03 November 2010

China yakataa pendekezo la Marekani.

HANOI,vietnam

CHINA imekataa pendekezo la Marekani kuandaa mazungumzo ya nchi tatu na Japan kuutanzua mzozo unaozunguka umiliki wa visiwa kadhaa katika bahari ya
Mashariki ya China.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China alisema jana kuwa mzozo huo unapaswa kutatuliwa na nchini hizo mbili bila kushirikisha Marekani.

Wazo hilo lilitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Bi Hillary Clinton wakati wa mkutano wa viongozi wa serikali za nchi wanachama wa Muungano wa Mataifa ya Mashiriki mwa Bara Asia uliofanyika Vietnam.

Lakini baada ya kutolewa wazo hilo,waziri huyo wa Mambo ya Nje alisema kwamba hakuna haja ya kuishirikisha Marekani kutokana na kuwa wao wana uwezo wa kukaa pamoja na kujadiliana kuhusu jambo hilo.

Uhasama kati ya China na Japan umeongezeka tangu wanamaji wa Japan walipomkamata nahodha wa meli moja ya uvuvi karibu na visiwa hivyo mwezi Septemba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment