Na Addolph Bruno
BAADA ya kuahirishwa mara mbili kwa sababu mbalimbali hatimaye Chama Cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BD), kimeruhusiwa kufanya Uchaguzi Mkuu wa
viongozi ambao sasa utafanyika Desemba 18, mwaka huu.
Awali uchaguzi huo, ulitarajiwa kufanyika machi mwaka huu, lakini uliahirishwa kutokana Ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam ambayo ndiyo inaunda Kamati ya Usimamizi ya uchaguzi huo
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa BD, Mbaga Mwamboma alisema baada ya majadiliano na Ofisi ya Mkoa sasa wamekubaliana kufanya uchaguzi, baada ya Uchaguzi Mkuu wa taifa.
"lakini pia lingine lililotuchelewesha ni kwamba idadi ya wadau waliojitokeza kuchukua fomu, ilikuwa hairidhishi, kwani ni watu sita pekee ndiyo walichukua fomu kwa nafasi mbalimbali, kwa hiyo nacho kilikuwa kikwazo na sasa tunaendelea kutoa fomu," alisema Mwamboma.
Mwamboma alisema nafsi zitakazowaniwa katika uchaguzi huo ni za Rais wa, Makamu wa Rais, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mhazini, na Wajumbe wa Kamati.
Mbali na hilo, Mwamboma alisema Ligi ya Mkoa daraja la pili, inatarajiwa kuanza Novemba 6, mwaka huu ambapo timu mbalimbali zipo katika maandalizi.
No comments:
Post a Comment