29 December 2010

Kazi ni kufukua 'panya' watafuna mapato-Malla

Na Peter Saramba, Arusha

KAZI kubwa ya madiwani wa Manispaa ya Arusha  kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo ni ukusanyaji na kudhibiti watu wanaotafuna mapato ya halmashauri na
kukwamisha ya maendeleo ya wananchi.

Akizungumza Majira Arusha juzi, Diwani wa Kata ya Kimandolu, Bw. Estomih Malla alisema yeye pamoja na wenzake watahakikisha fedha zote zinazokusanywa kutoka vyanzo vyote vya mapato ya halmashauri zinatumika kwa miradi iliyokusudiwa na lazima thamani ya mradi huusika ilingane na kiasi kilichotumika.

“Sisi tunaingia pale halmashauri tukiwa na tabia kama ya paka. Tunakwenda kukamata panya walioko pale wanaotafuna fedha ambazo zingeenda kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi. Kwa kipindi cha miaka mitano ya uhai wa baraza hili tunataka wananchi waone umuhimu wa kuwepo madiwani wengi kutoka vyama vya upinzani,” alisema Bw. Malla.

Alisema kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato na kudhibiti ubadhirifu, fedha za miradi ya maendeleo itapatikana na hivyo huduma za kijamii zitaboreka tofauti na hali ilivyo sasa ambapo licha ya mapato kutokusanywa ipasavyo, hata kiasi kidogo kinachokusanywa kinafujwa na watendaji wasio waaminifu kwa matumizi yasiyolenga maendeleo ya wananchi.

Bw. Malla  aliyekuwa mgombea wa nafasi ya umeya katika uchaguzi uliogubikwa na utata kamwe hawatatumika kama muhuri kupitisha mambo yasiyozingatia maslahi ya wananchi, badala yake watasimama imara kupinga na kudhibiti mambo yote yanayolenga maslahi binafsi au kundi fulani ya watu.

Kambi mbili za madiwani wa Manispaa ya Arusha wamejitangazia mameya, mmoja kutoka CHADEMA ambaye ni Bw. Malla na mwingine ambaye ndiye anatambuliwa na uongozi wa Manispaa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Gaudance Lyimo, diwani wa Kata Olorien.

Bw. Malla alitaja kazi nyingine ya kudumu ya madiwani wa CHADEMA kuwa ni kusimamia ugawaji mzuri wa viwanja na kuchunguza viwanja vyote vya wazi vilivyoporwa au kuuzwa kwa matajiri ili kuhakikisha vinarejeshwa kwenye umiliki wa umma.

Kwa muda mrefu, baraza la madiwani wa Manispaa ya Arusha kwa vipindi tofauti limekuwa likituhumiwa kujihusisha na ugawaji na uuzaji holela wa viwanja vya wazi ambapo baadhi ya madiwani akiwemo meya waliwahi kuvuliwa madaraka yao baada ya kuhutuhumiwa kuhusika kwenye uuzaji wa viwanja vya wazi eneo la Kilombero na Makao Mapya.

3 comments:

