14 December 2010

Mbaroni kwa kumpora askari bunduki

Na Salim Mhando

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limekamata watuhumiwa watatu wa ujambazi wanaodaiwa kupora silaha ya askari aliyekuwa lindoni katika tawi la Benki ya Akiba, Mwananyamala jijini Dar es Salaam.Watuhumiwa hao
walikamatwa maeneo ya pembezoni mwa jiji katika mikoa ya kipolisi Ilala, Kinondoni na Temeke  katika nyakati tofauti.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Bw. Suleiman Kova alisema askari namba G.128 PC Fikiri aliporwa bunduki aina ya SMG No. 00430 ikiwa na risasi 30 na msako ulianza mara tu baada ya tukio.

"Tumetumia saa 29 kufanikisha kupata silaha hiyo, Jeshi la Polisi kikosi cha kupambana na ujambazi wakishirikiana na askari wengine waliopo katika doria walifanikiwa kukamata silaha hiyo ikiwa na risasi 29," alisema Kamanda Kova.

Pia Kamanda Kova alisema kukamatwa kwa silaha hizo na watu hao kumetokana na taarifa za kiintelijensia, ufuatiliaji wa makini na hatimaye mapambano makali ya ana kwa ana kati ya polisi na watuhumiwa waliokuwa wakitumia gari lenye namba za usajili T 200 BLV Toyota Mark II Brand.

Bw. Kova alisema kuwa majina ya watuhumiwa hao yamehifadhiwa kutokana na sababu za kiupelelezi huku polisi wakiendelea kuwasaka majambazi wengine juu ya tukio hilo.

2 comments:

  1. kovaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa kidedea

    ReplyDelete
  2. nimeshuhudia gari hilo lililoyumiwa likiporwa na wao kuliacha gari walilokuja nalo la aina hiyo ila ni la blue ambalo liliporwa sinza namba T450 BJH. hawafai

    ReplyDelete