Na Omary Mngindo, Kibaha
TIMU ya netiboli ya Ruvu JKT ya Kibaha Mkoa wa Pwani, imeanza kambi kwa ajili ligi ya netiboli daraja la pili taifa.Akizungumza mjini hapa jana, kocha
wa timu hiyo, Zainabu Halakahiya
alisema kikosi chake kimeanza kambi kuanzia Novemba 2, mwaka huu kujiandaa na michuano hiyo.
Alisema kutokana na kuchelewa kuanza kwa mazozi ya timu yao, kwa sasa
watafanya kwa siku mara tatu kwa ajili ya kujiweka vizuri zaidi kabla ya ligi hiyo kuanza.
"Tumechelewa kuanza kambi kutokana na shughuli za kikazi, hivyo tumaanza mazoezi rasmi tayari kwa kinyang'anyiro, hicho ambapo tuna uhakika mkubwa kwamba tutafanya vizuri," alisema Halakahiya.
Alisema pamoja na kuchelewa kuanza kwa mazoezi, lakini kutokana na kuwa
na wachezaji wazuri waliokiwezesha kikosi hicho kutwaa nafasi ya pili kwenye ya ligi ya mkoa, wanaimani watafanya vizuri.
Ruvu JKT ni washindi wa pili wa Mkoa wa Pwani na bingwa wake ni Polisi Pwani, ambayo nayo inatarajia kuanza mazoezi hivi karibuni kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Absalom Mwakyoma.
Washindi wa tatu ambao nao watashiriki mashindano hayo ni timu ya Kwamfipa, ambayo pia
itashiriki ligi hiyo.
No comments:
Post a Comment