10 December 2010

Chadema wasusa sherehe za Uhuru


WA K AT I Ra i s Jakaya Kikwete akiongoza maelfu y a Watanzania katika maadhimisho ya miaka 49 ya Uhuru wa Tanzania Bara, viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hawakuonekana
kwenye maadhimisho hayo.

Tukio hilo lilijionesha jana katika uwanja wa Taifa ambako ndiko sherehe za uhuru zilifanyika na kuhudhuriwa
na viongozi mbalimbali wa kiserikali wakiwemo waZanzibar na Muungano na wa vyama vya kisiasa na wananchi kwa ujumlaInatoka uk. 1 kwa kukosa huduma, elimu bado ni duni hivyo tunaposherehekea
uhuru hatuhitaji kuona magari mengi na makubwa ya viongozi bali tunataka kuona huduma zinakuwa bora na zinapatikana kirahisi,” alisema Prof. Lipumba.

Naye Mwenyekiti wa Chama  cha NCCR Mageuzi, Bw. James Mbatia alisema kuwa miaka 49 ya uhuru bado hali si nzuri kwa kuwa bado kuna changamoto za kushuka kwa uzalendo, ufisadi kuongezeka pamoja nammomonyoko wa maadili mambo ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi ili nchi iweze kubaki katika misingi inayotakiwa.

Mbali na hao, mbunge wa Wawi, Bw. Hamad Rashid alisemakuwa katika maadhimisho hayo wananchi wanatakiwa kupiga kelele katika masuala ya rushwaambayo bado inaonekana kuwa tatizo na linalosababisha hataviongozi kupatikana kwa njia zisizo halali.“Bado kuna tatizo la rushwa linalosababisha viongozi kuingia madarakani isivyo halali na ndio maana CUF tunalilia mabadiliko ya katiba, tume ya uchaguzi, sheria za uchaguzi ili tuweze kufanya mambo ambayo kila mmoja ataridhika nayo,” alisema Bw. Rashid.A l i s e m a k u w a w a k a t i tunaadhimisha miaka 49 ya uhuru bado matumizi ya rasilimali za nchi hayako sawa hali nayosababisha nchi kubaki na matatizo kama ya umeme, mfumko wa bei na haya yanatokana na rasilimali
kutotumika ipasavyo hivyo Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba alisema kuwa hatua ya CHADEMA kususa sherehe hizo ni kutokomaa kisiasa kwa kuwa suala hilo linagusa Watanzania wote na si la kisiasa.

“Tupo kwenye mfumo wa vyama vingi lakini kwenye sherehe kama hii CHADEMA hawakupaswa kutoshiriki kwa kuwa haligusi itikadi za kichama, hivyo kitendo cha kususa ni cha kuwasusia Watanzania,” alisema
Prof. Lipumba. Akizungumzia changamoto ambazo bado zinaikabili nchi kwa sasa tangu Uhuru upatikane,
alisema bado kuna tatizo kubwa la kutoonekana matunda ya uhuru ambayo wananchi wanahitaji
kuyaona.
“Bado matunda ya uhuruhatujayaona...wakati tunapata uhuru kaulimbiu ilikuwa ni ‘uhuru na kazi’ na lengo lake lilikuwa ni baada ya uhuru ajira zipatikane lakini mpaka sasa sekta hiyo bado ni tatizo kubwa.
Kutokana na hali hiyo, Profesa aliutaka uongozi ulioko madarakani kujielekeza katika matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo nchini kama misitu, maji, madini na zingine katika kuboresha huduma mbalimbali
za kijamii na kuleta maendeleoya nchi.
“Inatisha kuona bado tuna tatizo la vifo vya akina mama wajawazito akasisitiza matumizi sahihi ya
rasilimali ili uhuru uliopatikana kutoka kwa mkoloni uweze kunufaisha Watanzania.

Wakati huo huo, Prof. Lipumba aliwabeza watu wanaopinga Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na kusema kuwa wanaofanya hivyo hawaitakii mema nchi hiyo na Tanzania kwa ujumla na kama ni wanasiasa
hawajui wanachokifanya. “Hatua hii imetibu majeraha yaliyokuwepo na kuwaunganisha Wazanzibari...walikubaliana kuwa na serikali hii ili iwaunganishe na kumaliza matatizo yaliyokuwepo
tangu awali ambayo hayakuwa na amani hata kidogo na ukiwa unazungumzia serikali hii kwa Zanzibar vyama vyenye nguvu ni CUF na CCM ambavyo vimeungana na kama kuna mtu anaona kuna kosa haitakii mema
na kama ni kiongozi wa kisiasa basi si mwenye busara na kama ana shughuli zake zingine kama za disko basi aende huko na sio kazi ya siasa kwani ukibeza hatua hiyo basi hujui siasa na huijui Zanzibar,” alisema Prof.
Lipumba.

Viongozi waliohudhuria sherehe hizo mbali na Rais Kikwete, ni Rais wa Zanzibar, Dkt.Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Bw. Seif Sharif Hamad, Rais Mstaafu wa Tanzania, Bw. Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Bw.Aman Abeid Karume, Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Gharib
Bilal, Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda, Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda na Jaji Mkuu wa Tanzania
Bw. Augustino Ramadhan. Mbali na hao pia mabalozi wa nchi mbalimbali, makatibu wakuu wa wizara, mawaziri na wengine
wengi.
Katika maadhimisho hayo mizinga 21 ilipigwa kwa heshima ya Amiri Jeshi Mkuu huku halaiki ya wanafunzi 700 wa shule za msingi wakinogesha sherehe hizo

44 comments:

  1. Prof. Pumba amesahau ya kule Zanzibar walivyo kuwa wanasusia. Au kwa vile kinachoitwa muafaka kinamnufaisha kwa kujipatia vijisenti? Wao ni CCM-B hivyo hakuna haja ya kuwasemea upinzani. Na kama yeye amekomaa kisiasa mbona ktk chaguzi zote anaambulia patupu?

