05 November 2010

Watatu gofu kuongeza nguvu Rwanda Open.

Na Andrew Ignas

WACHEZAJI wa tatu wa mchezo wa gofu nchini wanatarajia kwenda nchini Rwanda kuungana na wenzao sita walioopo nchini humo kwa ajili ya mashindano ya Rwanda Open
yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi leo.

Akizungumza Dar ers Salaam jana, Msemaji  wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU), Sophia Nyanjera alisema wachezaji hao wataondoka leo kwenda nchini Rwanda kwaajili ya kushiriki michuano hiyo.

"Katika michuano hii Tanzania imepata wawakilishi tisa ambao wataiwakilikishi taifa ambapo nchi za Afrika Mashariki na Kati kama Burundi,Uganda, Kenya, Malawi,Tanzania, pamoja na wenyeji Rwanda" alisema Nyanjera.

Aliwataja wachezahi hao ni ni Abbas Adam, Frank Roman na Jimmy Molel wote wa Dar es Salaam.

Aliwataka wachezaji kwenda kuonesha kiwango kizuri kitachowezesha timu yao kutwaa ubingwa huo.

No comments:

Post a Comment