14 December 2010

TANESCO Iringa kudhibiti wanaolihuhujumu

Na Eliasa Ally, Iringa

SHIRIKA la Umeme nchini(TANESCO) Mkoa wa Iringa limeanza kudhibiti uhujumu, ubadhilifu wa mali na wizi mbalimbali kwa baadhi ya wafanyakazi shirika hiloShirika hilo tayari limewafukuza wafanyakazi, na mwengine 10 wamefunguliwa
mashtaka.

Akizungumza jana na Majira ofisini kwa Meneja wa shirika hilo Mkoa wa Iringa, Bw. John Bandiye alisema kuwa uamuzi huo umefanyika baada ya wahusika kushikwa na vithibiti.

"Ili kuhakikisha tunafanya usafi ndani ya  shirika kupambana na wale ambao hawana nia njema na shirika hili, badala yake wanakuwa chanzo cha kulifilisi," alisema.Alisema kuwa wafanyakazi wa shirika hilo wa mkoani Iringa hawana budi ya kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa kuzingatia sheria za kazi na taratibu za TANESCO ili shirika hilo liweze kuleta faida zaidi kwa wananchi na siyo kuwahudumia wachache kwa manufaa
yao binafsi.

Bw. Bandiye ambaye hakutaka kuwataja waliofukuzwa na kufikishwa mahakamani kwa kuzingatia usalama, alisema kuwa kinachotakiwa kwa wafanyakazi wa Tanesco kwa kuwa wanaelewa sheria na taratibu zake, wazifuate kama zilivyo na shirika hilo litaweza kupata mafanikio yanayotarajiwa na wananchi walio wengi.

"Sitamwonea mfanyakazi yeyote lakini kwa yule anayekwenda kinyume na sheria na taratibu zetu sitalegeza kamba nitahakikisha shirika linakuwa na wafanyakazi safi,wanaotambua wajibu zao na ambao watafanya kazi kwa kuzingatia maamuzi ya ofisi na siyo kujiamulia wenyewe na kuwarubuni wateja wetu", alisema Bw. Bandiye.

Aidha aliyataja makosa ambayo yaliyosababisha kufukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani kuwa ni pamoja na kufanya kazi za shirika hilo kwa wateja bila kibali cha Tanesco na kulisababishia shirika hilo kupata hasara.

Alisema watu haoa walijenga  nguzo za laini ya umeme na kuwapelekea kuweka mita za umeme, kuwasaidia wateja kuiba umeme, kushikwa na mali za shirika hilo.Alisema shirika hilo limeanza kutoa bonasi ya  sh. 50,000 kwa watu watakaotoa taarifa za kulihujumu shirika hilo

No comments:

Post a Comment