28 December 2010

Teena Marie afariki Dunia

LOS ANGELES, Marekani

MWANAMUZIKI Teena Marie, ambaye alikuwa akifahamika kama "Ivory Queen of Soul" amefariki Dunia, Jumapili akiwa na umri wa miaka 54.
Nyota huyo alitamba na nyimbo zake kama 'Lovergirl,' 'Square Biz,'  na
'Fire and Desire' mshauri wake akiwa Rick James.

Taarifa kutoka kituo cha Polisi cha Pasadena, zimesema kifo chake ni cha kawaida. Askari polisi na wa Idara ya Zimamoto waliitwa nyumbani kwake, baada ya familia kufika na kuita bila ya kujibiwa.

Katika mahojiano yake na Shirika la Habari la Associated Press (AP) mwaka jana, Teena Marie alisema alikuwa amepambana na kuachana na matumizi ya dawa za kulevya, mwaka jana alifanya ziara ya kupromoti albamu yake yake mwisho ya 'Congo Square.'

Marie si wa kwanza kuimba nyimbo za soul ni mwanamuziki aliyekuwa na kipaji na alipendwa na kuheshimiwa na mashabiki.

Kabla ya kuanza kipaji chake, alikuwa na na mahusiano ya karibu na jamii ya watu weusi, ambapo mmoja wao alikuwa mama yake wa ubatizo.

Alianza kuimba muziki wa soul, tangu akiwa mdogo na kuendelea nao.

Marie alianza kupata umaarufu baada ya kujiunga na lebo ya Motown label 1979, akawa ni mzungu wa kwanza kuvunja ubaguzi kwa kuingia katika lebo ambayo mmiliki wake ni mweusi, iliyowatoa wasanii weusi kama Stevie Wonder, Jackson Five, The Supremes na Marvin Gaye.

Alitoa wimbo kama 'Wild and Peaceful,' ambao Motown ilihofia kwamba usingependwa na mashabiki weusi kwa kutambua kuwa umeimbwa na mzungu.

Marie alitoa wimbo wa, 'I'm A Sucker for Your Love' ambao ulipendwa na kumtoa na kuonesha kuwa angekuwa nyota wa R&B.

Akiwa na Motown, mwandishi na mwimbaji huyo, alitengenza nyimbo nzuri za mapenzi kama 'Need Your Lovin' na 'Behind the Groove.'

Aliandiaka nyimbo kama 'Cassanova Brown' 'Portuguese Love' na 'Deja Vu (I've Been Here Before)' ambazo zilipendwa.

Wimbo 'Fire and Desire,' ni moja ya nyimbo alizoimba na Rick James, ambao ulizungumzia mapanzi na kufarakana ambao ulitamba katika ulimwengu wa muziki na kupigwa kwenye vituo mbalimbali vya redio.Marie aliachana na Motown 1982 na kisha kuishitaki lebo hiyo, kutokana na kumzuia kuingia katika lebo nyingine huku, wakiwa hawajaachia nyimbo zake.

Alifanya vizuri katika miaka ya 1980, alitoa nyimbo kama 'Lovergirl' na 'Ooo La La La' lakini alipanda sana wakati akiwa na Motown.Bado aliendelea kurekodi muziki na kufanya shoo. Mwaka 2004 na 2006 alitoa albamu mbili, ambazo zilikuwa na rap ya kiasili zilizopokewa vizuri chini ya lebo ya Cash Money Records, 'La Dona' na 'Sapphire.'

Akizungumzia kuhusu tuzo aliyopata ya Mfuko wa R&B, alisema ameifurahia mno.Akihojiwa na AP, mwanamuziki huyo alisema hakuwa na mpango wa kuachana na muziki.

No comments:

Post a Comment