Na John Gagarini, Kibaha
TIMU ya Maili Moja United ya Kibaha, imeisambaratisha timu ya Back Town kwa mabao 7-0 kwenye mchezo wa Ligi ya Wilaya ya Kibaha, Pwani.Mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Mwendapole ulikuwa wa upande mmoja hasa Back Town kuonesha
udhaifu kwa kushambuliwa kila wakati.
Washindi walianza kuandika bao dakika ya kwanza ya mchezo kupitia kwa Musa Pablo huku wakishangaa walishtukia wakipigwa la pili na Valentine Kikuyo kwenye dakika ya 25 ambaye pia alifunga bao jingine dakika ya 61.
Timu hizo hadi zinakwenda mapumziko washindi walikuwa mbele kwa mabao 2-0, kipindi cha pili United waliendeleza mashambulizi na walifunga bao la tatu kupitia kwa Samson Sembuli dakika ya 46 ya mchezo.
Wakitandaza kandanda safi United walihesabu bao la nne kupitia kwa Mchemba Majaliwa dakika ya 70 na Inocent aliipatia timu yake bao la sita dakika ya 85 na la saba dakika ya 88.
No comments:
Post a Comment