28 October 2010

Yanga kumlipa Njoroge kwa awamu.

 Na Addolph Bruno

BAADA ya mchezaji Steven Marashi kulipwa Sh. Milion 1.5 kwa awamu, Uongozi wa Klabu ya Yanga sasa unatarajia kumlipa Mkenya John Njoroge, baada ya kuzungumza naye na
kukubali kulegeza masharti alipwe kwa awamu.

Marashi na Njoroge ni miongoni mwa wachezaji  wanaoidai Yanga kutokana na kuvunjiwa mikataba yao na klabu hiyo msimu uliopita wakiwemo Ali Msigwa na Wisdom Ndlovu raia wa Malawi.

Hata hivyo uongozi wa Yanga, awali ulitaka kupiga chenga kulipa deni hilo, lakini wachezaji hao walifikisha suala hilo kwenye Kamati ya Mashindano na Haki za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Lloyd Nchunga alisema Marashi alikuwa mchezaji wa kwanza kukubali kulipwa kwa awamu na hadi sasa ameshpewa Sh. milioni 1.5.

Alisema baada ya mchezaji huyo kuanza kulipwa, Njoroge naye alikutana na uongozi hivi karibuni na kuzungumzia ambapo amelegeza masharti ya
kutaka kuanza kulipwa kwa awamu.

"Tumefanya mazungumzo na Njoroge, naye amekubali kupunguza fedha kubwa aliyokuwa anataka kulipwa kama wenzake, ambazo zilizidi kiwango sasa tutaanza kumlipa wakati wowote na yeye amekubali," alisema.

Nchunga alisema wachezaji wengine Msigwa na Ndlovu, hawajafanya mazungumzo nao kuhusu suala hilo na kuongeza kuwa kama bado wanashikilia msimamo wao wa kutaka kulipwa fedha nyingi, hawatakuwa tayari kuwalipa.

No comments:

Post a Comment