08 November 2010

Newcastle yaifumua Arsenal.

LONDON, Uingereza

BAO pekee lililofungwa kwa kichwa na Andy Carroll, kupindi cha kwanza lilitosha kuwafanya Arsenal, kulala nyumbani katika Uwanja wa Emirates dhidi ya
Newcastle, ukiwa ni ushindi wao wa kwanza katika kipindi cha miaka mitano.

Carroll aliruka juu zaidi na kumzidi maarifa kipa wa Arsenal, Lucasz Fabianski aliyekuwa ameruka kutaka kuokoa mpira wa adhabu, uliopigwa na Joey Barton.

Awali, Cesc Fabregas alikosa goli baada ya shuti lake kugonga mwamba huku mpira wa adhabu wa Samir Nasri, uliokolewa na kipa wa Newcastle, Tim Krul.

Theo Walcott naye alipiga shuti na mpira kugonga mwamba, wakati Laurent Koscielny alitolewa kwa kadi nyekundu, dakika za mwisho na kufanya Arsenal kucheza pungufu.

Kwa matokeo hayo Arsenal, imebakia pointi 20 katika nafasi ya tatu, huku Newcastle wakipanda hadi nafasi ya nne kwa kufikisha pointi 17, huku zote zikiwa zimecheza mechi 11.

Chelsea kabla ya kucheza mechi yao ya jana dhidi ya Liverpool, ilikuwa ikiongoza kwa kuwa na pointi 25 ikifuatiwa na Manchester United, yenye pointi 23.

No comments:

Post a Comment