KIGALI,Rwanda
SERIKALI ya Rwanda imemshutumu meneja wa "Hotel Rwanda" kwa kufadhili kundi moja la waasi nchini humo. Bw.Paul Rusesabagina alijipatia jina ndani na nje ya nchi hiyo kupitia filamu iitwayo Hotel Rwanda ambayo inamuonesha akifanya jitihada za kuwaokoa mamia ya Watutsi kwa kuwahifadhi ndani ya hoteli yake wakati wa mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 kwa sasa hali inaonekana kumwendea kombo baada ya kujikuta akishutumiwa kwa kashfa hiyo.
Habri kutoka mjini Kigali zilieleza jana kuwa
Mwendesha Mashataka Mkuu anamshutumu meneja huyo kwa kuwatumia ferdha makanda wawaili wa zamani wa makundi ya waasi ingwa Rusesabagina anakana madai hayo akisema kuwa hizo ni kampeni za kutaka kumchafua.
Ilielezwa kuwa Mwendesha mashtaka Mkuu huyo wa Rwanda,Bw. Martin Ngoga,alisema juzi kuwa Bw. Rusesabagina anafadhili kile alichokiita shughuli za kigaidi nchini Rwanda kwa kutoa fedha kwa makamanda wa kikundi cha FDLR.
Mbali na kufadhili kundi hilo,Mwendesha Mashtaka huyo anamshutumu Bw.Rusesabagina,ambaye kwa sasa anaishi uhamishoni kwa kushirikiana na kiongozi mkuu wa upinzani, Bi.Victoire Ingabire ambaye alikamatwa wiki iliyopita na anashutumiwa kwa kufanya shughuli zake na makundi ya magaidi mashtaka ambayo anayakana.
Mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC alisema kuwa hivi karibuni,Bw. Rusesabagina amewahi kuishutumu Serikali ya Rais Paul Kagame, ambaye ameshakumbana na shutuma kutoka maeneo mbalimbali akidaiwa kuwakandamiza wapinzani.
Katika mahojiano na BBC,Bw. Rusesabagina aliishutumu Serikali ya Rwanza kwa kuanzisha kampeni chafu dhidi yake.
"Ni hatua mpya katika kampeni dhidi yangu zinazofanywa na Serikali ya Rwanda na yakiwemo mashambulizi kutoka kwa rais mwenyewe,ni uongo na unyanyasaji,"alisema katika mahojiano hayo.
"Mimi siyo mtu wa fujo lakini kila mtu atakayempinga Kagame anachukuliwa katika usumbufu kama huu,"aliongeza.
Hata hivyo hakuna mashtaka rasmi yaliyofunguliwa dhidi ya Bw. Rusesabagina.(BBC)
No comments:
Post a Comment