    ReplyDelete
  2. Kaka Anonimous umesema ukweli CUF ni wazandiki, Wanafiki na wanasahau historia. Wao walikua vinara wa migoma sasa wamekua CCM B wanaona wenzao wanafanya makosa.

    ReplyDelete
  3. Kuhudhuria au kutohudhuria sherehe za kumbukumbu za Uhuru si hoja sana kwangu, kwani sijui kama hiyo ni lazima kwa kila mtu. Jambo linalonikera mimi ni kwamba tunakwenda kusherekea nini? Matumaini yetu ni yapi kama Taifa? Kama mtu hakuenda uwanjani na maisha yake ni bora kuna tatizo gani? lakini utaona mtu amekwenda uwanjani analalamika kuwa maisha ni magumu huku wakubwa wanasikia halafu wanaelekea kwenye viyoyozi vya mashangingi yao (yetu) na wengine wakichapa kiguu na njia kuwahi daladala ya kwenda Mbagala. Hapa ndipo naona Tatizo. Tunakwenda kusherehekea Uhuru wa NANI? Nadhani tunakwenda kuwaunga wenzetu washerehekee baada ya kupata Ulaji. Maana kila siku ni maisha ni afadhali ya jana kuliko leo. Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  4. Wabara wanapaswa kuamka sasa ili wasichezewe na wazanzibar ambao nia yao ni kufaidi Muungano wa Tanzania na Zanzibar huku sisi wabara tukiendelea kuwabembeleza. Wao wakijifanya wanaonewa kumbe wanatufirisi. Sasa ebu angalia wao wana rais, makamu wa rais wa Muungano, makamu wawili wote hao wananufaika na wabara! Sisi tumebaki na rais na waziri mkuu! Hivi haki iko wapi hapo? Mimi ninaona hatuna haja na Muungano unaobembeleza upande mmoja. Ili wenyewe uendelee kufaidika. Jamani East Africa Community inakuja wazanzibar wafuate mambo yao ili wajiunge kwenye jumuiya Africa Mashariki kama Nchi. Tunawaongezea ajira bure tu. Wawe na wabunge wa Muungano, mawaziri wa Muungano. Kila kitu cha kwao tutawabembeleza mpaka lini huku wakitutawala kwa namna ambayo hatujijui. Tena wana udini mkubwa hawa. Wapemba wamejaa kila mahali Tanzania bara, wakati wabara hawatakiwi Pemba haki iko wapi? Wengi vijana wa siku za leo hawaoni umhimu wa Muungano unaonyonya upande mmoja.

    Chadema tunaomba wakaze uzi ili watanganyika tukombolewe kwenye minyololo ya utawala wa Wazanzibar. Chadema itashinda kwa sababu inasimamia haki. Hata kama sio leo lakini vijana wengi wameelimika na mwaka 2015 kundi hili litakuwa kubwa zaidi. Tunasema mabadiliko lazima wapemba lazima waondoke bongo warudi kwao. Chedema Oyeeee mmefanya vizuri kumsusia Kikwete! Sasa hivi anataka kuanzisha mahakama ya Kadhi. Tatizo la Muislam hata kama amesoma kichwani mwake ni kuwaza madrasa tu. Kikwete anatakiwa aende kuendesha msikiti na kiti cha urais.

    ReplyDelete
  5. Anonymous wa mwisho hapa, niko nawe kwa sana. Tanganyika tujikomboe na sisi. Kwa Lipumba sinshangai sana kwa sababu dhamira yake ni kupata MIMI na si kupata SOTE. Ameombwa na nani kutolea maoni CHADEMA? Acha kisjisemee chenyewe. Kweli Nyani haoni...............

    ReplyDelete
  6. WATU WA ZANZIBAR NI WANAFIKI,MABWABWA MENGI HUKO NDIO MAANA HATA HUJUI UMUAMINI NANI.

    ReplyDelete
  7. Nawaunga mkono wote walioyayatoa hapo juu. Lipumba acha unafiki, wewe siyo mpinzani ni CCM kivuli wanainchi tumeligundua hilo. Hapo Uhuru tuliokuwa tunausherekea ni 49 Uhuru wa mafisadi kutafuna nchi na kutugandamiza. Hivyo nawapa heko Chadema kwa kutohudhuria maana ni ufisadi tu, hakuna cha kusherekea pale zaidi ya kuona mishangingi na suti na vitenge vya gharama wakati wabongo umeme mnatupa wa mgao na vitu vinazidi kupanda bei kila kukicha. Ufisadi mtupu sisi vijana tunawaambia mliopo madarakani rekebesheni hayo la sivyo 2015 hampati kitu.

    ReplyDelete
  8. HUYU LIPUMBA NINA MASHAKA NA UPROFESA WAKE, HIVI KWELI KUNA PROFESA WA KWELI ANAKUWA NA USAHAULIFU KIASI HIKI KAMA YULE MNYAMA ANAYEITWA PIMBI? ANAYESAHAU HATA MKIA WAKE AKAUNG'ATA KAMA ADUE YAKE? LIPUMBA KWELI NI PUMBA TUU. HATA HISTORIA YAKE AKIWA UDSM INAONYESHA WANAFUNZI WAKE 90% WALIKUWA WANAFELI. LEO HATA UKIMULIZA AMEPATA KURA NGAPI HAKUMBUKI. MPUUZENI LIPUMBA HANA AKILI YA KUCHAMBUA MAMBO. MPUUZENI MPUUZENI MWISHO NAOMBA ELIMU YAKE ICHUNGUZWE.

