02 November 2010

Kura zayeyuka Segerea, Ukonga.

Na Kulwa Mzee

MATOKEA ya kura za urais na ubunge katika Jimbo la Ukonga na Segerea bado ni tata kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo sanduku la kura za rais kukutwa
likiwa wazi na halina kura hata moja.

Msimamizi wa Uchaguzi Manispaa ya Ilala, Bw. Fuime Gabrieli  alisema hayo jana alipozungumza na waandishi waandishi wa habari jana.

Alisema kazi ya kuhesabu kura za ubunge na urais haijakamilika kwa sababu ya uchelewaji wa masanduku ya kura kutoka katika vituo na kutokuwepo kwa karatasi za matokeo kwa baadhi ya vituo vyenye watu wengi.

"Uchaguzi ulifanyika vizuri vituoni, kura zilihesabiwa lakini tatizo lilianzia katika kitendo cha kupeleka karatasi za matokeo kwa msimamizi wa kata," alisema na kuongeza kwamba huenda baadhi ya wasimamizi waliweka karatasi hizo katika bahasha na kusahau mahali walipoweka, hivyo zinatafutwa.

Alisema hawawezi kuhesabu kura kama karatasi hizo hazijapatikana kwani ni muhimu na ndizo zinahitajika kwa ajili ya kuingiza katika kompyuta na kulinganisha matokeo.

Akizungumzia malalamiko yaliyojitokeza kutoka kwa viongozi wa vyama vya siasa kwamba kuna sanduku la kura za rais lilikutwa wazi na halina kura hata moja, alisema hawezi kutolea ufafanuzi badala yake atalipeleka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, wakalijadili na kulitolea uamuzi.

"Matatizo hayo siwezi kuyatolea ufafanuzi, tumezungumza na viongozi wa vyama, tumekubaliana wasubiri uamuzi wa tume, ikiamuru kuwachukulia hatua waliohusika hatua zitachukuliwa," alisema.

5 comments:

  1. Msimamizi awajibishwe kwani ameshindwa kuwajibika pia ni muhimu mfumo wa tume ya uchaguzi ubadilishwe badala ya tume kuwajibika kwa serikali iwajibike kwa wanachi kupitia vyama vyao

    ReplyDelete
  2. kwani wasimamizi waweke kura kwenye bahasha ili hali walikuwa na masanduku ya tume kwa ajili ya kazi hiyo....@msimamizi mkuu wa majimbo husika awajibishwa kabla sisi wananchi tulio na uchungu wa nchi yetu hatujamshughulikia...itamwagika damu yake ya watanzania tulio wengi...

    ReplyDelete
  3. kwani si zimeshahesabiwa? wajumlishe matokeo ya vituo waache longolongo

    ReplyDelete
  4. niaibu kubwa kwa Serikali Ya tanzania kwani Kitendo cha sanduku la kura kukutwa tupu inaonyesha jinsi gani hatuna demokrasi na watu wenye pesa wana nunua kura. Niaibu kubwa ndiyo maana hatuta endelea kama Nchi kwasababu ya vitendo kama hivyo.Wizi umejaa nchini kote hakuna haki ya kweli bali ni yakununua. Aluta Kontinua Mabadiliko yatatokea aitha kwa amani au kwadamu. Serikali inabidi isimamie haki za watu sio pesa.

    ReplyDelete
  5. Bila tume huru kura zitaendelea tu kuyeyuka hata kama kuna baridi. Cha msingi watanzania wenye kutaka kuona viongozi wakiwajibika kwa watanzania ni lazima kuhimiza katiba mpya ambayo itaweka namna ya kupata tume huru ya uchaguzi.

    ReplyDelete