Na Joseph Mwambije,Songea
Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Dkt. Emmanuel Nchimbi amewashukuru wananchi wa Jimbo la Songea kwa kumchagua kuwa mbunge wao na ameahidi kushirikiana nao
kuwaletea maendeleo.
Alitoa shukrani hizo hivi karibuni wakati akizungumza na wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi kwenye uwanja wa Majimaji.
Alisema hatawaangusha, atawatumikia na kutekeleza ahadi alizoahidikama zilivyoainishwa kwenye ilani ya Chama cha mapinduzi hivyo wategemee maendeleo katika jimbo la Songea Mjini.
"Nawashukuru kwa moyo wa dhati kwa kunichagua kuwa mbunge wenu, mmenipa heshima kubwa kunichagua kwa kura nyingi, nawaahidi kuwa sitawaangusha lakini ili niweze kutimiza yale niliyowaahidi nahitaji ushirikiano wenu," alisema Mbunge huyo.
Alisema katika kipindi chake cha miaka mitano iliyopita amejitahidi kuwalete wananchi wake maendeleo na kuwajengea sekondari kwa kila kata na kujenga barabara za katikati ya mji kwa kiwango cha lami.
No comments:
Post a Comment