27 December 2010

'Mwenye Dowans atajwe kabla ya kulipwa'

Na Waandishi Wetu

SAKATA la malipo ya sh. bilioni 185 kwa Kampuni ya DOWANS iliyorithi mikoba ya kampuni hewa ya Richmond imezidi kuchafua hali ya hewa baada ya wananchi kumtaka Rais Jakaya Kikwete kumtaja hadharani mmiliki wa kampuni hiyo
kabla ya kulipwa mabilioni ya fedha za walipa kodi.

Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti kutoka mikoa mbalimbali, wananchi hao wamesema wanasikitishwa na kauli ya serikali kukubali kuheshimu sheria kulipa Dowans fedha hizo wakati mmiliki wake hajulikani hadi sasa.

Tunataka serikali, hasa Rais Kikwete, atuonyeshe mmiliki wa Dowans, ajitokeze hadharani mbele ya vyombo vya habari tumfahamu. Haiwezekani nchi ikashindwa kesi na hewa, maana hadi leo hatujui mmiliki wa Dowans ni nani.

"Pia tunataka hiyo hukumu ipelekwe kwa Jaji Mkuu ili baadaye ilitolewe hadharani kwa vyombo vya habari tujue inasemaje,” alisema Bi. Catherine Maliwa wa Kigogo Dar es Salaam.

Alisema katika historia ya Taifa la Tanzania haijawai kutokea nchi ikashindwa kesi na mtu asiyejulikana na kuonya viongozi wa Serikali wanaohusika kutothubutu kutoa hata senti kulipa Dowans bila wamikiki wake kujulikana na kujitokeza hadharani.

“Jambo linalotusikitisha ni kuwa Richmond ni Kampuni feki na wamiliki wake hawajulikani, iweje Kampuni feki ambaye mmiliki wake hajulikani kuuzwa kwa Dowans, mtalipa pesa mashetani?” alihoji Bi. Maliwa.

Alisema hivi sasa Watanzania wamechoshwa na viongozi wazembe wanaowabebesha mzigo wajane na maskini huku wahusika wakibaki salama na kufurahia maisha ya anasa kwa jasho lao.

Alisema baada ya hatua ya Rais Kikwete kumtangaza mmiliki wa Dowans na mwenye kampuni hiyo kujitokeza hadharani na nakala ya hukumu kukwekwa hadharani kwenye vyombo vya habari wahusika wote wachukuliwe hatua za kisheria suala la kulipa fedha hizo liwe la mwisho.

Mkoani Shinyanya wananchi walisema licha ya Mahakama ya Kimataifa ya kusuluhisha migogoro ya kibiashara (ICC) kuipa ushindi Dowand, utekelezaji hauwezekani hadi mmiliki wake ajulikane kwa Watanzania wote.

Walisema ni ajabu na mshangao kwa shirika la serikali kupelekwa mahakamani na mtu asiyejulikana huku baadhi ya viongozi waandamamizi wakionesha kwa haraka dalili ya kutaka kulipa adhabu hiyo kwa mtu asiyefahamika.

“Umefika wakati kwa Rais Kikwete abebe jukumu la kuwafahamisha rasmi Watanzania mmiliki halisi wa Dowans, itakuwa ni miujiza na aibu kwake kulipa fedha hizo kwa mtu asiyejulikana. Watanzania hatujawa wajinga kiasi hicho, kila mara serikali imekuwa ikieleza wazi kutomfahamu mmiliki wa Dowans,” alisema Bw. Fredy Mmassy.

Wananchi hao walihoji kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa serikali inaheshimu sheria na kwamba ikibidi haina ujanja zaidi ya kulipa mabilioni hayo kwa Dowans.

Rais atueleze na amtaje huyo mtu, vinginevyo Watanzania hatutokubali fedha hiyo ilipwe, na hata ikilipwa kwa nguvu waelewe iko siku tutaidai kwao, alisisitiza Bw. Mmassy.

Wananchi hao walisema mbali na Rais Kikwete kumtaja mmiliki wa kampuni hiyo pia awaeleze Watanzania mwakilishi wa serikali aliyeiwakilisha TANESCO katika mahakama ya ICC.

