LONDON, Uingereza
CARLOS Tevez ataachana na soka kama klabu ya Manchester City haitamruhusu kuhama mwezi ujao.Mshambuliaji huyo kutoka Argentina anataka kuondoka huku akisema kuwa, hakuna kiasi cha fedha ambacho kinaweza kuzuia abakie.Gazeti la
SunSport, awali lilikuwa la kwanza kuandika kuwa, Tevez alikuwa akitaka kuondoka Agosti, lakini aliombwa kubaki na kupewa ofa ya bonansi ya pauni milioni 1.5.
Lakini, Tevez mwenye miaka 26, alikataa, akisema kuwa, hana tamaa ya fedha, lakini anajali maisha yake binafsi.
Jana usiku, alitoa taarifa akisema mahusiano yake na baadhi ya watendaji na watu wengine katika klabu yamevunjika, na kuwa hayawezi kukarabatiwa.
Wiki hii, amewasiliana na mwanasheria wake bila ya kupitia mshauri wake, Kia Joorabchian kuomba kuhama.
Lakini, inadaiwa kuwa, alimwambia Joorabchian amechoshwa na maisha ya City na kwamba, anafikiria kustaafu soka.Tevez yuko mbali na watoto wake wawili, ambao wamekuwa wakiishi kwa upweke nchini kwao Argentina.Wakati kukiwa hakuna nafasi ya kuweza kuwaunganisha pamoja, anafikiria kuwa, akienda kwenye nchi inayotumia lugha ya kihispania, ataweza kuwa na watoto wake.
Anafikiria kutobaki England, na badala yake anaweza kwenda Hispania kucheza Ligi Kuu ya huko 'La Liga', kwa kujiunga na moja kati ya timu kubwa za nchi hiyo Barcelona ama Real Madrid kama ataondoka City.
City imechukizwa na kitendo cha Tevez kutaka kuondoka na inaamini kuwa, anataka kuondoka kutokana na fedha.Ni mchezaji anayelipwa zaidi ya wote katika klabu, akipata pauni 200,000 (sawa na takriban wa sh.460,000,000 kwa wiki na wakuu wa Eastlands wanaamini kuwa, mawakala wake wanapiga debe ili apate pauni 250,000 sawa na sh.575,000,000 kwa wiki.
Taarifa ya City imesema ombi la uhamisho kwa Tevez ni kinyuma na nafasi yake katika klabu.
No comments:
Post a Comment