02 November 2010

Rais Kikwete atuma salamu za rambirambi.

Na Mwandishi Wetu

RAIS Jakaya Kikwete, ametuma salamu za rambirambi kwa Chuo Kikuu Huria (OUT), kwa kifo cha mkufunzi Syllersaid Mziray kilichotokea
Jumamosi jijini Dar es Salaam.

Mziray alizikwa jana kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Katika taarifa yake ya rambirambi kwa OUT, Rais Kikwete alimwelezea Mziray kama mmoja wa wachangiaji wakubwa katika mpira wa miguu nchini na atakumbukwa katika historia ya soka.
Kifo cha Mziray ni pigo kubwa kwa taifa letu, mashabiki wa mpira wa miguu nchini na wapenda michezo kwa ujumla.
Rais Kikwete alielezea masikitiko yake kuwa taifa bado lilikuwa likimhitaji katika wakati huu ambapo soka la Tanzania limeanza kukua, na hivyo mchango wake ulikuwa mkubwa katika kufikisha soka katika kiwango cha juu nchini.

Tumuenzi kwa kuongeza juhudi katika michezo hapa nchini, tutie juhudi katika kukuza viwango vya mpira wa miguu na michezo yote kwa ujumla, kama alivyokuwa anakusudia marehemu,¡± alisisitiza Rais.

Rais Kikwete ameitakia familia, ndugu na marafiki wa marehemu Mziray kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu kwao na pia ameungana nao katika kuiombea roho ya marehemu mapumziko mema peponi.

No comments:

Post a Comment