Walisema imefika wakati wa serikali kuweka wazi mkataba kati yake na kampuni hewa ya Richmond pamoja na ule wa Dowans ili kila kitu kifahamike na Watanzania wajionee wenyewe ni wapi TANESCO inapotiwa hatiani kabla ya fedha hizo kulipwa.

Katika hatua nyingine wananchi hao walimtaka Rais Kikwete kuangalia upya maamuzi ya TANESCO kupandisha bei ya umeme na kuweka wazi kuwa hali hiyo haiendani na maisha yao duni na umasikini uliokithiri.


Tunaomba Rais Kikwete kama kweli anawathamini Watanzania waliomchagua kwa moyo mmoja basi, azuie ongezeko la bei mpya za umeme, viongozi wetu wameonesha wazi kutokuwa na huruma na watu wao, wanakubali kulipa sh. bilioni 185 na kuongeza bei ya umeme,” alisema Bw. Masunga Jilaba, mkazi wa kitongoji cha Ndembezi mjini Shinyanga.

Hawa wana haki ya kufanya hivyo kwa sababu hawatoi hata chapa moja mifukoni mwao kwa ajili ya kulipia umeme, uchungu wataupata wapi? Ni Watanzania masikini wanaohangaikia hata mlo wao wa siku ndiyo watapaswa kulipa deni hilo la Dowans kupitia ankara za kila mwezi za matumizi ya umeme,” alisema Bw. Jilaba.

Wananchi hao walisema ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 18.5 ni dalili ya wazi kuwa wateja wa TANESCO ndiyo wanaopaswa kuilipa Dowand na kwamba hilo halihitaji mtu kuwa na elimu ya chuo kikuu kufahamu kuwa kampuni hiyo ni ya mfukoni na kuna watu wanafaidika nayo kwa njia moja au nyingine.

Katika hatua nyingine wanachi hao wamehoji kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Bw. Edward Lowassa, kwamba wananchi watangulize upendo kudai katiba mpya na kumtaka atafute kwanza upendo na huruma kwa Watanzania.

“Najiuliza ni upendo gani anaounzungumzia, yeye anajua upendo tumeumizwa na mengi ikiwemo mikataba mibovu, kama angejua upendo nchi isingeingia katika mkataba wa aibu wa Richmond wakati akiwa madarakani,” alisema Bi. Maliwa.

Alisema Bw. Lowassa anapaswa kuwaomba radhi Watanzania kwanza ili kuonesha upendo badala ya kujifunika shuka nyeupe wakati ndani kuchafu.

Wakati huo huo serikali imeshauriwa kuangalia uwezekano wa kusitisha mikataba yote na makampuni ya uzalishaji umeme ikiwemo IPTL na Songas ili fedha zinazotumika kulipa capacity charge zitumike kununulia mitambo itakayomilikiwa na serikali.

Umefika wakati wa serikali kukatisha mikataba mibovu inayowakamua Watanzania katika uzalishaji umeme hata kama ni kulipa fidia basi fidia ilipwe ili fedha zinazolipwa kila siku kwa makampuni hayo zielekezwe katika kununua mitambo yetu sisi wenyewe,

Kwa hii Watanzania tutakuwa radhi hata kama nchi itaingia gizani kwa miezi miwili mfululizo ni bora iwe hivyo, na katika kipindi hicho umeme kidogo unaozalishwa na TANESCO yenyewe uelekezwe katika maeneo nyeti tu ya uzalishaji, ili mradi tu baada ya muda mfupi tuwe na mitambo yetu wenyewe,” alisema Bw. Juma Shukuru.

