Na Said Njuki, Arusha
WAKATI Wadau wa madini ya tanzanite wakijifariji na kufungwa kwa usafirishai madini ghafi nje, serikali imekuwa ikipoteza mabilioni ya fedha kutokana na udhibiti
mbovu wa bidhaa hiyo adimu duniani.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili na kuthibitishwa
na baadhi ya wadau hao umebaini kuwepo kwa idadi kubwa ya wafanyabiashara wa madini ya tanzanite jijini Arusha wanaoruhusu leseni moja kutumika kwa wageni wanaokuja
kununua madini hayo.
Hali hiyo imedaiwa kukithiri hasa wakati huu ambapo serikali
ipo katika utekelezaji wa amri ya kuhakikisha tanzanite ghafi inayozidi gramu moja haitoki nje ikiwa aghafi, huku yakiwepo madai kuwa wafanyabiashara hao wa ndani wanakingiwa kifua na vigogo kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
Leseni ya biashara ya madini ya vito kwa mgeni ni dola
za Marekani 250, hata hivyo bado wafanyabiashara hao hawanunui leseni hizo, na badala yake hutumia leseni za wafanyabiashara wa ndani ili kukwepa kodi mbalimbali zikiwemo mapato.
Habari zaidi zinaeleza kuwa wapo wafanyabiashara wanaoazimisha ofisi zao za kununulia madini hayo kwa wageni na kununua madini hayo moja kwa moja kutoka kwa mchimbaji wadogo, badala ya biashara kufanywa kati ya mgeni na mfanyabiashara wa ndani, hali inayolipotezea taifa mabilioni ya fedha.
Kutokana na hali hiyo, wadau wa madini wanadai kuwa serikali
inapoteza fedha nyingi kwani kodi pekee inayolipwa na wageni hao ni mrahaba kutoka kwa kampuni hizo (majina tunayo), huku idadi kubwa ya madini hayo ikisafirishwa kwa njia za panya kupitia Zanzibar na Nairobi Kenya kwa lengo la kukwepa kodi ya
serikali.
“Sasa wafanyabiashara wa ndani wanashindwa kupata madini ya kutosha kwani mfanyabiashara anayepaswa kununua madini hayo ofisini kwako, leo anakuwa mshindani wako katika ununuzi kutoka kwa wachimbaji na kwa kuwa hana gharama za kulipia ofisi na kodi nyingine mbali na mrahaba anaotoa wakati wa kufanya mauzo ya nje,†kilibanisha moja ya vyanzo vyetu vya habari.
Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kaskazini, Bw. Benjamin
Mchwampaka alipotakiwa kuzungumzia suala hili alisema hajui kama tabia hiyo ipo na kuahidi kulifanyia kazi iwapo atapata uhakika na majina ya kampuni zinazohusika.
No comments:
Post a Comment