30 December 2010

Wakamatwa wakinadi nyeti za baba yao

Na Cresensia Kapinga,Songea

JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limewakamata ndugu wawili wakitafuta soko la viungo vya binadamu walivyotarajia kupita kwa kumuua baba yao mzazi.Vijana hao walikamatwa wakitafuta soko hilo kwa mfanyabiashara maarufu wa mafuta katika
manispaa ya Songea.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 6:00 usiku katika eneo la Msamala mjini hapa, kwenye ofisi ya kampuni moja ambayo inajishughulisha na uuzaji wa mafuta na usafirishaji wa abiria.

Alisema kuwa watu wawili ambao ni Mohamed Mohamed (25) na Hashim Yasin (25) wote wakazi wa Kijiji cha Hanga Monasteri wilayani Namtumbo, walifika kwenye ofisi hiyo na kumkuta mkurugenzi wa kampuni na  kumueleza kuwa wana viungo vya binadamu ambavyo wanataka kumuuzia.

Baada ya mazungumzo, watu hao walikubaliana kuwa viungo hivyo ni sehemu za siri za baba yao, ambazo zingeuzwa kwa sh. milioni sita na za kaka yao kwa sh. milioni tatu.

Baada ya makubaliano hayo, mkurugenzi huyo aliwasiliana na polisi ambao waliweka mtego na kufanikiwa kuwanasa watuhumiwa hao.

Kamanda Kamuhanda alisema kuwa watuhumiwa hao baada ya kuhojiwa na polisi kuhusiana na madai hayo walikiri na kuwa walikuwa na mpango wa kwenda Tunduru kuwaua baba yao na kaka yao ili wafanikiwe kuchukua viungo hivyo na kuviuza kwa mfanyabishara huyo.

5 comments:

  1. Yale yale! watu hawa wamejuaje kwamba mfanyabiashara huyo ananunua viungo vya binadamu! Pengine kauchunguzi kanahitajika maana kufikisha taarifa polisi haina maana wewe si mhalifu.

    ReplyDelete
  2. kweli kabisa,huenda jamaa kashtukia jambo akaona la maana awaangushie jumba bovu hao jamaa,kamata naye weka ndani asaidie jeshi la polisi

    ReplyDelete
  3. There is more to this story than eyes can see! It sounds hard to believe, they must have done it successfully in the past, but this time something went wrong somewhere! Ama kweli mwisho wa ubaya ni Aibu!

    ReplyDelete
  4. They are all partners in CRIME !

    ReplyDelete
  5. Jamani watanganyika mmekutwa na nini? Mbona matokeo kama haya husikii kutokea upande wa Zanzibar? Hapo ndipo wenzenu hao wanapokuwa na mashaka nanyi na wakahitaji kuwepo na njia ya kudhibiti uingiaji wa watu kwa kuhofia huo ushenzi wenu.

    ReplyDelete