Imeandaliwa na John Daniel Dar na Suleiman Abeid, Shinyanga

29 comments:

  1. unajua dhambi inayomtesa kikwete - hadi sasa anaamini kuwa urais wake amepewa na mafisadi na mtandao wake and haujui kuwa alipewa madaraka haya na wanananchi wote -japo kwa uchaguzi wa mwaka 2010 (ameingia kwa wizi), namshauri athibitishe kwa sasa kuwa ni rais wa wananachi na si rais wa kulinda maslahi ya Lowasa, Karamagi na Rostam, naamini historia haitamlinda kama anavyowalinda akina Mkapa siku nguvu ya umma itakavyoamua kuchukua hatua

    ReplyDelete
  2. Tatizo kubwa tulilonalo Watz ni mkuu wa nchi ndio cheche. watu wanafikiri urais ni pambo la kutaka kujaribu usilojua na kupata sifa kwamba nami nishakuwa rais, kumbe cheo hicho ndio muelekeo sahihi au mbaya wa nchi. nchi yetu inaenda mrama kwa kuwa rais hana vision ya kilichompeleka ikulu. iko hivi, kikwete ajiandae kupanda kortini siku nchi hii ikichukuliwa na wapinzani. anatetea maovu kwa hiyo yeye ndie atakaewajibishwa.

    ReplyDelete
  3. +Watanzania sisi ni wazuri sana wa kusifia na kusahau.Kwenye kampeni tulimwimbia sana na tukasahau maovu yote aliyoyafanya.Cha muhimu ngoja tuendelee kuumia maaana zawadi zetu walishatupatia wakati wa kampeni,kanga kofia na soda.Na hali hii iendelee kuwa ngumu mpaka 2015 ili tupate akili.

    ReplyDelete
  4. Viongozi wa Tanzania wanajua wananchi watanzania ni wajinga kufikiri kumbe ni jinsi walivyolelewa na wasisi wetu kuwa watu wa amani lakini ninaona huko tuendako uvumilivu utawashinda watanzania. Haiwezekani uwatweke maskini mzigo wa kuwaongezea gharama ya umeme huku baadhi ya viongozi wetu wakiwa wameingia dili na Downs ili wapate mabilioni ya shillings kwa kigezo cha kuvunja mkataba. Jamani hata wawekezaji wanapokuja si lazima wajua kwamba nchi ina taratibu na sheria zake? Wabunge walikataa kununua mitambo ya Dowsons kwa sababu ya sheria ya manunuzi. Lakini baya zaidi ni kampuni kurithi mkataba wa Richmond. Jamani hata kama mtu hujaenda chuo kikuu huwezi kugundua kwamba hiyo ni dili nyingine iliyofanywa na baadhi ya watu wa Serikali yetu. Nchi yetu imekosa wazalendo kabisa. Mimi ninaunga mkono kabisa kwamba watanzania wanataka kumfahamu anayeimiliki hii Dowans. Pia tujue wale waliosaini huo mkataba. Je ni wao wenyewe waliokwenda kwenye hiyo kesi kwa niaba ya serikali au wengine? Mawakili walioitetea Tanesco tuwajue ili tuamini kama hawakupewa rushwa ili waisaliti nchi yetu.

    Niseme tu kwamba hata kama watafanya njama walipwe hizo fedha. Ninajua ipo siku watanzania wataidai hiyo fedha kwa nguvu ya umma. Ipo tu siku. Nchi hii imebadilika sana wala Kikwete asifikiri kwamba ni nchi ya zama zilizopita. Ni nchi ya kizazi kimya watu wengi ni vijana waliosoma. Hawawezi kudanganywa tena. Na wanajua nchi hii ni yao pia. Sio ya wateule wachache. Tunajua kwenye dili hii inawezekana na Kikwete yumo. Ipo siku hata kama atakuwa amekufa familia yake watanzania watakuja kunyang'ganywa mali zote walizoiba.

    Ni ukatili mbaya kabisa kuamua kuwatwika mzigo wajane, yatima, na maskini kulipa Dowans kupitia katika ongezeko la bill za umeme.

