04 November 2010

Matokeo Segerea yatangazwa saa 8 usiku.

Na Kulwa Mzee

PAMOJA na mvutano mkali na shinikizo kutoka kwa wafuasi wa CHADEMA hatimaye Msimamizi wa Uchaguzi wa majimbo ya Segerea na Ukonda
, Bw. Fuime Gabrieli ametangaza matokeo ya ubunge yaliyoipa ushindi CCM.

Bw. Gabriel alitangaza matokeo hayo jana saa nane usiku baada ya kushindikana siku nzima ya juzi kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo ucheleweshaji wa masanduku ya kupigia kura kutoka kata sita za Segerea na tatu za Ukonga.

Bw. Gabrieli alimtanga Dkt. Makongoro Mahanga (CCM) kuwa mshindi baada ya kupata kura 43,554 na kumpita mpinzania wake, Bw. Fredy Mpendazoe (CHADEMA) aliyepata kura 39,150 wakiwa na tofauti ya kura 4,404.

Katika Jimbo la Ukonga, Bi. Eugen Mwaiposa (CCM) aliibuka mshindi kwa kupata kura 28,000 na mpinzania wake, Bw. James Binagi aliyeambulia kura 17,059, tofauti ya kura 10,941.

Kwa upande wa Jimbo la Ilala, Bw. Mussa Zungu (CCM) aliibuka na ushindi wa kura 25,940, CHADEMA walipata kura 8,530 tofauti ya kura 17, 410.

Matokeo hayo yanaonesha ushindi mnono wa CCM ambayo kwa upande wa udiwani, imepoteza kata mbili za Segerea na Kimanga.

1 comment:

  1. Matokeo haya ni upuuzi, aibu na fedheha kwa CCM, Kikwete na Serikali yake. Segerea haitakubali upuuzi huo kufanyika katika wakati huu. Ukweli wanawake na watoto ukiacha wanaume wanaishangaa Tume ya uchaguzi na kuchicheka CCm ilivyochoka. Sijui itawaleteaje wananchi maendeleo wakati hawatakiwi?

    ReplyDelete