Na Omary Mngindo, Chalinze
WADAU wa Michezo wa Chalinze Mkoani Pwani, wameuomba uongozi wa Chama Cha Mpira wa Miguu Pwani (COREFA) kuweka kituo cha Ligi ya Taifa ngazi ya mkoa katika mji huo.Wakizungumza na mjini hapa juzi, wadau hao Moses Monja na
Hamad Paroko walisema kwa miaka mingi sasa hawajawahi kuonja ligi taifa ngazi ya mkoa hali inayowafaywa mwaka huu watume ombi hilo kupitia vyombo vya habari.
Walisema kuwa mara ya mwisho kuona ligi hiyo ni wakati wa uongozi wa Mwenyekiti wa COREFA, Imani Mdega hali waliyoielezea ni kipindi kirefu hivyo wanauomba uongozi wa sasa chini ya Mwenyekiti, Hassan Othuman waukumbuke mji huo.
"Mji wetu wa Chalinze una wadau wengi wanaopenda na kufuatilia michezo hususani soka kwa ukaribu na katika miaka yote tuliyopewa kituo,tumekuwa tukijitokeza kwa wingi kushuhudia ligi hiyo kwa kuingia kwa fedha hali ambayo uongozi ulikuwa haupati hasara ya kuwalipa waamuzi," alisema Mojna.
Kwa upande wake Paroko alieleza kwamba kutokana na kukosa kushuhudia ligi kwa miaka mingi, wadau hao wanahamu kubwa ya kushuhudia ligi hiyo ya mkoa hivyo wameomba wakumbukwe kwa msimu huu.
"Kwa kuwa ombi letu lina nia njema ya kujenga pia kutoa msaada kwa uongozi wa COREFA ni imani yetu kubwa kwamba ombi hilo litakubaliwa na kupatiwa kituo mwaka huu," alisema mdau huyo.
Hivi sasa wilaya zote sita zilizomo ndani ya mkoa wa Pwani zinaendesha ligi zao ambazo zitatoa washindi watatu wataocheza ligi ya mkoa na kufanya jumla ya timu 18 kushiriki kinyang'anyiro hicho kitachompata bingwa wa mkoa.
No comments:
Post a Comment