    ReplyDelete
  9. Lipumba ni political reject,hana vision ndio sababu anang'ania chama ambacho hakina locus stand huku bara,ni chAma cha kidini cha mwelekeo wa OIC.Bora akae kimya ale hivyo viposho anavyopewa otherwise he is wasting his time as he becomes more and more unpopular

    ReplyDelete
  10. kwa ukweli prof.lipumba yupo sahihi.kwani Z'bar waliuwawa sana mbona aukushabikia kipindi cha mkapa au kwa sababu Jakaya. acheni ushabiki wa kidini kwani kanisa mbona lina ubalozi wa italy(roma)pamoja na mwakilishi wa papa hapa wote hawa wanini.unajua hilo tafakari.wanao mjua lipumba wanamthamini

    ReplyDelete
  11. Uhuru unaotakiwa kusherekewa ni ule unaowajali wananchi au walau unaoonyesha mwelekeo huo.Watu wanateseka halafu mtu anataoa maoni kwa nini fulani hajaudhuria:Waliohudhuria wamefaidika na nini?Viongozi watanzania mbadilike watanzanai hawako tayari kuja kuangalia mmevaa nguo za gharama gani?Pia maudhui ya sherehe yabadalishwe badala ya kuja uwanjani kuangalia gwaride na ndege za kivita iwe siku ya mdahalo wa ktaifa hapo uwanjani ili watu wajadili maisha yao yajayo

    ReplyDelete
  12. Hapa kinachojadiliwa ni Chadema kutohudhuria sherehe za Uhuru sasa masuala ya udini yanatoka wapi? kuweni wastaarabu wa kuheshimu dini za wengine,siasa sio ugomvi,chuki,fitna,udini nk bali ni fikra na mitizamo inayokubalika katika jamii. sasa leteni hoja za chadema kususia sio udini.

    ReplyDelete
  13. huyu lipumba anahitaji antivirus anaonekana kaingiliwa na virus wa rangi ya kijani na manjano

    ReplyDelete
  14. hivyo kweli wabongo mko tayari kuliachia koloni lenu la zanzibar ? kama mko kweli basi tambueni uwepo zanzibar kama nchi kisha muone jee zanzibar itakuwa omba omba ! hayo yanyofanywa na CUF ni matokeo ya mbegu mliyoipanda wenyewe kama msingeunganisha nchi kwa janja ya Mwalim JKN 1964 MSINGEKUWA NA HOJA HIZOLEO NA MLIONA HAMJATOSHEKA MKALAZIMISHA MUUNGANO WA VYAMA TANU NA ASP ACHENI WANA CUF SASA WAWWZUNGUKE NA UKWELI UJE KISHA TUONE KAMA KWELI NINYI NI WAZALENDO WA TANGANYIKA

    ReplyDelete
  15. ni kweli kabisa namuunga mkono mtoa mada ya hoja,hapa kweli kitakiwacho ni hoja na sio uzanzibar au ubara au udini hivi vitu vinaturudisha nyuma siku zote acheni habari za ubaguzi na udini sisi sote ni watanzania,tushachanganya damu hata muungano ukifa lkain udugu hawezi vunjwa na muungano kwa hiyo kama watu wenye vision mnaapoongelea masula ya muungano na hio mlione.by mkereketwa

    ReplyDelete
  16. •Nawafahamisha Watanganyika kuwa Wamejidhani wajanja kwa muda mrefu kwa mbinu za Mbuni kufukia kichwa akidhani kajificha. Tumwewaonjesha asali wamepata ladha ya shubiri, kelele kila upande. Lakini hizo sheria walizokuwa wakizitumia kujenga ufisadi wao, leo hii waona dhahiri kuwa walichotenda kilikuwa ni KUCHAMBA KWINGI. Na ZANZIBAR inapo wadhihirishia kwa vitendo, sheria zao huwaporomokea wakashindwa lakutenda.
    Nyerere alipofika Makerere kama Mtanganyika wa mwanzo kati ya umma usopunguwa milioni 15 wakati huo, alikuta tayari WAZANZIBARI wakimkaribisha sio tu kama wanafunzi bali hata walimu pia na wakati huo jamii ya kizanzibari haikufika hata nusu milioni. Leo hii Watanganyika wanajifanya wamesoma sana kushinda Wanzazibar
    Kwa hivyo hawa sio wajanja, walidhani wakitumia nguvu na leo wameanza kubaini kuwa ilikuwa ni nguvu ya mshumaa dhidi ya moto, huchachamaa hatimae humung’unyuka taratibu.
    KAMA KUNA KITU NATAMANI BASI NI KUWA NYERERE ANGEKUWA HAI LEO HII AKAMUONA SHARIFF HAMAD AMEKUWA MAKAMO WA RAIS VISIWANI KABLA HAJAVIONA VISIWA HIVYO VIKIELEKEA KULE ALIKOTAMANI

