14 December 2010

Siogopi kuchongewe kwa rais-DC

Na Yusuph Mussa, Korogwe

MKUU wa Wilaya ya Korogwe, Bw. Erasto Sima amesema pamoja na Rais Jakaya Kikwete kutembea na majina 'mkononi' ya Ma-DC wapya anaotarajia kuwatangaza wakati wowote, hataogopa kutimiza wajibu wake kwa
kuhofia kutemwa kwenye nafasi hiyo.

Akizungumza jana kwenye Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mombo, alisema mambo yanayofanyika kwenye jamii, na ambayo yanakwenda kinyume cha utaratibu lazima ayakemee bila kujali wananchi kumchongea kwa rais.

"Najua sasa hivi rais anatembea na majina mkononi ya Ma- DC atakaowateua, huku akiandika wapya watakaofaa, lakini sitaogopa kufanya kazi kwa kudhani wananchi wanampigia simu rais na kusema yule kijana hafai," alisema Bw. Sima.

Pia alisema 'stendi' ya sasa ya mabasi yaendayo Lushoto sio salama, hivyo kuagiza ihamishwe kwa kuwa inaweza kusababisha ajali."Kama kuna watu watakiuka maagizo yangu nitaleta askari pamoja na greda, tutavunja vibanda na kuwakusanya na kuwapeleka Kwamngumi, gereza maarufu kwa kilimo cha mpunga, lakini halina watu wa kufanya kazi hiyo," alisema Bw. Sima.

Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji wa Mombo, Bw. Richard Rwizile alisema kabla ya kuwahamisha waliojenga kinyume cha utaratibu, au kuhamisha vijana wa bodaboda tutawashirikisha ili kuzuia vurugu zisitokee.

1 comment:

  1. Wee mkuu wa wilaya vipi ushaanza kupaniki mapema ni kweli haufai huwezi kuwatishia wanachi hivyo kwa kuogopa kuchakachuliwa jina lako.Kwanza haufai hatukutakina ushike moja kutokuwepo au kuhamishiwa sehemu nyingine.

    ReplyDelete