    ReplyDelete
  5. Dowans, Richmond, IPTL, nk yooooote hayo ni miradi ya wakubwa. Sasa kwani hamuwajui? "list of Shame" na wapambe wao kwani hawajulikani? Mnataka wafanyeje? kwani waliwahi kukana popote? Wao ndio wanaoidai TANESCO, ndio waliokuwepo kwenye hiyo kesi kama walalamikaji na wawakilishi wa walalamikiwa(watanzania). Hapo unategemea nini! wao pia ndio wenye mamlaka ya kuidhinisha malipo! Ndio wenye majeshi yote, mtaandamana wapi? Ndio waliowaweka woote wanaotakiwa kufanikisha kila kitu, kila hatua. Tutapona wapi? Dawa ni kutokwenda kwenye ofisi zao kudai haki, maana hawataitoa. Tunachotakiwa kufanya ni kuwaomba ndugu zetu polisi na usalama wa taifa, JWTZ na watumishi wa serikali kwa ujumla watulinde badala ya kutupiga mabomu, TUTAKAPOGOMA NA KUANDAMANA KUDAI HAKI ZETU. TUMENYONYA KIASI CHA KUTOSHA, TUMEPUUZWA KIASI CHA KUTOSHA, NA TUMEDHARAULIWA KIASI CHA KUTOSHA. UNYONGE WETU NDIO ULIOTUFANYA TUFIKIE HALI HII. TUMEWAACHIA WANYONYAJI NCHI YETU NA SHERIA ZETU ZIMETOA MWANYA WA WAO KUINGIA MADARAKANI ILI WATUKANDAMIZE, WATUNYONYE KISHA WATUDHARAU. MIKATABA YAO YOTE TUIKATAE. HAIWEZEKANI MAMILIONI YA WATANZANIA YAENDELEE KUWALIPA WATU WACHACHE KILA MWAKA KWA VISINGIZIO KUWA WANATOA HUDUMA ILI HALI WAENDELEE KUTAWALA KWA NGUVU.

    ReplyDelete
  6. SASA KAMA JAJI MKUU MPYA NI OTHMAN CHANDE ALIYETUMWA ARUSHA MIAKA ILE KUMWACHIA HURU JAMBAZI SUGU JUSTIN NYARI WATANZANIA MNATEGEMEA NINI?KIKWETE KATUMALIZA. HAWA NI WASKAJI ZAKE NA KWA HIYO MAHAKAMA CHINI YA CHANDE ITALENGA KUCHAKACHUA KILA HUKUMU KULINGANA NA MATAKWA YA KIKWETE NA MAFISADI WENZIWE. WATANZANIA R.I.P TUJUE HILO.

    ReplyDelete
  7. Dowans ni kampuni ya kitapeli kama Richmond. wenyewe wako hapahapa Bongo na wanajulikana. Ndiyo maana Mh. samwel sita alisema kulipa hizo pesa ni kuhujumu uchumi. kwasabu anauelewa fulani kuhusu hao jamaa.hizo pesa zinaenda mikononi mwa hao jamaa. watz. INAUMA SANA.

    ReplyDelete
  8. tena nawasihi mjue list ya mafisadi imekamilika kwa uteuzi wa Chande kama jaji mkuu.ngoja muone kesi za chadema zilizofunguliwa zitakavyobadilishwa. ngoja Hosea aondolewe TAKUKURU,maana alikuwa anafanya kazi kwa mashinikizo ya rais lakini pia hakutaka kuachia ngazi. Hosea amekuwa si popo wala ndege.huyo ndio Kikwete AMABAYE NYERERE ALIMKATAA.

    ReplyDelete
  9. INATAKIWA JWTZ LICHUKUE MADARAKA YA NCHI YETU KWA MUDA CHINI YA VIJANA WAZALENDO (SIO LT.GEN.SHIMBO ALIYEPEWA TENDA YA KUNUNUA MATREKTA NA KIKWETE)NA KUVUNA SIFA YA FISADI. HATUNA RAIS WALA UONGOZI TANZANIA. KIONGOZI MKUU ANAPOKUWA ANATETEA WEZI NI WAZI KWAMBA NI MWIZI PIA. HEBU KAMA KWELI JWTZ KUNA WAZALENDO, WAJITOE. TUMECHOKAAAAA!