    ReplyDelete
  17. MUUNGANO UNAO SHEREKEWA NI ULE WA MANUFAA YA WOTE NA SIMUUGANO WA KIKUNDI AMBACHO HALIJALI MWANANCHI WA CHINI, TUMECHO KUDANGANYWA NA WANA CCM, ACHENI CHADEMA WANAAKILI SANA NA WANAWEZA KUWA WAKOMBOZI TATIZONI KUWEPO KWAKUNDIKUBWA LA WATU KAMA LIPUMBA AMBAO WANABADILIKA KUTOKANA NA WAKATI, WAKISHA PATA MWANYA WA KUJIPATIAVISENTI BASI WANASAHAU AHADI ZAO, WENGINE WENGI AMBAO HAWATAKI MABADILIKO. NAHUU UDINI MLIONG'ANG'ANIA LAITI MNGESHUGHULIKIA YALE YA MANUFAANDIYO HUO UHURU WA BANDERA TULIO NAO, NIBAHATI MBAY KWAMBA ANGALAU KABLA YA UHURU TULIJUA TUNAGANDAMIZWA NA WAZUNGU, LAKINI CHAKUSIKITUSHA NI LEO HII TUNA GANTAMIZWA NA WATANZANIA WENZETU WANAOJIFANYA VIONGOZI WETU LAKINI NI KWAMANUFAA YAO HAWAANGALII WANYONGE WANAISHIA KUSEMA MAISHA BORA KWAKILA MTANZANIA WAPINAWAPI. CHADEMA OYEEEEEEE

    ReplyDelete
  18. Wee mwandishi ulikuwa huna kazi ya kufanya ukafanya mahajiano na huyo PUMBA kwani ni mpinzani. Upinzani umewashinda hawa CUF. CHADEMA kutokuhudhuria sherehe ya uhuru ni jinsi walivyoo na uchungu na nchi yao. Kwanza ni uhuru gani alionao huyu mtanzania, wakibepari, Angalia maisha anayoishi alafu ulete kwenye picha ya uhuru. Wee LIPUMBA uko mjini nenda vijijini ukaone uhuru walionao na walisherekea kama wewe. CHADEMA msife moyo uzi huohuo mpaka kieleweke.

    ReplyDelete
  19. CHADEMA WAKO SAWA,MAGEUZI YA DEMOKRASIA NI GHARAMA NA HUKO NDIKO TUNAKOELEKEA!!NAWAUNGA MKONO CHADEMA....KWA GHARAMA YOYOTE TUTAFANYA MAGEUZI NDANI YA NCHI HII.

    ReplyDelete
  20. Bado watanzania tuko nyuma kimawazo na tunazidi kulemaa siku hadi siku. Hivi matanzania wa kawaida akiulizwa anachosherkea nini atajibu nini? Je ni kuona hayo magari ya mafisadi na gwaride la jeshi au ni kuona nyuso za mafisadi wapya?? Tunasherekea Uhuru tukiwa hatuna umeme wa uhakika, mashule hayana madawati, walimu wa kutosha hakuna. KWA HIYO TUNASHEREKEA NINI??

    ReplyDelete
  21. CUF NA CCM NI KITU KIMOJA KIKWETE HAFAI KUWA RAHISI WA NCHI NI MLIPIZA VISASI SANA. CHADEMAA KOMAAA 2015 NCHI NI YAKO NDIO MAANA CUF WANAFUNGA NDOA YA MKEKA WAKIDHANI WATASHINDA. CHADEMA MSIUNGANE NA CUF WALA NCCR WALA TLP WOTE HAWA NI VIBARAKA VYA KIKWETE NA CCM YAKE TNAWAJUA SANA HAWA JAMAA NI NDUMI LA KUWILI. HALAFU CHADEMA TUMIENI KILA MBINU MUMFUKUZE ZITTO HAFAI KABISA KWENYE CHAMA ANAFANANA NA WAKINA LIPUMBA, MBATIA KAFULILA NA MREMA WA TPL HAFAI KABISA USE ANY MEANS POSSIBLE TO THROW THIS YOUNG CHICK POTICIAN OUT THE SYSTEM HE IS UNFIT FOR BEING THERE HE IS A POISONOUS TOOTH IN THE FRESH MOUTH

    ReplyDelete
  22. kuna waonadika udini eti CUF ni ya kiislamu ! je hiyo chanyavu(chadema)ni ya kikristo ? CCM ni ya kanisa ? mbona pana balozi wa Vatican hapa nchini ? wa kazi gani balozi huyu ? je tanzania ni nchi ya kikatoliki ? Chadema mnachofanya ni fotokopi ya waliofanya cuf kule Zanzibar na hakuna jipya mtakalolifanya kwani wakati ule damu inamwaika kule zenji huku bara hakukuwa na kauli ila kuwa wazenji ni watu walozoea vita.......je upepo umegeuka sasa ? la muhimu ni kuwa Chadema wanataka nao muwafaka kama ccm na cuf !! kwani ndio njia pekee ya kujaribu kuianusha ccm.sifikirii kama cuf ni chama cha kidini ila hao wenye mawazo kama haya sasa waseme na kuwa ccm na chadema ni vya kidini pia.
    mtu anaweza kuchukia hili ila ndio ukweli kwani cuf walifanya hivi na sasa chanyavu nao waiga tu !!! hawana jipya na kama wana moyo basi wabunge wao waichukue pesa kama walivyofanya cuf..hapo tutajua kweli wanafanya na sio maigizo kama yalivyo sasa.
    Baadae watataka muafaka ...........
    ndio yale yale labda na baadae kura ya maoni hapa bara kama vile zenji
    naona hii ni ile hadithi ya cuf kujirudia ila mara hii ni huku bara .
    De Panne-België

    ReplyDelete
  23. wewe Anonymous wa mwisho kama hauna maoni siungelala tu waachieni wengine, naona unaandika utumbo na pumba za lipumba we shabiki wa ccm ns Cuf Without Succes. utashio tu kuwakondelea macho na kuwaangalia sura zao.

    Kinachojadiliwa ni swala la chadema kususa sherehe za uhuru sio udini na muungano.

