12 November 2010

Kashfa zamponza kipa Dalei wa China.

GUANGZHOU, China

KIPA wa China, Wang Dalei ambaye aliwatukana mashabiki kwa kuwaita wanaharamu na kundi la mbwa, ameomba radhi na amesimamishwa katika timu ya
taifa.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 21, amekuwa akitajwa kutakiwa na timu za Ulaya kama Inter Milan na Manchester City, alilaumiwa kwa kushindwa kuokoa goli katika mechi dhidi ya Japan iliyochezwa Jumatatu.

Mahasimu wa China, Japan katika mechi hiyo ya michezo ya Asia waliibuka na ushindi wa mabao 3-0, kitu kilichofanya mashabiki na vyombo vya habari kuilamu timu na kipa huyo.

Mchambuzi mmoja wa soka katika televisheni alimwelezea kipa
kwa kumlinganisha na mchezaji wa mpira wa wavu.

"Ninaomba radhi kwa mashabiki na vyombo vya habari kwa nchi nzima kwa lugha yangu mbaya, ambayo iliharibu sura ya timu ya soka ya taifa, michezo na China," alisema Wang.

"Ni makosa yangu. Ninatumaini kuwa mtanisamehe na kunipatia nafasi nyingine, alisema na kuongeza ninatumaini kuwa sitafanya kosa lingine kwa siku za baadaye."

Katibu Mkuu wa Michezo wa Asia, Cai Jiadong, alisema Wang amesimamishwa kuchezea timu ya China na kutakiwa kujirekebisha, limesema gazeti la Serikali la Xinhua.

"Wang alikiri kuwa kitendo hicho hakikuwa cha kiuanamichezo, kimeumiza hisia za mashabiki wa China akiwa kama mchezaji wa timu ya taifa," alisema Cai.

Hakusema mchezaji huyo atafungiwa mechi ngapi, hakucheza katika mechi ambayo China ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Kyrgyzstan.

No comments:

Post a Comment