    ReplyDelete
  10. KIUKWELI, KAMA KUNA NCHI AMBAYO VIONGOZI WAMEDHAMIRIA KULETA MACHAFUKO KWA BIDII ZOTE NI TANZANIA. WAMEENDELEA KUTUCHOKOZA TARATIBU MPAKA SASA WANAKUJA NA ARI MPYA, KASI MPYA, NA NGUVU MPYA YA UNYANG'ANYI WA HAKI ZETU. WAMETUBANA HATUNA HATA PA KUKIMBILIA. KODI IKO JUU KULIKO NCHI ZOTE AFRIKA MASHARIKI. UMEME, MAJI, MATIBABU, ELIMU, AJIRA, NI SHIDA TUPU. WAMETUFIKISHA MAHALI AMBAPO HAKUNA MTANZANIA ATAKAEWEZA KUISHI KWA RAHA AKIWA MUAMINIFU. HIVI KWELI TANZANIA HAPA TULIPO NDIPO TULIPOKUSUDIA KUFIKISHWA? MBONA NCHI ZA WENZETU ZINAENDELEA TU KWA AIDHA UTALII PEKEE, AU MADINI PEKEE AU HATA BANDARI TU. SISI TUNAVYO VYOTE HIVYO LAKINI BADO TUNAKAMULIWA KANA KWAMBA WOTE NI WATUMWA! AAAH, JAMANI VIONGOZI WETU, HEBU MUWE NA UTU NA HURUMA. HATUTAFIKA, MNAKOTUPELEKA SIKO! TUBADILISHE MUELEKEO.

    ReplyDelete
  11. Ndugu Wananchi, ifike mahali tuseme BASI! Nina hakika tulisema BASI kwa kupitia sanduku la kura. Lakini kilichofanywa na Usalama wa Taifa na Tume ya Uchaguzi ndiyo hicho mlichokiona - Rais kuingizwa madarakani kiwizi.

    Sasa tumejua ni kwanini Tume iliendelea na mchakato wa kutangaza kura hata pale Dr. Slaa alipotoa ushahidi wa idadi tofauti za kura zilizokuwa zinatangazwa - ni kulinda maslahi ya MAJAMBAZI na WEZI wa fedha za waTZ maskini.

    Sasa wakati umefika wa kufanya KWELI - kuingia barabarani kudai haki yetu bila kujali bunduki, maji ya kuwasha, virungu, n.k.

    HAKI mbele; woga wetu ndiyo KIFO chetu na cha vizazi vyetu. Kilio cha watu ni kilio cha MUNGU.

    ReplyDelete
  12. pETRO eUSEBIUS mSELEWADecember 27, 2010 at 3:33 PM

    Mi nilishasema CCM ni wasanii watupu...si mnaona? Mimi ni mwanasheria.Haiwezekani kuwepo na kesi ambayo ina upande mmoja tu ujulikanao.Hata kama ni kesi iliyohusisha makampuni ya Dowans na TANESCO,bado wamiliki wao lazima walijulikana kwa Mahakama na pande zote za kesi.CCM,twawaomba sana msisababishe makubwa jamani.Sisi Watanzania hatutakubali kumlipa asiyekuwepo...hata siku moja.Hii ni sawa kuchukua mabilioni hayo BoT na kwenda kuyachoma moto.We are not stupid...we are not! Ikitokea hali inachakaa hapa kwa mambo kama haya,hatutamlaumu mtu ila CCM na Serikali yao.Subirini muone mengine ya CCM...YA HATARI ZAIDI!

    ReplyDelete
  13. Ingawa mimi si rais, nawatajieni wenye kampuni la Dowans.
    1 Jakaya Kikwete
    2 Edward Lowassa
    3 Rostam Aziz
    4 Nimrod Mkono
    5 Andrew Chenge
    6 Nazir Karamagi
    Waliobaki malizieni wenyewe. Je mna swali jingine au wasi wasi juu ya kuwatajia wezi wenu wakuu wanaoitwa waheshimiwa?
    Kazi kwenu mchawi eshafichuliwa.

