04 November 2010

Maugo amwendea Cheka Kenya.

Na Addolph Bruno

BONDIA Mada Maugo, anatarajia kwenda Nairobi, Kenya keshokutwa kujiandaa na pambano lake lisilo la ubingwa, dhidi ya Bingwa wa Mabara
Francis Cheka, litakalochezwa Januari Mosi mwakani.

Maugo atapanda ulingoni kuzichapa na Cheka katika pambano lao la kwanza kukutana la uzani wa kati kg. 72.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Maugo alisema ameamua kwenda nchini Kenya kwa ajili ya kumfuata kocha wake, ambaye anaishi nchini humo.

"Nimeamua kwenda huko kumfuata kocha wangu, lakini pia nakwenda kujifunza mambo mengi kuhusu ngumi, ili nishinde mchezo wangu huo," alisema Maugo.

Maugo alisema hakuna kitakaochomzuia kumpiga Cheka, kwa kuwa hadi sasa anaona ushindi ni wake na atahakikisha anafanya hivyo, ili kuwafurahisha mashabiki wake.

Alisema Safari yake itaanzia Dar es salaam, baada ya kuwasili leo kutoka mkoani Mara, ambako alikuwa akitoa mafunzo kwa wanafunzi wa shule za msingi kuhusu mchezo huo.

No comments:

Post a Comment