    Nini kilichomfanya huyu Pumba atoe habari kuwa chadema wasusa sherehee za uhuru? kwani chadema wenyewe hawana midomo? Lipumba acha unafiki, tunajua kuwa wewe saizi ni CCM damu na Cuf ni mke mwenza na ccm. Kwa hiyo Lipumba acha kutoa habari zisizo kuhusu kwenye vymbo vya habari kwani chedema wao wamekwambia wamesusa? Pamoja na hilo hakuna uhuru wowote Tz zaidi ni kusherekea mafanikio ya mafisadi kuendelea kuifisadi nchi yetu.

    Goodbyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

    Writeneeeeeeeeeeeeee by Jm:a;f'old*R

    ReplyDelete
  24. anonymous wa 2 toka mwisho, Nadhani huana unachosema pia inawezekana una mawazo yaliyoganda, nakushauri uongee sense na si kukurupuka, msaliti wewe na kwa taarifa yako mwafaka wa CUF na CCM ni mwafaka hewa na ni mwafaka wa chumbani - wa mtu na mpenzi wake na siyo mwafaka wa heri hata kidogo ni mwafaka unaoleta ubaguzi na nyufa, na CHADEMA inaangalia nchi nzima wakiwemo CUF na wengine wote wasio kuwa na chama...pole sana

    ReplyDelete
  25. katika move zote za CUF za msuguano kati yake na CCM hata siku moja haijawahi kusikika chama chochote cha upinzani hapa TZ kilichotoa statement ya ku-discourage move ya CUF and naamini vyama vyote vilikuwa against ccm..sasa nashangaa huyu Lipumba katoa wapi hii confidence ya kuwavunja wenzake moyo na kuongea mambo ya kisengere nyuma?mie nilimuona Lipumba is a fool of himself pale alipokabidhi sera CUF kwa Kikwete, nilifahamu kabisa CUF ni CCM B na ni Photcopy yake (CCM), tumewazoea CUF ni wanafiki na wapo kwajili ya kujikomba na wanapenda kupiga magoti na si wananchi na wazalendo wa kweli

    ReplyDelete
  26. Naogopa kusema sana zambi kwa manani, au nilie au ninunee.Lipumba u need to be carefully. usilopoke wewe mzee we sio msemaji wa chadema. Mumeungana na ccm kama mume na mke mkagawana madaraka huko Zanzbar alafu mnatuletea upumbavu wenu huku bara? kuto kufika kwenye shrehe za uhru ni maamuzi ya mtu huwezi kmlazimisha fisi kula nyasi wakati hali. kwa hiyo Lipumba haupo sahihi kabisa uliishiwa cha kuongeaaa na waandishi wa habri mtu na elimu yako ukaanza kuchnguza Slaa Hayupo Lissu hayupo ukaamua ulopoke tutakufunga hilo domo lako. chadema kazi buti 2pamjo.

    ReplyDelete
  27. Asanteni sana Majira kuruhusu maoni huru kama hivi. Ukienda michuzi wanazuia maoni ya kuunga mkono chadema. Majira mko juu. Chadema mko juu.

    ReplyDelete
  28. Hakuna haja ya kwenda uwanjani kusherehekea wakati una njaa! Utakuwa unasherehekea nini?
    Miaka 49 ya Uhuru lakini Maisha ya Mtanzania yanazidi kuwa magumu kuna haja gani ya kuwa na sherehe hizi?

    ReplyDelete
  29. *Vijana wafurika, wapigana visu
    *Wagombea makombo ya hotelini
    *Wizi warejea kwa kasi

    Na Waandishi Wetu, jijini

    KUNDI la vijana wamevamia katika dampo la Pugu Kinyamwezi kisha kuanza kuchakachua mabaki na uozo wa vyakula vinavyotoka kwenye mahoteli na kwenye mabucha kisha kuanza kugombea hadi kutishiana visu.

    Gazeti hili lilifanya uchunguzi katika dampo hilo na kushuhudia vijana hao wakiwa wamekaa pembeni wakisubiri magari ambayo wanayafahamu yakitoka kwenye mahoteli makubwa kisha kuanza kuchakua wakati magari hayo yakiendelea kumwaga uchafu huo.

    NDIO WANASHEREKEA SIKUKUU YA UHURU KAMA WATU WENGINE. MBONA HAWAAMBIWI WAMESUSA KWENDA KWENYE MAADHINISHO YA UHURU? KWANI SIO WATANZANIA KAMA WANAOAMBIWA WAMESUSA. JIBU LAKO HILO HAPO LIPUMBA!!!!!!!!!!!!.

    ReplyDelete
  30. kama ni udini basi CHADEMA ndio wadini na uthibitisho wa haya ni kanisa kuwafukuza waumini wao kwa sababu waliishabikia ccm badala ya chadema, kama mulikuwa munashabikia wazanzibari kuuwana wameshaona janja yenu kwa sasa wazanzibari kitu kimoja.

    ReplyDelete
  31. Anonymous wa 9 nadhani unaumwa tumbo, bora ungekwenda kujitibu kwanza maana itakuadhiri. Kwahiyo balozi wa Vatican ndo anawafanya nyie mtake mahakama ya kadhi!!!!! na huo udini umeotoka wapi wewe Anonymous said! shwaini!! wakati tunazungumzia kususa kwa CHADEMA, tatizo lenu nyie CCM (chama cha Mafisadi) na CUF mnapenda kutupandikiza udini na hilo tatizo mnalolipandikiza haki ya nani liwatafune wote ndani ya vyama vyenu Shwainiii!. watu wanachangia kususa kwa chadema nyie mnaleta udini. kalaleni huko.