    ReplyDelete
  14. UJINGA UMEFUNGWA NDANI YA MTANZANIA FIMBO YA ADHABU ITAUONDOA UJINGA WA MTANZANIA.HAKUNA NJIA MBADALA ILA FIMBO YA ADHABU....MATESO MAKALI NDIO FIMBO ITAKAYOMPA MTANZANIA AKILI

    ReplyDelete
  15. ITAKUWAJE UWAJUE HAO SITA NA HAO WENGINE MSIWATAJE? NYINYI MNAMUANDAMA KIKWETE KWA KUWA MUISLAMU, PILI KWA KUWA AMEIMARISHA NCHI NA UHURU HUO WA KUSEMA HAPA MMEUPATA KWAKE WAKATI WA BABA YANE MTAKATIFU NA MKAPA MLIKUWA MIKIA MUMEIKUNJA BAINA YA MAKALIAO YENU KWA WOGA, KWA HAYA MLIONDIKA HUMU NDANI HATA MSINGALIAMKIA JUU YA VITANDA VYENU! MSITUDANGANYE AGENDA YENU INAJULIKANA CARDINAL PENGO ALITANGAZA WAZI KUWA 2010 NA 2015 LAZIMA RAIS AWE MKRISTO, NYINYI MNATAKA KUJENGA UHASAMA BAINA YA DINI WATU AMBAO TUMEISHI PAMOJA KWA MIAKA NA SOTE TUMESHIRIKI KUIGOMBOA NCHI HII KUTOKA KWA WAKOLONI WA KIINGEREZA NA KIJERUMANI! ACHENI AMALIZE MUHULA WAKE NA NYINYI MUWEKE HUYO MGOMBEA WENU MUONE KAMA MTAPATA AU MTALALAMIKA KAMA SASA! UFISADI HAKUUANZA NA KIKWETE AMERITHI UCHUMI CHINI YA MISINGI YA UFISADI WA MIAKA 46!

    ReplyDelete
  16. inonekana hoja zingine zinagusa umuhimu wa mijadara, na zingine zinahitaji mwelekeo zaidi. issue'kwa sasa ni captalism'na democracy,, kwa hivyo, kaaeni mkao wa kula!

    ReplyDelete
  17. watu wengine mnaingiza masuala yenu ya udini kwenye masuala muhimu wala hao mitume wenu hawawajui ninyi watu weusi mnajipendekeza kwa wazungu na waarabu. tuachieni nchi yetu haina dini ni mimi Nyakanyahura

    ReplyDelete
  18. Ila wewe mchangiaji uliyegusia udini unashangaza.Andrew Chenge,Nimrod mkono,Edward Lowossa nao ni waislamu?Shida ukiwa mdini mawazo yako yanakuwa kidini dini tu.Huwezi kufikiri zaidi ya hapo ndugu?Toa hoja jinsi gani tulisaidie taifa letu!

    ReplyDelete
  19. huyo mdini hata darasa la kwanza alilo soma halimsaidi ndg huu niwakati wakutoa hoja si utumbo kama huna hoja ukalale na dini yako ebo.

    ReplyDelete
  20. Hatari ya Amani kutoweka Tanzania imekaribia kutokana na uongozi mbovu tulionao yaani watu wanawaburuza wenzao bila hata kujali kuwa na wao ni binadamu waliowaingiza madarakani. Sasa ndio watawaona kuwa Tanzania ya zamani sio ya sasa wananchi wa sasa ni waelewa na wanasoma.

    ReplyDelete
  21. jamani usomi tu haumsaidii mtu kua na huruma,hivi waliosaini richmond,dowans ni wa darasa la 7?mimi (si Mbunge) nitapeleka hoja binafsi bungeni ili tuwe kama wachina;kwamba mtu akikwapua mijihela hata kama kaisaidia ccm akipatikana na hatia anyongwe

    ReplyDelete
  22. Joseph Kaaya
    Washinton DC 4545
    USA.
    Inafikia wakati watanzania tutaamua kujitoa muhanga kwakuwa hakuna mtu anaependa kulala njaa na wakati mwizi akiendelea kulindwa na serikali. Hili liko wazi. Kikwete na lowasa pamoja na vibaraka wao kama makamba na na wana ccm wote wasio kuwa na elimu ya ubinadamu ni maadui wakubwa kwa binaadamu wa aina yeyote, hii ni kuanzia kwa wake zao na familia zao kwa ujumla sasa ni hivi, wajiandae siku yaja watakuwa na hizo ela ila amani kwao itakuwa ni historia. Unawezaje kuishi kwa kuujumu majasho ya wanyonge? Unakumbuka Bush alipokuwa Iraq, yule alie mtupia kiatu sio kwamba alikuwa anatafuta ujiko ni kwamba aliamua kuonyesha wazi machugu yake. Ninaichukia nchi kwajili ya hawa wachache wanaotunyima usingizi.

