13 December 2010

Muuguzi mbaroni kwa kunyanyasa mjamzito

Na Damiano Mkumbo, Singida

MUUGUZI mmoja wa Hospitali ya Mkoa wa Singida, Bi. Tatu Hassani (50) amekamatwa na polisi baada ya kufanya vitendo vya kumnyanyasa na kutukana mwanamke aliyetaka msaada wakati wa kujifungua.Hayo yalibainishwa juzi na
Kamanda wa Mkoa huo, Bibi Celinna Kaluba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kisa hicho kilichozua mzozo hospitalini hapo.

Kamanda Kaluba alieleza kuwa siku ya Desemba 9, mwaka huu saa 7:30 asubuhi mwanamke mjamzito Bi. Hadija Hassani (22) mkazi wa Majengo mjini Singida aliyekuwa amelezwa wadi No. 7 kwa ajili ya kujifungua alimwomba Bi. Hassani mssada kutokana na kujisikia hali ya uchungu.

Kamanda huyo alisema badala ya kumsaidia, muuguzi huyo alianza kumtukana matusi ya nguoni na kumlazimisha ajifunge kanga ili ahamishiwe wadi No. 6 chumba cha kujifungulia.

Alizidi kusema kuwa hata hivyo mzazi huyo akiwa katika hali isiyo nzuri alimweleza mtoa huduma huyo kuwa hatua iliyokuwa imefikia ni ngumu, kwani kichwa cha mtoto kilikwishatokeza na hangeweza kuondoka kitandani hapo.

Alisema kama vile haitoshi, muunguzi bila huruma alimlazimisha mama huyo anyanyuke na kwenda kwenye chumba cha kujifungulia kwani angechafua shuka na kitanda alichokuwa amelalia.

Alieleza kuwa muuguzi huyo alimpeleka kwa nguvu, lakini kabla ya kumfikisha wadi hiyo kichanga kilitoka na kudondoka sakafuni.
 Kamanda Kaluba alibainisha kuwa muuguzi huyo bado anashikiliwa na kuhojiwa na polisi wakati upelelezi unaendelea, huku hali ya kichanga hicho pamoja na mama yake zinaendelea vizuri.

4 comments:

  1. Pole sna mama, Mungu yupo nawe. Polisi na huyo muuguzi ahukumiwe hata miezi sita 6 iwe fundisho kwa wengine wasijewakafanya kitendo chas ukatilii kama hicho.

    ReplyDelete
  2. Kina mama ndo tunaenda labor lakini ndo tunaroho mbaya kuliko. Yaani ukienda hospital ukimkuta daktari mwanaume utajifungua salama na hutasikia akikutukana. lakini wamama mmmh! jamani achukuliwe hatua kali huyo nurse.

    ReplyDelete
  3. This is Bongo Bwana! hakuna Maadili sehemu za kazi wala nini! Pole dada, Mungu awapa Afya njema wewe na mtoto! Ila kwa huyo nesi kesi yake isiishie mahakamani tu, lakini pia kwenye kamati ya maadili ya chama cha wauguzi na wakunga TZ.

    ReplyDelete
  4. mimi huwa nawaonea sana huruma kina mama kwa ugumu wa maisha lakini kwahili alilolifanya.si vema akarudishwa tena katk fani hio

    ReplyDelete