Na Mwajuma Juma, Zanzibar
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amesema kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa haijafuta jina la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, bali imebadilisha mfumo wa muundo wa serikali.Balozi Seif alitoa tamko hilo
jana, Mgambo alipokuwa akiwahutubia wana Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa wadi hiyo katika Jimbo la Kitope Wilaya ya Kaskazini B. Unguja.
Serikali ya Zanzibar ipo kutoka ilipoundwa baada ya Mapinduzi matukufu ya Januari 12 mwaka 1964 na itaendelea kudumu, alisema.
Balozi alisema kuwa na wale wanaosema imefutwa sio kweli na ni upotoshwaji mkubwa wenye malengo yaliyokusudiwa.Hivyo aliwataka wanachama hao kuiunga mkono serikali hiyo ili kutimiza ahadi na kutekeleza ilani kwa ufanisi mkubwa.
Balozi Seif alisema kuwa itafanyakazi kwa maslahi ya nchi na wananchi wote na sio kwa maslahi yake binafsi.Mimi nipo kwa ajili ya nchi na nitawatumikia wote, sitofanyakazi kwa ajili ya maslahi yangu binafsi, alisema Balozi Seif.
Kabla ya kuhutubia mkutano huo, Balozi Seif alikuwa na mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea ya Kusini nchini Tanzania Bw. Young Hoon Kim aliyefika ofisini kwake kujitambilisha.
No comments:
Post a Comment