  1. SAWA MUSTAHIKI MEYA MALLA. KAZI KUBWA ARUSHA ILIYOSHINDIKANA MIAKA 49 YA UHURU WA TANZANIA HAPO ARUSHA NI:
    1.KUDHIBITI MAPATO HASA YATOKANAYO NA PARKING.
    2.KUDHIBITI UTOAJI TENDA MBALIMBALI, PAMOJA NA KUFANYA THOROUGH REVIEW NAMNA TENDA HIVYO ZILIVYOTOLEWA NA KUTOA TAARIFA KWA UMMA.
    3.KUTENGENEZA/KUSIMAMIA BARABARA NZURI ZA MIFANO HASA TOKA NJIRO KUINGIA MJINI, TOKA SOMBETINI KUINGIA MJINI NA TOKA KIJENGE JUU NA CHINI KUINGIA MJINI.PIA KUTENGENEZA MITAA YOTE YA ARUSHA IWE NA MAJINA NA KUWEKA TAA ZA KUTUMIA SOLAR MJI MZIMA.UHURU ROAD IONEKANE KAMA JINA LILIVYO MAAN KWA SASA MVUA ZOTE NA MITARO YOTE INAISHIA HAPO.
    4.KUTENGENEZA MASOKO YA UHAKIKA
    5.KUTUNZA MAZINGIRA KOTE, MSIJE MKAWA KAMA BATILDA WAZIRI WA MAZINGIRA LAKINI AKAIACHA ARUSHA MBOVU KABISA.
    5.KUDUMISHA USAFI NA USALAMA KATIKATI YA MJI NA MAKAZI YA WATU.
    6. KURUDISHA MAENEO YOTE YA WAZI YALIYOJENGWA KINYUME NA TARATIBU AU KUUZWA NA VIONGOZO WA CCM NA SERIKALI.
    7.KUFANYA UCHUNGUZI WA NAMNA UGAWAJI WA VIWANJA BURKA ULIVYOFANYIKA NA KUWANYIMA HAKI WATU WA ARUSHA, HUSUSAN WALIVYOPEWA LOWASSA FAMILY(3),MINISTER NYALANDU FAMILY(2),RIDHIWANI KIKWETE, MINISTER...,NK NA MADAI YA KIKWETE RAIS KUPEWA VIWANJA 50 NA KWAMBA WALIFUATA UTARATIBU GANI? PIA FOMU ZILIGAWA NGAPI NA PESA ZILIENDA WAPI ZINGINE? NANI WALIGAWA? HUYO MTUMISHI WA MANISPAA ALIYEJIPA VIWANJA VIWILI NA KUVIJENGA NYUMBA 2 ZA MIL 400 ACHUNGUZWE PIA.
    8. KUPIMA VIWANJA VIPYA, VIWEKEWE MIUNDO MBINU HASA MAJI, BARABARA ZA UHAKIKA NA UMEME HALAFU VIUZWE KWA BEI YA BIASHARA ILI KUONGEZA MAPATO HALMASHAURI.
    9.KUFANYA KILA LINALOWEZEKANA KUONDOA WATOTO OMBAOMBA MITAANI ARUSHA. HAWA NI TIME BOMB NA NI KERO KUBWA MJINI.
    10.KUPANUA JIJI LA ARUSHA LIFANANE NA HADHI YAKE, HASA MAENEO YA FAYA, MIANZINI, KIMANDOLU,MJINI KATI,KIJENGE,SOMBETINI NK
    11. MUWAELIMISHE WANAARUSHA HASA WANA CCM WANAOTUMIWA VIBAYA NA KUWATIA HASARA NA FAMILIA ZAO KWA MANUFAA YA VIONGOZI WAO KWA KUTUMIA SHAHIDI MBALIMBALI ZILIZOZAGAA KILA KONA. MUWAAMSHE WATU WAJUE MATENDO MABAYA WALIYOTENDEWA NA NYIE MUONYESHE NJIA MYA YA KUKUMBUKWA HATA BAADA YA MIAKA MITANO HATA KAMA CHADEMA HAMTACHAGULIWA TENA. MUENDE KWA WANANCHI CHINI KABISA MUWAONYESHE TOFAUTI NA HASARA YA UTAWALA DHALIMU NA UTAWALA MPYA WA HAKI. HUO NDIO MCHANGO WANGU KWA SASA.

    ReplyDelete
  2. naungana kwa 100% na mto maoni wa kwanza. Mimi ni mkazi wa NJIRO Arusha block B
    1.Hapa Njiro block B kuingilia TEMDO, kuna watu walijenga chini ya nyaya za umeme mkubwa, mmojawao akiwa jaji mkuu mteuliwa Hon Othman Chande. Kwa busara yake, bila kujali influence yake, hakuendelea kuimalizia hiyo nyumba. angekuwa kiongozi mwingine, angetumia nguvu. Huyu baba amenipa somo la uadilifu kwa hiyo anastahili nafasi aliyopewa.ANAHESHIMU taratibu na anaheshimu watu.
    2.Lakini katika mazingira yanayoonekana dhahiri ni ya rushwa kuu Halmashauri/Ardhi, kuna mtu kazungushia uzio eneo lililokwishafidiwa na serikali kwa kuwa liko ndani ya umeme mkubwa akitaka kujenga.liko MBELE ya nyamba ya bwana aitwae KANISA, unapopita nyumba ya Chief Justice. Watu wa hivi sio wa kufumbia macho hata kidogo.
    3.Twengenezeni barabara hizi za ndani Njiro ijulikane ni makao ya watu mapya na watu wapate moyo wa kuchangia maendeleo yao.
    4. CHADEMA NA TLP onyesheni tofauti na wengine na watu waione, MTADUMU.

    ReplyDelete
  3. TENA BASI CHADEMA NA TLP MSIPOONYESHA UTOFAUTI WENU NA WADHALIMU WA CCM, ARUSHA MUNICIPAL HAMTAIPATA TENA. WAPENI ELIMU WATU WAJUE. MKIKOSEA THIS TIME AROUND, MSAHAU MBELE KWENU. WALIPISHNI WATU KODI INAYOWASTAHILI.

    ReplyDelete