyDelete
  33. Majira ahsante sana kwa kutochakachua maoni hapa tunatoa kweli yaliyo moyoni,magazeti mengine yanamilikiwa na jamii hii mbovu ambao kila kitu dunia hii wanataka wao. SASA NAPASUA JIPU:- NYIE MNAOMILIKI HICHO CHAMA CHA CHADEMA MNAOTOKA MKOA WA KILIMANJARO HATUWAAMINI KUSHIKA MADARAKA YA JUU KATIKA NCHI YETU KWANI HISTORIA YENU NI CHAFU KATIKA JAMII NI MAKATILI,WAUWAJI,WEZI,MAJAMBAZI,WAHUJUMU UCHUMI WA NCHI YETU NA KILA KIBAYA MNACHO NYIE ACHILIA MBALI UKABILA. SEHEMU KUBWA YA UTAJIRI WENU MNAOMILIKI UMETOKANA NA VITENDO VIOVU, HAMNA ASIYELIJUA HILO,HAYO MAKABILA MENGINE YALIYOJIPACHIKA HUMO KIPINDI HIKI AMBACHO CCM IMEBORONGA NIA NI WANASIASA WA UPEPO WANAOANGALIA UPEPO UNAVUMA WAPI. HUU UGOMVI WA UDINI NI UMAFIA WA HAO JAMAA.MSIMSINGIZIE KIKWETE,KWANI KIKWETE KAMA KIONGOZI WA NCHI NA MGOMBEA ALIWASIHI MARA KWA MARA WATANZANIA KUWA HAWACHAGUI SHEIKH WALA ASKOFU BALI WANAMCHAGUA MTANZANIA WA KUONGOZA WATANZANIA WA DINI MBALIMBALI JAPO NI WAZI KULIKUWEPO NA USHABIKI WA KIDINI KWA PANDE ZOTE MBILI KUTOKANA NA UDUNI WA FIKRA,HATA KINACHOTOKEA SUMBAWANGA NI HASIRA ZA PADRI SHETANI ALIYEJAA NA UDINI NA KUZUSHA MAMBO YA UONGO KWA MGOMBEA WA CCM. HUYO MBUNGE KISHAKANUSHA LAJINI YEYE HAWEKI WAZI KANISA LILITOA AGIZO GANI

    ReplyDelete
  34. Chadema matatizo yenu msitafute mchawi,mchawi wenu ni uroho wa madaraka,mlikuwa kidogo mkaweza kufanya mnayoyataka na sasa mko wengi mtegemee pia matatizo mengi,msiseme ccm kwani nao wana matatizo yao wanayatatua wenyewe bila kusema ni pandikizi la Chadema. Wanasiasa wa Tanzania mmegeuza siasa mgodi wa kuwanyonya wananchi hivyo vurugu katika vyama hazitakwisha mpaka pale ruzuku na marupurupu na mafao makubwa kwenye siasa yaondolewe na kwa namna fulani nakubaliana na huyo aliyeandika hapo juu,ruzuku ilikuwa ni kutokana na uchanga wa vyama sasa toka 1995 hadi 2010 hamna uchanga tena hiyo ruzuku iondolewe na vyama viishi kutokana na mchango wa wanachama wao,inashangaza wasomi wazuri sana,madaktari,mainjinia na wengineo wengi wamezikimbia taaluma zao kukimbilia kwenye siasa kutokana na mlo mkubwa huko

    ReplyDelete
  35. HATA MIMI NISIYEKUWA MWANACHAMA WA CHADEMA SINA IMANI NA ZITO. Hivi kweli mtu mwenye ushawishi na umaarufu mkubwa CHADEMA, na KIGOMA atashindwa kuongeza jimbo lingine kwenye mkoa au wilaya yake? Hivi ni kweli NCCR walikuwa na ushawishi mkubwa kuliko ZITO huko Kigoma? Kwa nini hakuwakampenia wenzake wa CDM wakati kwake hakukuwa na hofu ya kushindwa?
    Hana uzalendo kwa chama chake. Nahisi amaikampenia NCCR Kigoma, sio CDM.

    Wengi tulikipa CDM na wabunge wake kura kwa sababu ya SLAA, naamini Kigoma pia wangewapa wabunge wa CDM kura ila ZITO alikuwa kinyume na CDM tangu mwanzo wa kampeni. Lazima ana maagano na watu wa CCM na wa NCCR.

    Ukilinganisha mchango wa viongozi wengine wa CDM kwenye uchaguzi uliopita utagundua kuwa ZITO amechangia kuokoa jimboni kwake tu! Sasa huyu ni kiongozi wa taifa au ni kiongozi wa jimbo tu! Hafai kuwa kiongozi wa taifa. Kiongozi wa taifa anatakiwa achangie mafanikio kwa majimbo mengi zaidi ya jimbo lake!

    Zito kama naibu Katibu mkuu ambaye wakati wa Kampeni alibeba majukuma ya SLAA alitakiwa kuonyesha mchango mkubwa kwa SLAA kuliko viongozi wote wa CDM na sio kumzunguka SLAA na kuwa na uhusiano na wapinzani(kama RA na afande wa usalama wa taifa) wa CDM, na juzi kumpeleka EL kuwashawishi wabunge wa CDM kumsikiliza Kikwete.

    Hivi kweli askari gani ataenda kuongea na adui bila kuwasiliana na wenzake? Hivi kweli yeye akiwa mwenyekiti wa CDM atawashirikisha wenzake kwenye maamuzi? Sidhani!!!

    Ushauri wangu kwa CDM: Mwondoeni mtu kama huyu kwenye uongozi, kutoka bungeni hata chamani. Ajifunze kuheshimu viongozi na madaraka aliyopewa. Ni hatari kumpa strategy za chama mtu kama yeye! Haaminiki! Hata CCM wanaomtumia hawatampa hata ubunge!

    ReplyDelete
  36. Mimi ninakuunga mkono mtoa maoni hapo juu, huyu ZITTO amekuwa ni matatizo chadema, ni afadhali avuliwe uwongozi aanze kupiga kampeni za maendeleo ya wananchi. Mimi sio mchaga lakini sioni ukabila wowote, na wala udini. Hawa waropokaji wanalao kwanza ukiwauliza wao ni chama gani hawajui ndio wanao hama vyama kila kukicha ndio waroho na walevi wa madaraka. Mbinu zao chafu zitajitokeza tu muda sio mrefu. CHADEMA tuungane tuachane na hawa mapobo bawa, kwanza wananuksi. Kama wamerizika sasa si watulie wajenge nchi wasubiri Chadema wafanye mambo yao, kwa nini wanatoa maneno ya uchochezi. KIDUMU CHADEMA.

    SALUM CHILEWA. (KIGOMA)

    ReplyDelete
  37. Dawa ya kuondoa na kuepuka vurugu na migogoro katika vyama ni kuondoa hizo ruzuku. Kwa mfano kama Chadema walichangiwa 200m na Jafarjee (Sabodo) peke yake na tena baada ya uchaguzi kawapa 150m nina imani kuna wanachama wengine wanachangia pia (ingawa Sabodo ni CCM) chama chao. kwa hiyo umefika wakati sasa kwa serikali kuondoa RUZUKU Na MARUPURUPU kibao ya wanasiasa, wawe wanalipwa Mishahara kama watumishi wengine wa umma ndio hapo tutakapojua pumba zipi na mchele ni upi!

    ReplyDelete