Na Theonestina Juma, Ngara
MCHUNGAJI wa Kanisa la Pentekoste wilayani Ngara, Bi. Anna Mulengera (40) na waumini wake wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ngara na kuamriwa kupimwa akili baada ya kudai watadhaminiwa kwa damu ya Yesu katika
kesi yao ya kuanzisha kanisa bila kibali.
Nchungaji huyo na wenzake ambao walikuwa wamepiga kambi katikati ya pori la Nyakafandi wilayani hapa baada ya kukimbia nyumba zao kunyunyiziwa dawa ya kuua mazalia ya mbu, wamekuwa wakiripotiwa na gazeti hili kuhusu imani yao ya ajabu ambayo wanasema haitaki kuchanganya mambo ya Mungu na ya dunia.
Kutokana na kauli hiyo, waumini hao licha ya kukiri kuanzisha kanisa bila kibali, wako rumande wakisuburi kupimwa akili, ili mahakama kujiridhisha kama wako sawa au la au hadi 'Damu ya Yesu' itakapowadhamini.
Wakisomewa maelezo ya kosa na Mwendesha Mashtaka, Inspekta John Kesi, ilidaiwa kuwa watu hao kwa pamoja walianzisha kanisa bila kibali Oktoba 17, mwaka huu katika Kijiji cha Mukubu wilayani humo.
Pamoja na waumini hao pamoja na mchungaji wao kukiri kuanzisha kanisa hilo bila kibali, walimwacha hoi Hakimu wa Wilaya hiyo aliyekuwa akiendesha kesi hiyo alipowataka kuleta wadhamini, nao wakamjibu 'tutadhaminiwa kwa damu ya Yesu kwa vile mdhamini wetu ni Mungu'.
Kauli hiyo ilimfanya Hakimu wa Mahakama hiyo, Bw. Idrisa Katera kuagiza watu hao kupimwa akili zao kama ziko timamu au la kabla ya mahakama kuchukua hatua zaidi dhidi yao.
Pamoja na Mchungaji Mulengera, wengine waliofikishwa mahakamani, Bw. Fransisco Zakaria (54), Emmanuel Revelian (27), Beatrice Leonard (21) na Mercy Fransisco (41), wote ni raia wa Burundi.Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Desemba 10, mwaka huu lilipotolewa agizo la kuwapima akili, na kesi yao kutajwa tena jana, ambapo iliahirishwa tena kwa kuwa agizo hilo halikuwa limetekelezwa.
Hakimu Katera aliahirisha tena kesi hiyo hadi Desemba 27, mwaka huu itakapotajwa, huku ikisubiriwa hatua ya kuwapima watuhumiwa akili.
Wakati huo huo, waumini wa wengine waliobaki katika pori hilo wakiwemo watoto sita wenye umri wa mwaka mmoja hadi mitano wameamuriwa kuondoka katika eneo hilo, kwa vile kanisa hilo halitambuliwi kisheria.
Habari kutoka eneo hilo zinaeleza kuwa tayari watoto ambao wazazi wao wanashikiliwa wamekwenda kwa walezi wao huku waumini wengine wakirejea kwenye nyumba zao, ambapo inadaiwa kuwa kabla ya kuingia 'waliangusha' sala za nguvu kwa ajili ya kufukuza mapepo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mukubu, Bw. Christian Ndenzako alisema hana uhakika kama watu hao washarejea kwenye nyumba zao kulingana na imani yao kali.
Duh...Ukristo una kazi..mara binadamu anakuwa na haki ya kumpokonya Ukristo mfuasi....mara wanataka kusafiri na kufika Uwanja wa ndege wa kimataifa wakisubiri paspoti kutoka kwa Yesu....mara wanatengwa kumshabikia muislamu kwenye uchaguzi....mara hili mara lile. Hivi hamuutukanishi ukristo mbele ya waumini wakristo duniani? Hivi ni ukosefu wa elimu au ujinga uliokithiri? Nadhani waanze kupimwa akili viongozi wa Kuu wa dini hapa nchini kwanza. Tuanze na shina badala ya matawi
ReplyDeleteHawa ni vichaa tu toka Burundi.Wameathirika kisaikolojia kutukana na vita.
ReplyDeleteHawajui walitendalo hakimu watoe tu.
ReplyDeleteAcha wakale sikukuu huko lupango,wakitoka watamkuta yesu anawasubiri kuwapa dhamana
ReplyDeleteHAKIMU HAWA WATU HAWAJAMTUKANA MTU HAWAJATENDA KOSA LOLOTE LA JINAI,HILO KANISA NA WAUMINI WAKO WAPI? KUNYUNYIZA DAWA YA KUUA MAZALIA YA MBU SI KIGEZO CHA KUWAKAMATA.AU WAO KUISHI MSTUNI ILI MLADI HAWAVUNJI SHERIA BAADO HAITOSHI KUWAKAMATA LABDA KWA VILE UMESEMA SI RAIA WA TZ HILO NI SWALA LINGINE.KUHUSU IMANI KILA MTU ANAHAKI YA KUABUDU ATAKAVYO ILI MLADI ASIVUNJE SHERIA. NA SWALA LA KUTHAMINIWA NA YESU KIPI CHA AJABU : NI UPEO WENU TU WA KUELEWA UKRISTO : WAO =MAANA YAKE "WAO WAKO TAYARI KUTESWA KWA AJILI YA YESU KRISTO HATA KAMA NI KUFUNGWA" MAANA SIKU YA MWISHO HAKIKA WATAVALISHWA TAJI. KWANI KIPI CHA AJABU HATA MITUME WALIFUNGWA, WALIPIGWA, WALICHOMWA MOTO WALIPITISHWA KWENYE MAFUTA YALIYOCHEMKA.
ReplyDeleteNB:
(1)NATAATHARISHA KWAMBA MASWALA YA IMANI YASIRUHUSIWE KUCHANGIWA KWENYE MITANDAO KWANI NI MAMBO AMBAYO YANAGUSA IMANI YA KIKUNDI AU WATU WA IMANI FULANI.
Anonymous said...
ReplyDeletewewe ni kipi kilichokuumiza kwa imani ya hao watu hadi kuingiza kwenye ukristo ni kipi bora kati ya imani yao na kujilipua na kuuwa watu wasikuwa na hatia kunakofanywa na waislam, mambo ya imani ya mtu usiingize kwenye imani ya watu wengine.
yaani hawa hawana tofauti na wale wasabato masalia, saizi wenzao wanaishi porini kule segerea sanene. wanahabari tunaomba mkawamulike hawa watu kujua kulikoni manake wanalala kwenye nyumba za miti na majani. mvua zikinyesha wanatia huruma sana,kama inawezekana warudishwe kwao
ReplyDelete