07 November 2010

Mtoto auawa kikatili.

Na Mwandishi Wetu,  Shinyanga
 
MWANAFUNZI wa Darasa la Kwanza katika Shule ya Msingi Bukondamoyo wilayani Kahama mkoani Shinyanga ameuawa kikatili baada ya kupigwa na kitu
butu kichwani na watu wasiojulikana na kufa papo hapo.
 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga Bw. Daudi Siasi amemtaja mwanafunzi aliyeuawa kuwa ni Sofia Juma mwenye umri wa miaka nane mkazi wa Kijiji cha Mhungula wilayani
Kahama.
 
Kamanda Siasi alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 9.45 mchana huko katika kijiji cha Mhungula baada ya mwanafunzi huyo kupigwa na kitu butu kichwani na mtu au watu
wasiojulikana.
 
Hata hivyo kamanda Siasi alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha mauaji hayo kinatokana na ugomvi wa kumgombea mwanafunzi huyo kati ya Bw. Chogole Alphonce (33) na Bw. Juma Kagunila (48) wote wakazi wa kijiji cha Shunu wilayani Kahama.
 
Kamanda Siasi alisema mpaka hivi sasa polisi inamshikilia Bw. Chongole anayetuhumiwa kuhusika na mauaji hayo na kwamba baada ya upelelezi huenda akafikishwa mahakamani
kujibu shitaka la mauaji.

No comments:

Post a Comment