28 October 2010

Soka la Uingereza si chohote

LONDON, Uingereza

IMEDHIRIKA kwamba soka la Uingereza si chochote.
Katika kikosi wachezaji 23 wa England kinachonolewa na kocha Fabio Capello, waliocheza Kombe la Dunia hakuna hata mchezaji mmoja aliyeteuliwa katika orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia wa Mwaka.

Hii ni mara ya kwanza kabisa, kwamba soka ya Uingereza imeshindwa kutoa mtu anayeshindania tuzo hiyo ya heshima zaidi katika soka.

Na wakati Mtendaji Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu England (FA), Richard Scudamore amekuwa akisifia ubora wa Ligi Kuu ya nchi hiyo, lakini ni wachezaji watatu tu wa kigeni wameteuliwa kuwemo kwenye orodha ya wanaowania ambao ni
Didier Drogba wa Chelsea, Cesc Fabregas wa Arsenal na Asamoah Gyan wa Sunderland.

Capello ambaye ni kocha anayelipwa mshahara mkubwa zaidi duniani wa pauni milioni 6 kwa mwaka, ameshindwa kutoa hata mchezaji mmoja na pia mwenyewe kutokuwemo kwenye orodha ya wanaowania tuzo ya kocha bora wa mwaka.

Hata Wayne Rooney, ambaye amesaini mkataba mpya utakaofanya kulipwa pauni 250,000 kwa wiki katika klabu ya Manchester United na kuwa mchezaji mwenye mshara kubwa zaidi duniani, hayumo kwenye orodha hiyo.

Rooney awali alikuwa akitajwa mara kwa mara kuwania tuzo hiyo, sambamba na wachezaji wenzake wa England, Frank Lampard, Steven Gerrard na John Terry.

England hawakufanya vizuri sana katika fainali za Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini, safari hii wamepuuzwa.

Katika orodha ya wanaowania tuzo hiyo, Ujerumani iliyoifunga Uingereza mabao 4-1 imetoa wachezaji watano.

Hispania ina wachezaji 11, wanaowania tuzo hiyo na watano wa timu ya mabingwa wa Ulaya Inter Milan.

Orodha kamili ya wachezaji wanaowania tuzo hiyo ya FIFA ya Mchezaji Bora wa Dunia wa Mwaka:
X Alonso (Hispania), D Alves (Brazil), I Casillas (Hispania), D Drogba (Ivory Cost), S Eto'o (Cammeroon), Fabregas C (Hispania)), D Forlani (Uruguay), A Gyan (Ghana).

Wengine ni A Iniesta (Hispania), Julio Cesar (Brazil), M Klose (Ujerumani), P Lahm (Ujerumani), Maicon (Brazil), L Messi (Argentina), T Mueller (Ujerumani), M Ozil (Ujerumani), C Puyol (Hispania), A Robben (Uholanzi), C Ronaldo (Ureno), B Schweinsteiger (Ujerumani), W Sneijder (Uholanzi), D Villa (Hispania), Xavi (Hispania).

Wanaowania tuzo ya Kocha bora wa mwaka ni:
C. Ancelotti (Chelsea), V. del Bosque (Hispania), A. Ferguson (Man U), P Guardiola (Barcelona), J. Loew (Ujerumani), J.  Mourinho (Inter/ Real Madrid), O. Tabarez (Uruguay), L van Gaal (B Munich), B van Marwijk (Uholanzi), A Wenger (Arsenal).

No comments:

Post a Comment