Na Mwandishi Wetu
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), limetangaza viingilio vya mechi kati ya timu ya Taifa ya Wanawake chini
ya miaka 20, Tanzanite na Afrika Kusini, ambapo kiingilio cha chini kabisa
sh.1,000.
Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura alisema
mashabiki watakaoshuhudia mechi hiyo ya mchujo ya Kombe la Dunia watalipa
kiingilio cha chini kabisa cha sh,1,000 ili kila mmoja amudu gharama hiyo.
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano hiyo itachezwa
Jumamosi ijayo Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam kuanzia saa 10:00 jioni.
Wambura alisema kiingilio cha sh. 1,000 ni kwa viti vya rangi ya
kijani, bluu na orange. Viingilio vingine kwa mechi hiyo vitakuwa sh. 2,000 kwa
VIP C, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP A watalipa sh. 10,000.
Tanzanite chini ya Kocha Rogasian Kaijage inaendelea na mazoezi
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na ule wa Taifa kujiandaa kwa mechi hiyo.
Kambi ya Tanzanite hivi sasa imehamia Msimbazi Hotel kutoka Ruvu mkoani Pwani.
Tanzanite
wamefanikiwa kusonga mbele katika hatua hiyo baada ya mechi ya kwanza dhidi ya
Msumbiji kuwatungua mabao 10-0. Mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na ile ya
ugenini walishinda mabao 5-1, hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 15-1.
No comments:
Post a Comment