    ReplyDelete
  32. JAMANI EEH NYIE HAMJUI KITU, CHADEMA HAWAJASUSA NA WALA HAWAJASEMA HAWAMTAMBUI RAIS NDIO MAANA WAKO BUNGENI WANAMTUMIKIA KUPITIA MHIMILI HUO WA DOLA.

    WASUSE WANAUMWA? Uliona wapi mchaga akasusa pesa wewee? Wacheni uwongo wenu hawajasusa ndio maana pesa wanachukua na na bungeni wanakwenda. Ushahidi kuwa hawajasusa ni pale walipoangalia hotuba ya Rais kwenye luninga, na hata hizi sherehe watakuwa wameziangalia kupitia luninga, hata wananchi wengine hawajaenda uwanjani wameangalia sherehe kwenye luninga.

    ILA WAO WANAOGOPA KUKUTANA USO KWA USO NA JK KUTOKANA NA MITUSI WALIYOKUWA WANAMWAGIA WAKATI WA KAMPENI, SASA MWENYEWE NDIO KESHAKUWA RAIS WATAMWANGALIAJE USONI? ni hayo tu masuala ya kuona aibu na haya maana uso wa mwanadamu umeumbwa na haya. Hata ningelikuwa mimi jamaa ningelikuwa namkwepa kila nikisikia yuko mahala fulani namkwepa.

    ILA NGONDO YA CUF CHADEMA HAWAIWEZI, MAANA WENZAO HATA PESA HAWAKUCHUKUA HUKO NDIKO KUSUSIA SIO MCHEZO WA KITOTO WANAOUFANYA TUNATAKA WASUSE KIKWELI KIKWELI WASIINGIE BUNGENI WALA WASICHUKUE POSHO WALA MASHANGINGI AMA SIVYO NI UNAFIKI NA UZANDIKI TU.

    ReplyDelete
  33. Mimi sitochangia juu ya mambo ya Uhuru wa Tanganyika kwasababu una wenyewe na mimi i Wa-Zanzibar.

    Kama walivyotangulia kusema wengine, kuwa hata CUF nao walikuwa wakisusia Rais, Vikao vya Baraza la Wawakilishi, hilo halina mjdala. Sema kuna kitu kwenye CUF, wanasema lazima tuangalie wakati.

    Wakati CUF wanasusia vikao na kuto mtambua Rais, walikuwa na ushahidi wa wazi kabisa. Uchaguzi 1995, CUF ilishinda kwa kishindo kabisa, lakini baadaye Mwalimu Nyerere ndiye aliye saidia kubadilisha matokeo yale. Haya yanajulikana na hivi karibuni tu, mmoja wa makada wa CCM Zanzibar alikiri hili tena magazetini. Uchaguzi wa 2000 naona ulikuwa wa wizi wazi wazi, hata hivyo CUF walikuwa wakipata shindikizo la hapa na pale kutoka vyama vyote na si kweli kwamba vyama vyengine vilikuwa havilaani jamb hilo.

    Kuna makombano mengi yalifanyika kwa Zanzibar na Tanzania Bara na wengi walikuwa wakiwashauri CUF, wasisusiye vikao na kutomtambua Rais. Kwa njia moja ama nyengine CUF alikuwa inajaribu kuchukuwa maoni ya Wa-Tanzania na Wasomi wetu na walikuwa wakijaribu kutumia njia ya mazungumzo na CCM kama hivi wanavyotaka kufanya Chadema kukaa na CCM meza moja.


    Kwa hiyo haina maana kama CUF wamefanya na ikaonekana ilikuwa si vizuri, bsi wengine pia waige mabaya ya CUF. Haina maana CCM leo yupo madarakani na anaiba/kuchakuchuwa kura, kwa hiyo kesho ikija Chadema madarakani nao wafanye hivyo hivyo kisa CCM amefanya.

    Tujaribu kutofautisha mambo. Wakati CUF waliamua kutomtambua Salmin na Aman Karume kama Rais Halali, walikuwa wana kauli moja, wakati Chadema katika hatua za mwanzo mwanzo tu, tumeona baadhi ya Wabunge hawakutoka Bungeni, wengine wazito wawili, nao hawahudhuria/kuingia Bungeni, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zitto kabwe na Makamo mwenyekiti wa Chadema...
    Hatutaweza kuwaunga mkono Chadema kama wao wenye hawana msimamo makini kama vile CUF.

    sauti ya mwana CUF...

    ReplyDelete
  34. Tukio lina matokeo yake. Udini wa vyama kweli upo. Tusiwe wanafiki. Udini upo. Kama unapingina, kama ungeshiri misikitini Zanzibar walivykuwa wakinadiwa viongozi wa CUF na CCM Misikitini Zenj na baadhi yake hapa Bara hususan Dar. Ninachotaka kusisitiza ni kwamba msukumo wa kuichagua CCM/CUF ni zile ahadi zao za kuwapa Waislam kile walicho penda yaani Mahakama ya Kadhi. Ukweli ni kwamba huku Bara kikatiba hakuna sababu ya hizo mahakama ila kwa Zenj kama katiba ya Nchi hiyo haiwatendei haki kupitia mahakama zilizipo ni vema wakawapa hizo Mahakama za Kadhi kwa sababu karibu asili mia 99% ya Wazenj ni Waislam. Kwa hiyo ni haki yao. Ila Bara, lazima swala hili la mahakama ya kadhi liamuliwe kikatiba.

    ReplyDelete
  35. HUYU LIPUMBA NI PROFESA KWELI KILA KITU YEYE NI KUZUNGUMZIA CHADEMA HANA AGENDA NYINGINE KWELI AU HIYO SERIKALI YA MSETO NDIYO INAMPUMBAZA HUKO ZANZIBAR AU ANAHITAJI ATEULIWE NA JK UBUNGE MAANA HANA JIPYA.YEYE ALIKWENDA UWANJANI AMENUFAIKA NA NINI KUONA GWARIDE,MIKA 49 YA UHURU WAPO WATANZANIA WANAKULA MLO MMOJA LEO UNAONA KUONA GWARIDE NA KUPIGWA MIZINGA NDIYO DILL ACHA KUIFUAFUATA CHADEMA HICHO NDICHO CHA UPINZANI TANZANIA BARA WEWE UMEFUNGA NDOA NA CCM MNGEITA CHAMA CHENU CCM B.

    ReplyDelete
  36. Jamani mnashindwa kuelewa kitu kimoja cuf ni chama cha WAJANJA,kama mnakumbuka vizuri wakati wa mgogoro wa kisiasa znz kipindi hicho KOMANDOO SALIMIN ndiyo alikuwa Rais ,kila wakikaa kikao Seif moja ya mambo alikua akidai ni MAFAO YAKE ya uwaziri kiongozi!,(HUYO NDIYO MWANADEMOKRASIA) akaanza kulipwa mafao akanyamaza kimyaaa,karibu na uchaguzi kaanza kelele KAPEWA umakamu wa kwanza wa Rais,huyoo kaanza kuwanyooshea kidole chadema kuwa kususia hutuba ya Kikwete ni UHAINI ,huyo ndiyo SEIF SHARIF HAMAD,kasahau wamesusia vikao miaka KUMI,na kutomtambua rais wa znz kwa miaka kumi,dk za mwisho kuambiwa kuwa atakuwa makamu wa kwanza wa rais KAGEUKA oooo tunamtambua Rais Karume ,wacha afanyiwe fujo na wanachama wa cuf waliona ni MNAFKI MKUBWA HUYO JAMAAA, kwahiyo leo nikisikia POROJA za bwana Lipumba hanishangazi kabisaa ,hivi nyie mlitegemea Lipumba awe tofauti na Seif??,akifanya hivyo kesho hayupo kwenye uenyekiti,nimalizie kusema hivi ,waziri mkuu wa ISRAEL Benjamini Netanyahu ALIWAHI KUSEMA HIVI mwarabu mzuri ni yule aliyekufa,lakini akiwa hai usimwani hata siku moja chochote anaweza fanya,kwahiyo seif ni mwarabu usimwani hata siku MOJA,na sifa mojawapo ya mwarabu ni UNAFIKI,seif alishawahi kuwadanganya wanachama wake kuwa Dr Salimin hamalizi miaka mitano akiwa Rais wapi bwana KOMANDOOO kamaliza salama usalimi ni tena chupuchupu abadilishe katiba agombee kipndi kingine,bahati kule dodoma wakampinga ,yule angekuwapo ndiyo KIBOKO cha watu wanafiki kama seif na wenzie,naomba kama katiba inaruhusu KOMANDOO agombee tena na hamu sana kusikia katia ndani viongozi wengine wa cuf kama alivyofanya kwa kina juma duni na wenzie
    ooooo KOMANDOO MUNGU AKULINDE,AKUPE AFYA

    ReplyDelete
  37. ongeleeni vitu vinavyohusu maisha ya mtanzania na sio swala la udini. je ni chadema tu ndiyo hawakuwepo kwenye hiyo sherere? acheni unafiki. Taifa letu litakombolewa na mtanzania mwenyewe. jukumu letu vijana ni kulikomboa taifa letu kama wakati wa vita vya Uganda na Tanzania.

    ReplyDelete
  38. Toeni maoni yanayowajenga na wananchi, yanayojenga umoja wa kitaifa badala ya yale yanayobomoa na kuigawa nchi kwa mijiri ya udini. Hoja ni muhimu kuliko kulalamika na "adhominem" ni kukosa hoja. Kama Lipumba kaongea pumba si vyema kumhusisha yeye na chama chake na udini wala kukituhumu CCM kuwa chama cha kanisa kwa vile kuna balozi wa Vatican kwani kuwa na balozi hakumaanishi kuwa nchi hii ni ya kidini. Unapotoa maoni yako usiwe mbumbumbu wa historia, siasa, wala ukweli wowote wa jambo unaliongelea ama sivyo utaonekana kama mlevi wa kilabuni unayepwayuka bila kujua usemalo. Si vizuri kueneza kudini katika ukurasa huu wa maoni.

    ReplyDelete
  39. Baada y miaka 49 y uhuru wa Tanganyika, bado Tanzania bara kuna watu walio jaa kasumba za ubaguzi. Mmoja wapo ni huyu aliyetuma ujumbe "December 11, 2010 8:05 AM " Haya ndio matatizo ya Chadema, ubaguzi, udini na ujuwaji mwingi.

    Kwa taarifa yako, Maalim Seif Shariff Hamad, amekuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya Zanzibar. Na kwa taarifa yako, Maalim Seif kama angekuwa anaangalia nafsi yake, basi kwa vyeo alivyo shika, angekuwa na maisha mazuri. Kwa taarifa yako Maalim Seif, hana hata nyumba, ana gome tu (nyumba ambayo haijamaliza) kule kwao Pemba. Kwa taarifa, katika muaafaka wa mwanzo, ilikubalika, watu wote walio fukuzwa kazi kwa sababu za kisiasa wote walipwe fidia. Hata yeye amekuwa akizungushwa juu ya malipo yake. Ya Zanzibar huyajuwi tuwachiye wenyewe. Leo Zanzibar tunashukuru kutokana na juhudi za Maalim Seif na Dr Aman Karume. Tulizoweya kupigwa, kuteswa, kubakwa na askari na majeshi yanayo letwa kutoka bara, kila wakati wa uchaguzi. Mara hii tumpiga kura tukiwa salama. Hii ni hatua ya mwanzo, na Inshallah Mwenyezi Mungu atasaidia kuwa wamoja. Kasumba za Muaarabu tushazifukia, sisi Zanzibar ni Biriani, Mbara yupo, mwarabu/mwalabu, yupo, mhindi yupo, mchina yupo...

