01 November 2010

Mchuano Mkali.

Na Waandishi Wetu.

MATOKEO ya awali ya Uchaguzi Mkuu yaliyoanza kutolewa jana jioni baada ya kura kuhesabiwa na kubandikwa vituoni yalionesha mpambano mkali baina ya
vyama vya CCM na CHADEMA na CUF ikifuatia kwa ngazi zote, urais, ubunge na udiwani.

Katika vituo vya wilaya ya Temeke, CCM imeonesha umwamba na kushikilia vizuri ngome yake. Katika Kituo cha Weno, kata ya Weno CCM ilipata kura za urais 82, CHADEMA (42), CUF (18), APPT 1 na NCCR 1. Ubunge CCM iliibuka na kura 68, CHADEMA 36 na CUF 34. Wakati udiwani CCM ilipaya 64, CHADEMA 31, CUF 31 na TLP 2.

Katika kituo cha Polisi Post CCM ilipata kura za urais 79, ubunge 86 na 82 za udiwani; CHADEMA 42 za urais, 33 za ubunge na 35 za udiwani wakati CUF ilipata 21 za urais, 18 za ubunge na 21 za udiwani. TLP ilipaya kura 2 za ubunge.

Kwenye kituo cha Garden kata ya Miburani CCM ilinyakua kura 85, za ubunge 76 na udiwani 76; CHADEMA 20 za urais, 18 za ubunge na 16 za udiwani; CUF iliambulia 15 za urais, 23 za ubunge na 22 za udiwani. TLP iliambulia kura 1 ya ubunge na moja ya udiwani.

Katika Jimbo la Segerea Wilaya ya Ilala, Kituo cha Minazi Mirefu B (5), mgombea urais wa CCM alipata kura 22, CHADEMA 67, CUF 08; Ubunge Chadema 67 na CCM 57.

Kituo cha Minazi Mirefu B 1, CCM ilipata kura za urais 65, CHADEMA 82 na CUF 3; Kituo cha Minazi Mirefu B2 Mgombea urais wa CCM 51, CHADEMA 83 na CUF 3, Kwa ubunge CCM 48 CHADEMA 82 na CUF 5.

Minazi Mirefu A5 Urais CCM 75, CHADEMA 75; Minazi Mirefu A CHADEMA 88 na CCM 82.

Jimbo la Kinondoni, Kata ya Mwananyamala Kisiwani, Kituo Shule ya Msingi Kisiwani C2 Urais: CCM 74, Chadema 3, CUF 39; Ubunge CCM 76 CHADEMA 30 na CUF 37 na Udiwani CCM 61 CHADEMA 20 na CUF 62.

Kisiwani B4 urais CCM 82, CHADEMA 35 na CUF 47; ubunge CCM 82, CHADEMA 25, CUF 55, DP 7. Udiwani CCM 66, CHADEMA 13 na CUF 86.

Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, Picha ya Ndege 1 urais CCM 86 CHADEMA 112; ubunge CCM 83 CHADEMA 113 UPDP 1, DP 1; Visiga urais CCM 113, CHADEMA 33 CUF 9; ubunge CCM 106, CHADEMA 33, CUF 9, SAU 1 na DP 1.

Kibaha Sekondari urais CCM 46, CHADEMA 96, CUF 1 Ubunge CCM 43 CHADEMA 97, CUF 2 na DP 1.

Hadi tunakwenda mitamboni matokeo ya awali yalikuwa yanaendelea kumiminika.
Imeandaliwa na Zamzam Abdul, Grace Michael, Rabia Bakari, Peter Mwenda na Yusuf Katimba

2 comments:

  1. CCM itashinda kwa upande wa raisi lakini hali ya bunge letu tukufu itabadilika. Lamsingi ni kuwa sasa CCM inaelewa wazi kuwa hii ni karne ya 21 na siasa za uzushi na ahadi zisizotekelezeka waache na halizileti maendeleo kwa mtanzania.

