Na Mohamed Hamad Babati, Manyara
JESHI la Polisi Mkoa wa Manyara limewaua kwa kuwapiga risasi watu wawili kwa tuhuma za ujambazi wakati walipojaribu kuwatoroka polisi baada ya kukamwatwa.Kamanda wa Polisi mkoani Manyara, Bi. Parmena Sumari alisema majambazi hao
walikamatwa wakiwa ndani ya basi wakitokea Singida kwenda Hydomu wilayani Hanang
Alisema baada ya kupekuliwa walikutwa wakiwa na bastola mbili aina ya Cloka na Rivova zikiwa na risasi 16.Aliwataja watu hao kuwa, Yusuph Mohamed (47) maarufu kwa jina la JJ mkazi wa Singida na Elia Philipo (35) mkazi wa Galapo Babati.
“Baada ya kuyakamata watu hao waliwekwa ndani ya gari ili kwenda kituoni, njiani waliomba kujisaidia hapo walitimua mbio ndipo polisi wakawarushia risasi na kuyajeruhi lakini baada ya muda walifariki dunia,” alisema Bi. Sumari.
Bi. Sumari alisema kuwa watu hao wanadaiwa kuwa ni majambazi ambayo hufanya uhalifu sehemu mbalimbali ikiwemo Mikoa ya Singida, Manyara, Arusha, Tanga na Kilimanjaro.Alisema silaha zilikamatwa si halali na kwamba baada ya mahojiano na majambazi hayo walisema moja walipora mzungu mjini Arusha na nyingine walinunua Kigoma.
Bi. Sumari alisema awali Yusuph Mohamed aliwahi kufungwa miaka 24 gerezani kwa kosa la kuiba kwa kutumia silaha lakini alitoroka hadi alipokamatwa na kuuawa.
“Kwa kweli kama ilivyokuwa tabia yake huyu bwana hata hivyo alijaribu kukimbia na ndipo polisi nao wakamuwahi na kujeruhi kwa risasi na kumkamata ambapo baadaye alifariki dunia akipelekwa hospitalini,” alisema Bi. Sumari.
No comments:
Post a Comment