    ReplyDelete
  40. Kwa taarifa yako uliyoandika hapa juu hiyo pumba ya CUF, ujue nyinyi waislamu mnalenu mnalotafuta. Sisi wakristo tumeshajua ya kuwa nyinyi ni wachokozi, wabinafsi, waroho na wanafki. Kwanza kuingilia dini (imani) za watu wengine katika kujikampenia. Kwanini msichukue uislamu mkaji kampenia? Mfano huyu mbunge wa Sumbawanga hata kanisani hakujui lakini anachukua msalaba nikutudhalilisha kwa kweli. Sasa msubiri na wakatoliki waingie msikini wachukue mafyekeo (MAKWANJA)yenu tuone mtafanya nini? Mnachotaka kuanzisha ni kilichopo NIGERIA kwa sasa. Kama mnataka kuanza si muanze kama hakijawatokea puani. Ninajua mnapima au mnatikisa kibiriti kama kimejaa. OLE OLE OLE WENU!!!!!!!!

    ReplyDelete
  41. Njooo Zanzibar ufunze mambo ya dini na ustaarabu wa kuheshimu uhuru wa kuabudu na heshima kwa dini isiyo kuwa ya kwako.

    Zanzibar inajulikana asilimia zaidi ya 90% ni Wa-Islam, lakini tizama makanisa yalivyo huru kuabudu watakavyo. Tuna mabaliani, tuna masingasinga (Sikh) wote wapo huru kuabudu. Unaweza kushangaa mtaa mmoja watu wanavyo ishi kwa amani. Ukitaka haya njoo mji mkongwe Zanzibar uyaone haya yote. Utakuta makanisa ya madhehebu kubwa dunia, tena si ya kitoto na yamejengwa tokea karne ya 18 na kulikuwa na ufalme wa Kiarabu.

    Hata huko bara, kumekuwa na umoja baina ya Wa-Islamu na Wakiristo na dini nyengine zote. Haya ya udini tunaanza kuyaona leo yakiongozwa na Chadema. Sijuwi ulimsikia Hamad Rashid? Kwenye ile debate, alisema alifuatwa na kiongozi wa chadema na kumuambia wao wako tayari kuungana na CUF, sema wanahisi CUF, ni waislau waislamu! Naye Hamad akamuambia na nyinyi munaonekana kama catholic catholic ndipo Mwenyekiti wenu wa Chadema akaangua kicheko... Sasa na hii Pumba?

    Unaanza kuleta mambo ya kutikisa kibiriti. Hivi wewe wadhani leo kukianguka vita, atakaye umia ni Mu-isilamu tu? Fahamu kwa yale maeneo yenye wakiristo wengi basi waislamu watauwawa wengi na kwa yale maeneno ambayo yana waislamu tambua wakiristo ndio watakao kufa kwa wingi... Sasa niambiye hivyo vitisho unamtisha nani? Kwenye vita hakuna anayeweza kujigamba kwamba yeye atashinda, angeshinda mmarekani kule afghanstan, Iraq...

    ReplyDelete
  42. Mijadala yenu ya kitoto na kichochezi haina maana kwa mtanzania anayetafuta maendeleo. Udini wenu tokeni nao hatutaki muwapandikize watanzania kasumba za kidini. Kama CUF mnawatuhumiwa kuwa chama cha kidini wala hakitafika mbali kwa watanzania wapenda amani na kama CHADEMA wanatuhumiwa kuwa chama cha kidini nao mwisho wao hautakuwa mbali bali hali kadhalika CCM kama nayo ina kasumba ya udini mwisho wake hautakuwa mbali. Chama kinachotakiwa ni kile kinachowatazama wananchi kama watafuta maendeleo bila kujali dini, kabila, chama au ubara na uvisiwani. Acheni mijadala isiyo na maana.Sijui elimu yenu ninyi mnaowapandikiza wanatanzania fikra za udini. kama mnaelimu ya juu au ya sekondari basi au mliiba mitihani au mlipewa marks za bure. Mjadili mambo ya kujenga na kuwaunganisha watanzania na si kuwasambaratisha.

    ReplyDelete
  43. Enyi wachangiaji acheni jazba zisizo na msingi.Leteni fikra sawa.ndio maana hata Chadema wenyewe wameliona hili la kutomtambua rais ni upuuzi.Hivo wameamua kuachana na fikra mgando na kumkubali rais kisheria...fuatilia mahojiano ya Dk.Slaa na mtangazaji BBC jana jioni.
    tatizo la Prof.Lipumba liko wapi?Kumwambia ashiriki sherehe za uhuru???
    Mafanikio waliyoyapata CUF si kwamba wanalipwa fadhila na CCM la hasha ni mafanikio halali.Dunia inatambua hilo...labda wewe na na chuki zako binafsi.
    Demokrasia ina gharama zake ndugu zangu hasa pale wazandiki wanapong'ang'ania kuongoza wakati hawatakiwi.
    Leo hii CUF inaongoza serikali.

    ReplyDelete
  44. ni lazima wajipendekeze cuf imekosa mwelekeo ndiyo maana huku bara wamepata viti viwili tu kwa miaka kumi na tisa wanasuasua waache wajikombe 2015 bara hawatapata kiti hata kimoja

    ReplyDelete