    Mabadiliko makubwa yanaweza yasionekane sasa lakini mwaka 2015 itakuwa ni mwaka wa mabadiliko makuu kwa nchi yetu.

    Upinzani uungane na kuwa na sauti moja yenye nguvu ili kuingoa kabisa CCM katika uongozi wa nchi yetu. Kwani uharibifu uliofanywa na CCM hauwezi kurekebishwa na CCM.

    Nguvu ya Umma iko mkononi mwa umma na sio sera za CCM.

    Wananchi hongereni sana kwa uchanguzi wa amani na utekelezaji mwema wa haki yenu ya kuchangua viongozi watakaofaa kuleta maendeleo na usio umasikini.

    ReplyDelete
  2. Wananchi Tukifuatlia Exit Polls Chadema Imeshinda Huu Uchanguzi. Yes Tulijua CUF wangeweza Kupata Viti Visiwani lakini Bara CUF Haina Support Hivyo na NEC na CCM Wanachanganya Kura na Kuzigawa Kama Pipi za Watoto. Wameshatufanya Wabara ni Wajinga Sikunyingi Kwa Sababu Hakuna Jambo Zaidi Lilishatokea Kuwatishia. Hii Ndio Inawapa Jeuri Lowasa, Chenge na Hawa Mafisadi. This time we have to Do Iit Right. Hakuna Nafasi Nyingine na Muda wa Kuumizwa Tena. Watanzania Wenzangu:
    I. Tufanye Mikakate ya Kuzunguka Vituo na Kuhesabu Kura na Kuhakisha Hizo Kura Hata Zile Zilizotangazwa Ziko Sawa. Wao Wanatumia Computer Casino na Sisi Tutumie Transparency. Tunajua Kura Zipo Miji Mikubwa na Ndio Maana Uoni Wanatangaza Haraka Haraka. Dar Inaongoza Kuwa na Mamilioni ya Wananchi na Ndio Raisi Atatoka. Miji Hii ni Muhimu: Moro, Mbeya, Iringa, Arusha, Mwanza, Mara, Kigoma, Moshi, Sumbawanga, Singida, Musoma, Shinyanga na Tanga. Angalia Strategies za Utangazaji Utaona Pattern za Kumpa Kikwete early lead ili Wananchi Waamini Kashinda. This is Bogus, Tanzanians are not fools no more.
    II. Mafunzo Kutoka Kenya, Uganda, Rwanda na Zimbabwe: Tufuate Wenzetu, Wakenya Walikataa Kukaa Nyumbani na Kuonewa na Leo Matunda Yake Tunaona New Constitution na Solutions ya Matatizo Yao Yanatokea. Zimbabwe, Mugabe Kalazimika Kuongoza Nchi na Waziri Mkuu Kutoka Upinzani. Tanzania Tusipoangalia Tutakuwa Kama Iran na Huko North Korea Kwamba Hatuna Haki Tena. Akiondoka Kikwete Atakuja Kiongozi worse than this na Itakuwa Ngumu Kumwondoa. Mabadiliko Yanahitajika Kila Mahali: Kiuchumi, Elimu, Afya, Ardhi na Vita vya Wizi wa Pesa za Serikali. Haya Hayatafanyika Bila Hizi Kura Kuwa za Wazi. Hata Wazanzibari Wanatucheka, Walikataa Kuonewa na sasa CCM Inawaogopa. CUF Walijua Watapewa Uwaziri Mkuu Ndio Maana Wamekubali Matokeo Kiraisi na Matakwa Yao Watatimiziwa. Hakuna Mtanzania Mwenye Imani na NEC na CCM, Tunahitaji New Constitution to Address These Issues.
    "Dr Luther King na Mandela Walitumia Peaceful Means na Leo Hii Tunaona Matunda Kila Mahali, Tumieni Hivyo Vituo na Kura Zetu Ndipo Maendelo Yetu Yalipo! Kwenye Hayo Masanduku ya Kura"

    ReplyDelete