29 October 2010

Slaa apagawisha mikoa mitatu.

Na Waandishi Wetu

MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa jana alipata mapokezi makubwa katika mkutano yake mitatu iliyofanyika
katika mikoa minne tofauti ikiwa ni harakati zake za kukamilisha kampeni zake kuwania kiti hicho.

Harakati zake jana zilianzia katika Jimbo la Kigomboni, Dar es Salaam alipohutubia katika viwanja vya Mbagala Zakhem jana asubuhi kabla ya kwenda kuhutubia mkutano mwingine mkoani Morogoro, uliofanyika katika Uwanja wa Saba Saba, Jimbo la Morogoro Kusini.

Baadaye alihamia mkoani Dodoma alipohutubia mkutano mkubwa katika Uwanja wa Barafu ambao unaelezwa kuwa haujapata kutokea katika kipindi hiki cha kampeni kianze zaidi ya miezi miwili iliyopita. Baadaye mgombea huyo alipanga kumalizia kazi yake mjini Iringa, ambako alichelewa na mkutano kuahirishwa.

Akiwa Mbagala, Dkt. Slaa aliitaka Jeshi la Polisi nchini kufuatilia taarifa alizozipata kuwa kuna wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaotaka kukichafua chama chake kwa kufanya fujo siku ya uchaguzi huku wakiwa wameshika mabango ya chama chake.

Alisema kuwa watu hao wamedhamiria kuichafua Chadema ili ijulikane kuwa wanafanya fujo jambo ambalo halina ukweli.

"Nataka jeshi la polisi kufanyia kazi taarifa hii,kuna watu wa CCM wanapanga kutumia mabango na bendera za CHADEMA siku ya uchaguzi kufanya fujo ili wajulikane wanafanya fujo watu wa CHADEMA," alisema.

Pia alisema CHADEMA haibabaishwi na kauli za kuitwa wao majuha au wapuuzi kwa kuwa wao wanasimamia ukweli siku zote.

Alisema anashangaa wao kuitwa wapuuzi wakati mgombea urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa katika moja ya mikutano katika Jimbo la Bagamoyo anakozaliwa alisomewa taarifa ya ujenzi wa matundu manne ya vyoo katika shule tano za singi tano kwa sh. milioni 700 kila shule na kuridhika.

Alizitaja shule hiizo ni Mbaruku, Kilomo, Kihalaka, Kongo na Visegese ambazo kila moja ilijengewa choo chenye matundu manne.

Alipohutubia mkoani Morogoro na Dodoma aliitaka CCM ikae pembeni kumpisha aongoze nchi kwani chama hicho kimeishiwa uwezo wa kubuni na kutekeleza sera zinazolenga ukombozi wa wananchi wa kawaida ndio maana imeamuua kuiga sera ya elimu ya lazima kuwa ni
kuanzia chekechea hadi sekondari.

“Kama CCM kinaweza kuiga na kutekeleza sera na mikakati ya chama cheti kama vile elimu bure hadi sekondari na ujenzi wa chuo kikuu mkoani Dodoma, zahanati kila kijiji, kwanini sasa wasitupishe sisi tuongoze na kutekeleza sera zetu kwa ufaniisi zaidi,” alisema Dkt. Slaa.

Akihutubia mkutano wa kammpeni  jana, Dkt. Slaa alisema kauli ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe kuwa elimu ya lazima na bure itakuwa kuanzia chekechea hadi kidato cha nne ni ushahidi wa sera anayonadi tangu mwanzo wa kampeni zake inawezekana.

Alisema kauli hiyo ya Profesa Maghembe aliyoitoa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wilayani Mwanga kimedhihirisha unafiki wa viongozi wa CCM na serikali yake waliokaririwa wakidai elimu bure haiwezekani.

“Kitendo cha CCM na viongozi wake akiwemo mgombea wao wa urais rafiki yangu JK (Rais Jakaya Kikwete), meneja wa kampeni Bw. Abdulrahaman Kinana na wengine wengi wamekaririwa wakisema kutoa elimu bure haiwezekani.

Lakini leo hii Waziri wa Elimu kwenye serikali hiyo
hiyo anajitokeza wazi na kusema inawezeka ni ishara ya kutosha kuwa sera hiyo inateekelezeka,” alisema Dkt. Slaa.

Alitaja sera na mikakati mingine iliyobuniwa na chama chake na baadaye kuigwa na kuuanza kutekelezwa na CCM kkuwa ni ujenzi wa chuo kikuu mkoani Dodoma na zahanati kila kijiji ambayo imewekwa kwenye ilani ya chama hicho tawala ya mwaka huu.

Akifafanua alisema katika Uchaguzi Mkuu uliopita mwaka 2005 CHADEMA ilitangaza kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa sehemu maalumu kwa ajili ya ujenzi wa taasisi za elimu ya juu (Jiji la Elimu) lakini baada ya uchaguzi CCM iliiga sera hiyo na kuamuua kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na kujivunia jambo hilo akisema lina manufaa kwa umma ya Watanzania.

Alisema hata sera ya kujenga zahanati kila kijiji CCM iliiga kutoka katika mpango wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu inayoongozwa na CHADEMA tangu mwaka 1995.

Katika hatua nyingine, mchumba wa Dkt. Slaa, Bi. Josephine Mshumbusi alimtupia kombora mke wa Rais Jakaya Kikwete akimshauri kutulia nyumbani na kumshauri mumewe aache kupuuza kero na maendeleo ya wananchi kwani Mungu wa Watanzania yuko hai na atawatetea dhidi ya uovu na udhalimu wa viongozi.

“Namshauri rafiki na mama yangu Salma Kikwete leo jioni akirejea nyumbani amshauri mumewe Rais Kikwete asifanye mchezo na maisha ya Watanzania kwani Mungu wao yu hai atawatetea,” alisema Bi. Mshumbusi.

Akiwa Dodoma, Dkt. Slaa alisisitiza mpango wake wa kuufanya mji huo 'University City' (Jiji la Elimu) ili kuuendeleza badala ya mpango wa CCM wa miaka 40 wa kuhamishia makao makuu ya nchi, usiotekelezeka.

Dkt. Slaa anayetarajiwa kuhitimisha kampeni zake kesho mjini Mbeya leo anaendelea mikutano mikoa ya Iringa na Ruvuma ambako chama hicho kina matumaini ya kupata kura nyingi katika ngazi ya ubunge na urais.

No comments:

Post a Comment