14 December 2010

Ancelotti aridhishwa na kiwango

LONDON, England

KOCHA Carlo Ancelotti ameridhishwa na kiwango cha  Chelsea ilichoonesha katika mchezo ambao timu hiyo walitoka sare ya bao  1-1 na Tottenham, baada ya kuchechemea katika siku za hizi karibuni.Blues imeshindwa kupata ushindi katika mechi
kadhaa za Ligi Kuu,  wakati ikieelekea kwenye mechi ya Jumapili katika Uwanja wa White Hart Lane, na kwa mara nyingine ikashuhudiwa ikiambulia pointi moja.

Timu hiyo ilikuwa ikikaribia kupata ushindi, lakini ikashuhudiwa penalti iliyochongwa na Didier Drogba dakika za nyongeza, ikipanguliwa na kipa, Heurelho Gomes.

Hata hivyo, Ancelotti anakiri kuwa, matokeo hayo yanafadhaisha, lakini anahisi kuwa, Chelsea ilicheza vizuri kiasi cha kutosha na akaeleza kwamba, sasa wimbi lililokuwa limewafunika, limetoweka.
"Ni muhimu mno kushinda , tulistahili kushinda, lakini hatukuweza kufanya hivyo," alisema Muitaliano huyo.

"Nadhani tupo katika njia sahihi. Mechi hii imeonesha kuwa, tuko njiani kurejea katika kiwangio chetu, tumecheza vizuri, tulianza vizuri na tulipokuwa nyuma, hatukupoteza morali wetu wa kudhibiti soka," aliongeza kabla ya kusema kwamba, walistahili kushinda na walikaribia kufanya hivyo, huku akijipa matumaini ya kuwa, watashinda mechi ijayo.

No comments:

Post a Comment