    ReplyDelete
  23. Karibu asilimia 70 ya maoni mbalix2 yatolewamo hapa Majira huwa yanamalizikia kumlaumu JK in person na kama kwamba yeye tulimpa pesa atunulie nchi iliyo nzuri na badala yake katuletea Tanzania.

    Munajisumbua tu. Nani anaeiendesha TZ? Tanzania imetoa wasomi wangapi hadi sasa. Pia angalia sehemu zote nyeti zinaongozwa na waTz lakini bado tunalalamika.

    Ukweli ni mfumo(system) mulioukubali na kuupigia debe miaka karibu 50 sasa ndio wa kulaumiwa. Na ukifanya hivi, wewe na mimi ndio wa kulaumiwa kwani kwa sababu ya roho zetu ni mbovu na hatutaki kwenda na wakati. Na ikiwa hamtobadilka vichwa vyenu, tutaendelea na sakata hili kwa nusu karne ijayo.

    Hata wewe mchangiaji ikiwa utapewa uongozi katika mfumo huu nini kipya utakileta. Usijidanganye, muda utapita na lawama zitakuwepo pale x2.

    Kutafuta mchawi, yaani JK, udini, ukabila ni kupoteza wakati. Mgonjwa hamfichi dakitari vyenginevo, hatopata matibabu sahihi.

    Tunatakiwa tuwe na SYSTEM OVERHAUL baada ya kujua nini tunataka.

    Mwisho, ICC na waTZ c wapumbavu kukubali kuheshimu uamuzi wa mahkama. Ikiwa kampuni imesajiliwa kihalali na wamiliki hawakujulikana tokea awali, ni Mrajisi wa Makampuni na Wizara husika ndio responsible sio JK, uisilamu, ukabila na lawama za kijinga!.

    ReplyDelete
  24. NAKUUNGA MKONO HAPO NI PERSONAL ATTACK TO JK, LAKINI AGENDA YAO HAWA HAWA JAMAA HAILENGI HUKO KWENYE SUBSTANCE NA ROOT COURSE ANALYSIS, NA NDIO MAANA MCHANGIAJI ALIOYOTAJA HIDEN AJENDA YA UDINI AKAGUSIA HILO, KWANI HATA MZEE RUKSA WALIMWANDAMA PERSONAL AS IF HAWA VIOGOZI HAWAKUTAWALA CHINI YA CCM MANIFESTO! HIVYO NI HAKI KUMUANDAMA JK AS IF NI ABSOLUTE MONARCH WAKATI NCHI INAONGOZWA NA SYSTEM ILE ILE TOKEA AZIMIO LA ARUSHA LIANZE KAZI? WAKATI WA MWALIMU KULIKUWA NA RAMPANT CORRUPTION HATUKUSIKIA FISADI HATA MMOJA KUPANDISHWA MAHAKAMANI, SOKOINE AMEKWENDA NA MAJI KISA NI VITA DHIDI YA MAFISADI! LEO MAFISADI TUNWAONA WANSHUSHWA KWENYE KARANDINGA KUINGIZWA MAHAKAMANI KATIKA UONGOZI WA NANI KAMA SIO JK? USISHNGAE HWA WANOPIGA KELEL KAMA JK HAFAI NI HAO HAO MBWEHA KATIKA NGOZI YA KONDOO, WANALILIA KAMA NDIO VICTIMS KUMBE WANATAKA AONDOKE WAENDELEE KUPORA MALI ZA TAIFA NA RUSHWA!

    ReplyDelete
  25. Matatizo yaliopo ni makubwa sana ila nyinyi waandishi wa habari labda ndio mliochangio hili tatizo la Tanzania. Waandishi wengi wao wana agenda zao kibinafsi, au wametumwa, na matukeo yake TRUST in Tanzania is a non exist pheomena. Sasa sisi wasomaji tunachanganwa, na nyinyi wenye dhamiri hamupati munachokitaka. Maendeleo hayo munaojidai kuyatafuta mutayapata kweli? Musijidanganye watanzania...... Badilisheni mfumo wa Mawazo. Hizo mbio za Mwenge katika vichwa vyenu zitoke.

