13 December 2010

Dhambi ya ubaguzi yaitafuna CCM Zanzibar

Na Emmanuel Kwitema

MFANYABIASHARA maarufu na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar, Bw. Mohamed Raza amekitahadharisha chama hicho kuwa kitatoweka visiwani humo endapo hakitarekebisha mapungufu yaliyojitokeza katika Uchaguzi Mkuu wa
Oktoba 2010.

Alisema hayo alipokutana na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana wakati akitoa tathmini yake kuwa ushindi wa chama hicho katika uchaguzi huo haukuwa wa kishindo kama walivyotarajia, kwani asilimia 50 na nukta kidogo walizopata ni dalili mbaya.

Alitoa mfano kuwa miaka ya nyuma CCM kilikuwa na majimbo Pemba, sasa hakuna hata moja na pale Zanzibar hivi sasa majimbo manne yamechukuliwa na wapinzani wao na kuongeza kuwa kama chama hakitakuwa wazi kuelezea yaliyojiri, basi Uchaguzi Mkuu ujao wa 2015 kwa upande wa Zanzibar wasishangae majimbo zaidi yakaangukia upinzani kitendo kitakachofanya chama chao kuambulia nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.

"Kwa kuwa Uchaguzi Mkuu ujao hauko mbali, basi ni vyema chama kikakaa chini na kufanya tathmini ya kina na kwa uwazi kikihusisha Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya chama hicho ili kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza", alisisitiza Bw. Raza.

Bw. Raza alionesha kushangazwa na kutoshirikishwa kwa viongozi wastaafu wa Zanzibar katika mchakato mzima wa uchaguzi. Alisema tangu ufunguzi wa kampeni za uchaguzi visiwani humo hadi kumalizika hakuna kiongozi aliyepewa nafasi kuhutubia mikutano hiyo.

Alisema hata kiongozi aliyepangwa katika ratiba kuhutubia moja ya mikutano hiyo, ratiba hiyo ilifutwa na viongozi wenyewe wa CCM bila sababu za msingi.

Aliutaka uongozi wa chama hicho visiwani humo kuwaeleza wanachama wao kwa nini walifanya hivyo na kusisitiza kuwa viongozi wastaafu wana nafasi zao.Akizungumzia usawa, Bw. Raza aliitaka CCM na SMZ kutenda haki kwa viongozi wote wastaafu, kinyume cha hivyo kitakuwa kinatayarisha na kuunda matabaka ya viongozi hao.

Alisema haoni sababu kwa nini kati ya viongozi hao wastaafu wengine wawe na magari ya kuwaongoza na wengine wasiwe nayo; wengine wapewe magari aina ya benz na wengine wasipewe.Alisisitiza kuwa katika CCM hakuna bwana mkubwa wala umaarufu wa mtu, bali chama wanachokitumikia na kusisitiza kwamba asingetaka kuiona Zanzibar yenye matabaka ya wastaafu na ili kuondokana na hilo katiba ya nchi na sheria zifuatwe katika kuteleza usawa huo.

Awali, Bw. Raza alitoa shukrani na pongezi kwa ushindi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 na hasa Zanzibar ambako baadaye kuliundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyojumuisha Chama cha Wananchi (CUF).Bw. Raza alisema serikali hiyo isibezwe wala kupuuzwa ili kudumisha hali ya amani na utulivu visiwani humo.

4 comments:

  1. Raza unajulikana kwa kumpigia debe na kujipendekeza kwa Salmin Amour! Kumbukumbu zinaonyesha ulikwenda ikulu kumuona Salmin alipokuwa rais, ukaingia straight ndani kwa mzee, wakati wengine walikua ktk bench kusubiri zamu zao including Karume ambaye alikuwa ni waziri wa mawasiliano! lakini wewe kwa ushawishi wako tu ukamdharau na kuingia tu bila kujali kuwa kuna watu wamekaa foleni kungoja kuingia ndani! Waswahili husema aliye juu mngoje chini! naam, enzi za salmini zikapita akaingia Karume, na wewe ndio ulishamkera teana ukawa hupati importance yoyote kwa karume, ni kama heshima yako ilishuka! ukajitia kugombea uwakilishi jimbo la kawo salmini, ukaambulia kura moja ktk preliminaries! Oh God! uchungu wako basi unapita ukieneza sumu tu against Karume, Kila siku ukiamka una mpya juu ya Karume! mara hili, mara lile, ili mradi tu umchokoe chokoe, kwani umesahau kuwa ulimpita ktk benchi ikulu ukaingia ndani kwa mheshimiwa? wacha choko choko zako, Karume ndio ameifikisha Zanzibar hapa tulipo! kama si yeye sijui tungekuwa wapi! kama unauchungu basi kunywa sumu ufe! Kama Salmini kakutuma basi wacha ukuwadi, na yeye ni mwanaume mwabie apande ktk kiriri aongee, ni hodari kwa hilo tunamjua!

    ReplyDelete
  2. Nice,Tabora
    Bw .Raza wewe ni fisadi,unategemea kuiba fedha serikalini kwa kuagiza na kuuza mchele mbovu kwa wazenji.wamekubana sana unaropoka ovyo.kuwa mkweli ,umesahau nini kwa Wazanzibari..

    ReplyDelete
  3. Mpeni haki yake Raza na msimzushie. Raza hafanyi biashara ya mchele. Mchele mbovu umeletwa na Bombay Bazar ambaye rafiki yake Karume na wakati wake Wazanzibari walikuwa wanalazimishwa kula mchele huo huo. Inashangaza, ama kweli nyani haoni kundule! Karume ametufikisha hapa, nani aliosababisha wapemba kukimbilia Mombasa? mauaji ya Pemba yalitokea wakati wa Salmini? au mnampongeza Karume kwa kumfanya Seif asikose cha kuambulia kwenye uchaguzi?

    Salmini kama mstaafu ana haki ya kpata kile kilichomuajibikia kwa mujibu wa Katiba bila ya ubaguzi. Viva Komandoo

    ReplyDelete
  4. Haya ndio mambo ya kuongea sio makamba anasema kila saa kuenda mahakamani kupotezea watu muda na akili yake mgando. kama amekosa la kuwaambia wanachama apishe, makomandoo wakimemende chama.

    ReplyDelete