Na Mwandishi Maalumu
VIONGOZI na Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika- SADC wamemaliza kikao chao cha siku moja mjini Gaborone Botswana
juzi ambapo
walizungumzia masuala mbalimbali yanayohusu Jumuiya hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal ambaye alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika mkutano huo ambao ulitanguliwa na
sherehe za uzinduzi wa Makao Makuu ya Jumuiya hiyo alirejea nyumbani jana.
Katibu Mkuu wa SADC, Dkt. Tomaz Augusto Salomao aliwaambia waandishi wa habari baada ya mkutano huo mjini hapa kuwa viongozi hao wamewaagiza mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Jumuiya hiyo kukamilisha taarifa juu ya ushirikiano kati ya Umoja wa Afrika-AU na Jumuiya za kikanda (ikiwemo SADC) hususan katika suala la namna maamuzi yanavyopitishwa na kutekelezwa katika vikao vya Umoja huo wa Afrika.
Kwa mujibu wa Dkt. Salomao kikao cha viongozi wa SADC kilichofanyika mjini Windhoek, Namibia Agosti mwaka huu kilieleza haja ya kufanyika kikao maalumu cha
kuzungumzia suala la hilo baada ya kutafakari matukio kadhaa yanayohusiana na maamuzi yanavyofanyika ndani ya vikao vya AU.
“Wameona (viongozi wa SADC) mambo hayaendi vizuri…maamuzi mengine hayafuati utaratibu na miongozo ya Umoja huo hivyo wamewataka mawaziri wa Mambo ya Nje wa SADC
wakamilishe taarifa yao haraka ili iwasilishwe katika kikao kijacho cha AU kitakachofanyika mjini Adis Ababa,” alibainisha Dkt. Salomao.
Wakuu hao pioa walipokea taarifa juu ya uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika tarehe 31 Oktoba ambapo Jumuiya hiyo
ilipeleka timu ya waangalizi 97.
Taarifa ya awali ya Timu ya waangalizi hao ilieleza kuwa
uchaguzi huo ulifanyika kwa uhuru, haki na kwa utulivu na kwamba SADC imempongeza Rais Kikwete kwa uchaguliwa tena kuiongoza Tanzania na kuwapongeza wananchi wa
Tanzania kwa kufanya uchaguzi kwa amani na utulivu.
Kaka yako aliitwa Vasco Da Gama...wewe tukuitaje? Mmeanza hivyo?! Waone kwanza...
ReplyDelete