02 November 2010

Kikwete, Slaa haitabiriki.

Na John Daniel

WAKATI Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajiwa kutangaza matokeo ya jumla ya urais muda wowote kuanzaia leo, mchuano umeendelea kuwa mkali
baina wagombea wa CCM na CHADEMA kwa ngazi ya urais bara na CUF Zanzibar huku vigogo kadhaa wa CCM, wakiangushwa vibaya katika ngazi ya ubunge.

Kuangushwa kwa vigogo hao ni dalili ya mabadiliko makubwa katika bunge lijalo, ambalo ni dhahiri kuwa litakuwa na sura nyingi mpya kutoka kambi ya upinzani, endapo CCM itaendelea kushikilia kiti cha urais.

Baadhi ya vigogo waliobwagwa katika uchaguzi huo ni Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Lawrance Masha pamoja na Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dkt. Baltilda Burian, na Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Bw. Anthony Diallo.

Wakati vigogo hao wakiangushwa vibaya pia magwiji wengine wa CCM bado wako hatarini kufuata mkondo huo baada ya hali kuwa tata katika majimbo yao.

Vigoho hao ni aliyekuwa Spika wa Bunge la Afrika Dkt. Getrude Mongela, Waziri wa habari Utamaduni na Michezo Bw. George Mkuchika, aliyekuwa mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Andrew Chenge pamoja na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Bw. Basil Mramba.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa jana jioni na Msimizi wa Uchaguzi Jimbo la Nyamagana, Bw. Masha alibwagwa na mgombea wa CHADEMA) Bw. Ezekia Wenje kwa kura huku Dkt. Burian akiangushwa na Bw. Godbless Lema wa CHADEMA.

Awali kucheleweshwa kwa matokeo katika majimbo hayo kulizuia tafrani baada ya wananchi kuamua kujikusanya katika Ofisi za wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha matokeo yanatangazwa kama walivyotarajia baada ya kufanya majumuisha yao kwa kila kata.

Katika Jimbo la Ukerewe kwa mujibu wa matokeo ya awali, mgombea wa CCM, Bi. Getrude Mongela alikuwa ameshindwa na mgombea wa CHADEMA.

Lakini kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kwenye majimbo ya uchaguzi ambayo matokeo rasmi ya urais yalitangazwa, Rais Kayaka Kikwete alikuwa anaongoza kwa kura nyingi, akifuatiwa na Dkt. Willibrod Slaa wa Chadema huku Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF akichomoza kwenye kura za Zanzibar.

Kulingana na matokeo hayo, rais Kikwete alionekana kupata kura nyingi hata kwenye maeneo ambayo wagombea wa chama chake wamepata kura kidogo.

15 comments:

  1. Hii tume ya uchaguzi(NEC) iwe tume huru.Sio viongozi wake wateuliwe na Rais ndo maana wanaogopa kumwangusha aliewaweka Madarakani

    ReplyDelete
  2. Tunahitaji katiba mpya

    ReplyDelete
  3. Atakaye kuja kuikomboa Tanzania ni Slaha au mtu yeyote toka upinzani, wengini ni ufisadi tu

    ReplyDelete
  4. Nyerere uko wapi Baba tunazidi kuangamia tuokoe baba. haki haipo, kilio cha watanzania nani atakisikiajamani, haki inauzwa wapi nininunue na niigawe kwa viongozi hawa?

    ReplyDelete
  5. Watanzania tulio wengi hatujui umasikini wetu unatokana na siasa chafu zilizomo katika chama tawala.
    Iweje leo Tanzania katiba yake ni ile ya enzi za ukoloni, na hakuna anayewaza kuifanyia marekebisho. Watanzania tuamke, nchiyetu itapaa pale tu katiba itakapobadilishwa, kwani mafisadi wanatetewa sana na katiba hii tuliyonayo.

    ReplyDelete
  6. Tunawatakia chadema mafanikio mema kwa ushindi walioupata wa kuongeza majimbo. lakini msibweteke mtumie muda wa kwenda kutoa shukrani kwa wapiga kura kupata wanachama zaidihasa vijana na kampeni ya kuchukuA NCHI 2015 ZIANZE SASA MSISUBIRI MPAKA WAKATI WA UCHAGUZI.

    MMETUFURAHISHA TUMEWAPENDA

    ReplyDelete
  7. Hongera kwa wote walioshinda. lakini naomba watanzania tuamke na kuacha kuitegemea serikali kuondoa umaskini wetu kama tabia zetu za uvivu zitabaki pale pale. Nina imani kubwa kuwa watanzania wengi wanaojituma au walioweka uvivu pembeni na kutoshinda vibao vya kujadili mechi za soka au kunywa pombe siyo masikini. Ardhi nzuri na maji mengi tunayo kwanini watu wengi hawajitumi kulima kwa bidii na kuuza ziada nchi za jirani kama kenya ambako chakula ni haba.By kalenga Boy

    ReplyDelete
  8. hakika Slaa ni dume, ahsante baba tunakuaminia . hawa mafisadi tumechoka nao. Nawapa hongera sana Wapinzani kwa kazi mlioionyesha.Washenzi hawa CCM, Wamejaa vizee hawataki kuachia ngazi, Wapinzani hoyeeee, CCM ni Mafisadi wantakiwa kulazwa barabarani na kuchapwa viboko na kila mwananchi, na huyu Kikwete na Serikali yake wanafuja sana mali ya walala hoi, ni kuwango<oa madarakani, nashangaa watu wanaendelea kumpa kura, WATANZANIA BADILIKENI ACHENI UWOGA!

    ReplyDelete
  9. “UTAJIRI unaotokana na wizi wa mali ya umma, na wizi wa fedha za kigeni na unyonyaji na uharamia wa aina mbalimbali, hautupunguzii umaskini wetu, bali unauongeza. Chama chetu hakiwezi kuikubali hali hii, na kikaendelea kuwa CCM, na wala kisitazamie kuwa wananchi wataendelea kukikubali” (Mwalimu Nyerere, Oktoba 1987).

    Mungu Ibariki Tanzania yetu. Mungu tupe nguvu ya kuendelea kupambana na Mafisadi waliokumbatiwa na CCM !

    ReplyDelete
  10. Live long Dr. Slaa
    Do not slow down. WE WILL GET THERE. The whole Tanzania is behind you, except for the few ignorants na a little group ya Mafisadi!
    WE SUPPORT YOU DR.God bless Tanzania.

    ReplyDelete
  11. Hongera Dr. SLAA Umebadilisha fikra za Watanzania waliowengi na kuiweka Tanzania katika hali ya vuguvugu la ukombozi mpya usikate tamaa jipangeni upya wote kuendeleza ukombozi. Tanzania bila CCM INAWEZEKANA

    ReplyDelete
  12. CCM wasituhadae na amani. Amani haiwezi kuwapo bila kutenda haki. Kwanini amani ya Tanzania itegemee ukondoo na si kutenda haki? Hata Kikwete na waramba viatu wake wanajua hakushinda kihalali bali kwa kutegemea uchakachuaji na upuuzi mwingine utokanao na jinai ya kuiba. Ni ushindi wa aibu na pigo kwa taifa hasa wale wanaochukia ufisadi ambao Kikwete anaulinda kwa vile ulimuingiza madarakani. Slaa shikilia msimamo maana hakuna wa kukufanya kitu. Wanaogopa kunyea debe The Hague.

    ReplyDelete
  13. Katiba mpya ni lazima ili Tanzania iweze kuendelea. Inafaa katiba ibadilishwe tuwe na utawala wa majimbo na pia mawaziri wasitokane na wabunge. Mbunge akiwa waziri anabanwa sana na shughuli nyingi na hawezi kutimiza kamwe wajibu wake ipasavyo kwa wananchi wake. Kwanza tuangalia mikono mitatu ya serikali:

    1. Executive
    2. Legislature
    3. Judiciary

    Ikiwa mbunge (ambaye yupo kwenye legislature) atateuliwa kuwa waziri ( Executive, kama ilivyo katika katiba yetu ya sasa), atakuwa anawatumikia mabwana wawili na kamwe kazi zake hatazitekeleza kwa ufanisi mkubwa.

    Kazi kubwa ya Bunge ni kuhakikisha kuwa inaibana Executive kutimiza wajibu wake kwa wananchi. Hivyo Mbunge ni kiungo muhimu kati ya serikali na wananchi wake. Haifai huyo huyo Mbunge kuwa tena ndani ya Executive!

    ReplyDelete