    ReplyDelete
  26. HATA KAMA NI MKEWAKE WA NDOA ATAJWE TU.

    ReplyDelete
  27. NA AKITAJWA ITAKUWA NINI? ITAPINDUA HUKUMU YA KULIPA HAYO MABILIONI YA HELA? MNAJIDANGANYA NYINYI. HII NDIO KARNE YA UTANDAWAZI! SHERIA ZINAPOTUMIKA MNALALAMIKA MNAFIKIRI SHERIA NI ZA TANZANIA TU ULIMWENGU HUU? ILIVYOKUWA TANZANIA IMAO KATIKA JAMII YA KIMATAIFA, HAINA BUDI KUFUATA SHERIA PALE AMBAPO ILIKOSEA!

    ReplyDelete
  28. Suala hapa si mfumo tu pia mkuu wa nchi anahusika moja kwa moja kutokana na mfumo huo kwa sababu anamadaraka makubwa kutokana na mfumo husika. Rais ana uwezo mkubwa wakubadili mambo na kukemea na kuwachukulia watu hatua. suala la dini halipo! kuhusu marais waliopita hawahusiki kwa sasa.Tadhmini alichofanya JK kwa kipindi chake kwa kuangalia mipango ya serikali na matokeo halisi. wanasiasa watakuchanganya kwa kukudanganya masuala ya dini kumbe anakunyonya. wanao umia ni wewe na mimi si dini. cha msingi kama Mkapa alikosea mbona JK ajamchukulia hatua? naye analea Mafisadi, wadini zote. hivyo JK ni msanii namba 1. Watz kwa sasa wameelimika si kama zamani. Malipo ya Dorwans yasifanyike hadi hadi wamiliki wajulikane. K'sasa tunahitaji katiba mpya, tume huru ya uchaguzi na TAKUKURU huru. madaraka ya rais kupunguzwa pia. ili kulinda maslahi. si kumtetea rais kutokana na udini. ni ufinyu wa kufikiri na ujinga. rais kachaguliwa na dini zote. acha ushamba.Kielimu tz ni ya 47 kwa africa, kiuchumi ni ya 147 kidunia. kwa mwaka watz kati ya elf 60 na elf 80 hufa kwa malaria. hebu fikiria na rasilimali tunazo we unazungumzia udini. kifo hakichagui dini. acha hizo. tazama mustakabali wa nchi achaufinyu wa mawazo!Jk naserikali yake ni wasanii. badilika

    ReplyDelete
  29. it is is not real possible ! Richmond ilitamkwa ni kampuni ya mfukoni, mafisadi kwa kuwa wanajua ya hakika kuwa watanzania watasema tu na hawatachukua hatua yeyote, wakahamisha mali za kampuni hewa kwenda kwa DOWANS, bado wanasheria na viongozi wa serikali ya Tanzania wakanyamaza wakijua baada ya miaka tatu watanzania watakuwa wamesahau,

    kisheria kampuni feki haiwezi kutrasfer kile amabcho hakina uwezo wa kumuliki. "NEMO QUOD NON HABET" HUWEZI KUHAMISHA KILE AMBACHO HUNA AMA HUKIMILIKI KIHALALI

    fedha hizo zikilipwa basi naungana na MIZENGO PINDA kuwa kuna genge la watu wachache ambao hawaoni huruma na wana nia ya dhati kabisa ya kuchukua pesa za wavuja jasho.

    hivi kwenye mahakama ya usuluhuisho watanzania hawakuwakilshwa na waseme kuwa kile kilicho hamishwa kiulikuwa batili. Kama RICHMOND ilitajwa batili na kule nchi inayosemekana ilisajiliwa kukosekana je watanzania tunahitaji nini

    JE TUNATAKA MALAIKA AJE KUTUSEMEA, oh tanzania the beautiful cesspit" i hate your leader

    ReplyDelete