Na Daud Magesa, Mwanza
VIMWANA na wanawake wenye sifa za kuwania taji la Kisura wa Tanzania linaloendeshwa na kampuni ya Beautifully Tanzania Agency (BTA), wametakiwa kujitokeza kwenye usaili utakaofanyika kesho mkoani Mara.Mratibu wa mashindano
hayo, ambaye ni kisura anayemaliza muda wake, Diana Ibrahim, jana jijini Mwanza, alisema wasichana wenye vigezo vya kuwania taji, wajitokeza kwenye usaili.
Malkia huyo wa BTA , alisema mashindano hayo yatafanyika mwakani, ambapo mkoa wa Mara, usaili utafanyika kesho katika ukumbi wa hoteli ya Mativila.
Kisura huyo alisema usaili wa mkoani Shinyanga umepangwa kufanyika Desemba 16, katika hoteli ya Ibanza mkoani humo.
Diana alisema washiriki watachujwa na kila mkoa utatoa washiriki wawili watakaoingia kambini mwezi mmoja jijini Dar es Salaam, watachujwa na kubaki 10 ambao watakaoingia fainali.
Fainali ya mashindano hayo itafanyika Machi mwakani jijini humo.
Alivitaja vigezo vitakavyotumika kuwapata visura hao ni urefu wa sm 174, nyonga sm 36 kushuka chini, na kiuno sm 64 yabila kujali kuwa, ameolewa ama hajaolewa.
Diana alirithi nafasi hiyo kwa mshindi Emmy Milao ambaye alishinda mwaka 2008.Alisema mshindi atazawadiwa kitita cha fedha na mkataba wa kazi na kampuni mbalimbali, na kunufaika na mafunzo yanayohusu ugonjwa wa Ukimwi.
Wadhamini wa mashindano hayo ni Family Health International (FHI), Kituo cha Televisheni cha TBC 1, Baraza la Sanaa na Taifa (BASATA), Clouds FM, SBC Tanzania Ltd, TanForm Arusha, Kiromo View Hotel, Flare Magazine na Hugo Domingo& GRM Production.
No comments:
Post a Comment