11 November 2010

Asamoah Gyan azidi kutakata Sunderland.

LONDON, England

MSHAMBULIAJI Asamoah Gyan, juzi aliibuka shujaa baada ya kuisawazishia bao timu yake ya Sunderland na kuifanya kwenda sare ya bao 1-1 dhidi ya Tottenham
, katika michuano ya Ligi Kuu ya England.

Katika mechi hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa White Hart, Gyan alioneka shujaa baada ya kusawazisha bao lililofungwa kipindi cha kwanza na Rafael van der Vaart na kuipokonya pointi moja Tottenham Spurs.

Kabla ya bao hilo, Spurs awali walionekana kuwa wangeondoka na ushindi ambapo katika kipindi cha kwanza Tom Huddlestone, aliachia mkwaju akiwa umbali wa yadi 25 lakini shuti lake likagonga mwamba.

Bao la timu hiyo lilipatikana baada ya Gareth Bale kuachia krosi kutoka upande wa kushoto na Peter Crouch, akaurejesha mpira nyuma kwa Van der Vaart, ambaye aliutuliza kabla ya kuukwamisha kimiani.

Baada ya bao hilo, Sunderland walikuja juu na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha kutokana na Gyan, kutumia makosa ya mabeki kushindwa kuondosha mpira langoni mwao na kumfanya mfungaji huyo kufunga bao hilo kirahisi.

No comments:

Post a Comment