29 October 2010

ZEC yawaondoa wasiwasi waangalizi.

Na Mwajuma Juma, Zanzibar

TUME ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), imewaondoa wasiwasi waangalizi wa uchaguzi juu ya baadhi ya kasoro wanazoziona katika hatua hii ya kuelekea upigaji kura
Jumapili.

Akizungumza na waangalizi kutoka taasisi za ndani na za kimataifa jana, Mwenyekiti wa Tume hiyo Bw. Khatib Mwinyichande alitoa jibu hilo baada ya waangalizi kumuuliza majukumu ya baadhi ya viongozi wa serikali na masheha katika mchakato wa shughuli za uchaguzi.

Baadhi ya maswali ya waangalizi hao yaliyoomba ufafanuzi juu ya msuala mbali mbali ya zoezi la uchaguzi yaligusa jukumu la wakuu wa mikoa, masheha na ukosefu wa mjumbe wa Mahakama Kuu katika ZEC.

Mwinchande alifafanua kwamba wakuu wa mikoa na masheha hawana jukumu lolote katika suala la uchaguzi juu ya upigaji na kuhesabu kura.

“ZEC inafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria bila ya kuingiliwa na mtu yeyote, na hawa wakuu wa mikoa na masheha hawana jukumu lolote kuhusu uchaguzi wala uhesabuji wa kura,” alisema.

1 comment:

  1. Ikiwa masheha (na wakuu wa mikoa) hawana jukumu lolote katika shughuli za uchaguzi, inakuwaje wao ndio wanaoamua nani aandikishwe, nani asiandikishwe? Wadanganyeni haohao wageni ambao haelewi kinachoendele, lakini sisi tunoonja joto ya jiwe msitudanganye.

    ReplyDelete